Tukiacha kuficha sabuni kwenye maji, tutalinda maadili yetu

Sep 13, 2012
4
0
Na Gordon Kalulunga

Watu wa Nyikani wanatuonya kuwa hatupaswi kuficha Sabuni kwenye Maji maana itayeyuka.

Na anayeshangaa kutokuta Sabuni ndani ya Maji bali kuona povu wakati yeye aliificha hiyo Sabuni kwenye Maji nasi tunamshangaa.

Katika suala la mmomonyoko wa maadili serikali ilificha Sabuni kwenye Maji Kwa muda mrefu na sasa inashangaa povu la sabuni.

Dini ni Moja ya nguzo ya kulinda maadili. Lakini Serikali mashuleni somo la dini siyo lazima na hata wanaofaulu mitihani ya dini hawahesabiwi kuwa kuna umuhimu.

Kutowekwa mkazo kwenye masuala ya dini ni Moja ya jambo la kuficha Sabuni kwenye Maji matokeo yake ni kukutana na mapovu.

Uholela wa upatikanaji wa vileo mitaani kisa tunapata Kodi vivyo hivyo ni kuficha Sabuni kwenye maji.

Filamu zenye viashrikia vya ngono kwenye vyombo vya usafiri ni kuficha Sabuni kwenye maji.

Urahisi wa upatikanaji wa maeneo ya starehe ikiwemo Kamali ni Moja ya vielelezo vya kuficha Sabuni kwenye maji.

Inatafakarisha kupiga marufuku watoto wa Tanzania kutonunuliwa bima za Afya ila tunaruhusu uvutaji wa sigala kisa Kodi kubwa inapatikana huko.

Ikiwapendeza wenye Mamlaka na hii nchi watazame namna ya kurekebisha baadhi ya mambo haya ili kurejea Edeni.

Ndiyo maana ninasema kuwa tukiacha kuficha Sabuni kwenye Maji tutalinda maadili yetu.
 
Back
Top Bottom