Kwanini Simba ilisitisha kuvaa nembo ya "Visit Rwanda" kwenye African Football League?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,151
7,921
Watanzania tuna hulka ya kupuuzia mambo ya msingi na kuna katabia kalijengwa na kameota mizizi ambapo ukihoji ukagusa maslahi ya watu fulani wanajaribu kukunyamazisha unaambiwa "acha ujuaji". Matokeo yake watu wanaogopa kuuliza maswali ya msingi na makosa yanajirudia kama siyo matatizo kuwa makubwa zaidi.

Siku chache tu kabla ya ufunguzi wa AFL, zilitoka taarifa kuwa Rwanda ni moja ya wadhamini wakuu wa AFL na kwamba wachezaji wa timu zote shiriki watavaa nembo ya "Visit Rwanda" katika bega.

Hii ilileta minong'ono na nakumbuka kuwakumbusha wale walioona kuwa hili ni jambo dogo msije kushangaa miaka 20 ijayo baadhi ya vitu vya Tanzania ikiwemo Dar es Salaam au hata Simba SC vikadhaniwa vipo Rwanda na itakuja kuhitajika nguvu kubwa kurekebisha huo mtazamo. Wengi hatujui Kenya walitumia mbinu gani mpaka kuiaminisha dunia kuwa Mt. Kilimanjaro uko Kenya ila inawezekana zilikuwa ni mbinu zinazofanana na hizi.

Anyway, ingekuwa vizuri tukajua nini kilipelekea Simba katika game ya marudiano kule Misri kusitisha uvaaji wa nembo hiyo na ilileta athari gani katika makubaliano yaliyokuwa yameshafikiwa kati ya Simba, TFF na waandaaji wa AFL. Unaweza kuta kwa kukiuka mkataba wa ushiriki, Simba ilipoteza haki za maokoto waliyoahidiwa kutoka AFL na yamepelekea mvurugano tunaouona sasa hivi Msimbazi. Kama hili lilitokana na shinikizo la Serikali, hili linaweza kuathiri ushiriki wa Simba na timu zingine za Tanzania katika mashindano yajayo ya AFL.

Jana Simba imekabidhiwa tuzo ya kuwa na mashabiki bora wa AFL na tuzo waliyopewa ina maandishi makubwa ya VISIT RWANDA. Popote ambapo Simba inapost picha ya tuzo hii, tunaitangaza Rwanda tena kwa ukubwa kuliko hata nembo katika jezi.

Screen Shot 2023-11-13 at 7.05.36 PM.png


Hatuwezi kujifunza kwa kufukia makosa au maamuzi kama haya chini ya kapeti. Yawekeni wazi tuyajadili kwa pamoja, hii ni nchi yetu sote. Wengine hatujabahatika tu kupata teuzi huko serikalini ila tuna mawazo yanayoweza kuisaidia nchi.

Nasubiri kuambiwa nipunguze ujuaji.
 
Umeelewa mkuu ila tusiilamu Simba ilaumu Serikali yako kwa kuzubaa Rwanda wameweka Pesa ila waptete kitu sisi huku bongo akili zetu zinawazaga Pesa za wahisani mwisho wasiku ubunifu na kuchangamkukia fursa unakua FView attachment 2812705
Sijailaumu Simba, nimeuliza nini kilitokea na kimeiathiri vipi Simba kifedha maana najua hauwezi kukiuka mkataba namna ile bila kuadhibiwa.

Tunakosa watu sahihi katika maeneo mengi muhimu yanayohitaji kufikiri kwa kina.
 
Niliuliza hili swali sikupewa majibu. Simba imepoteza kiasi gani kwa kutovaa "Visit Rwanda" katika ile game ya mwisho?

Screen Shot 2024-04-17 at 5.08.12 PM.png
 
Back
Top Bottom