Tukaribishe furaha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukaribishe furaha.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Roulette, Oct 23, 2011.

 1. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  nimegundua threads nyingi members wanaleta zinahusu matatizo na namna matatizo hayo yanasababisha matokeo katika maisha yao (au jamii, au taifa, ulimwengu etc), zaidi matokeo mabaya (negative impact). Na hili nimelikuta jukwaa karibu zote.
  Ni kweli ni muhimu kuzungumzia matatizo na kuyatafutia suluhisho ila itasaidia zaidi kama tutaweza kubadilisha mtazamo wetu kutoka matokeo mabaya kwenda matokeo chanya. Najua Great thinkers wanatakiwa kutafuta suluhisho na ni lazima wajadili the negatives in order to bring the positive, ila nadhani ni muhimu kila mtu binafsi awe na positive attitude, hata kwenye negative circumstance, na hii huhitaji kubadilisha mtazamo wetu wa maisha.

  Lengo la thread hii ni kusaidia kubadilika huko.

  1. Kuna wakati (na hii hutokea sana) umeamka asubuhi na umepanga "goals" za siku. Ikifika jioni unagundua kuna vitu hukufanikiwa kutimiza na hii inaleta frustration, unaona kama siku hiyo imepotea. Unasahau kama kuna vitu ulitekeleza na kwa utekelezaji huo unastahili kujipongeza. Ukiwa na glass imejazwa nusu, usisemi liko half empty, sema liko half full.

  2. Kuna watu wengi sasa hivi wamefikia hatua ya kutojua ni vitu gani wanapenda, ila wanajua na hutaja sana vitu wasivo vipenda. Kutambua vitu vyenye kukuletea furaha nido mwanzo wa kukaribisha furaha. Binafsi napenda sana kucheza na watoto karibu na maji (iwe maji ya mpira wakati wa kuosha gari, iwe beach, swiming pool au hata kwenye bath tube). Kazi yangu ni ya safari kwa hivo mara nyingi nashindwa kufanya hivi vitu ila kila niwezapo, nachukulia nafasi ya kuvifanya sana na baadae nikija kuvimiss nakumbukia na inatosha kurudisha furaha.
  3. Kumbu kumbu ni kitu muhimu katika kukaribisha furaha maishani mwetu. Matatizo ni sehemu ya maisha na tunatakiwa kukabiliana nayo tukiwa na nguvu. Nguvu hiyo itatokea kwenye kumbu kumbu ya siku za furaha. Mfano, ukihisi hali ya upweke, kumbu kumbu ya siku ulikua na watu uwapendao inaweza kutosha kurudisha furaha moyoni. Sio kukumbuka na kusema: siku zile nilikua na watu ila leo niko peke yangu, bali nikukumbuka kua wakati ulipata fursa ya kufurahia kuwepo kwa watu uwapendao ulifurahia kwa kiwango kikubwa na furaha hiyo imebaki moyoni mwako ili uweze kuitumia utakapo wakosa karibu yako.
  4. Sababu za kufurahi ni nyingi sana. Kuna watu wanasema maisha kwao hayana maana sababu wanahishi tabu tupu. Ukimuuliza ni tabu gani anasema mume wake anatembea nje, au anaumwa ugonjwa usio pona na kadhalika. Anasahau hicho kitu kinacho mnyima raha ni sehemu moja tu ya maisha, na wala sio maisha yenyewe. Uhai ni chanzo cha furaha. Kuona mbingu, ardhi na chochote ilicho kati ya mbingu na ardhi ni furaha. kua na afya ni furaha, kua na watoto ni furaha. Kula chakula, kulala ndani ya nyumba, kazi, marafiki, familia, imani nakadhalika, vyote vinaweza kua vyanzo ya furaha, kama utavitambua kua vinakufurahisha na kama utaamua kukaribisha furaha maishani mwako.

  5. Kukaribisha furaha ni rahisi na hakuhitaji kua msomi, haihusiani na hali ya uchumi, jinsia, kabila au miaka, haichukui muda wako na haitegemei watu wa nje kuhusika (ingawa hii itasaidia). Kama nilivo sema mwanzo ni swala la kujiamulia, kujua ni vitu gani vinakuletea furaha na kutenda hivyo vitu kila uwezapo, ni kukumbuka vitu vinavyo kuletea furaha zaidi na kujifunza namna ya kuona positive zaidi ya negative katika maisha.

  Vitu hivi vitasaidia kuanza kubadilisha mtazamo wako wa maisha na kukaribisha furaha maishani mwako, ila kuna mengine mengi unahitaji kufanya kwa kuimarisha furaha... Natumai kuna member atapost zaidi kuhusu kuimarisha furaha. Asanteni
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  6. Mtazame aliye chini yako kuliko kujilinganisha na aliye juu yako: Mara nyingi huwa tunadefine furaha zetu kwa kulinganisha na wale walio juu yetu. "Yeye anakula milo mitatu, mimi mmoja. Yeye ana gari, mimi sina. Wenzangu wana waume/wake/ wachumba na familia zao, mimi sina"
  Kwa nini hujilinganishi na asiyekula hata huo mlo mmoja kwa siku, ambaye hana miguu ya kutembelea, mtoto wa mitaani ambaye hajui wazazi wake wako wapi?

  Tunapima furaha kwa mali na afya? Wangapi wana afya njema, wana mali nyingi na hawana furaha? Huwaoni wagonjwa hospitali waliosota kitandani miaka na miaka na bado wakiamka neno lao la mwanzo ni "ninamshukru Mungu niko hai". Huwaoni masikini wanahangaika na cha kutia mdomoni, wakipata wanashukuru, wakikosa wanashukuru?

  Tajiri si yule aliye na vingi bali anayetosheka na vichache. Furaha yako ni kutosheka kwako na ulichonacho, kutosheka kwako na hali uliyonayo.
   
 3. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Very relevant Mamamia. Asante kwa mchango wako.
  Wakati mngine tunatami vitu ili watu wa nje waone mafanikio yetu ila moyoni labda hatuhitaji hivyo vitu. Mi nimegundua naweza kabisa kuhishi bila gari. Kweli sina gari ila nimefikiria sana na nimeona hata nikiweza kununua gari, sihitaji gari. Bahati mbaya, dunia ya leo, ukipata ka senti kadogo, badala ya kuinvest katika kitu muhimu kwako, kinacho weza kukuletea furaha, unainvest katika vitu vinavyo wafanya watu wa nje wakuone umefanikiwa... na vile vile, mafanikio ya watu wa nje zinakua ni chanzo cha frustration na unaishia kusahau vile unavyo kwa kufikiria vile ambavyo huna/hujapata (point number 2)
  Umeongea point aisee...
   
 4. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nayafahamu sana mambo yanayonifurahisha na najaribu kuyatekeleza licha ya kutingwa na muda ila kila wakati mama watoto anaondosha furaha hiyo. teh. yote kwake yanamkera. nimejaribu kuzoea mazingira saivi kukasirika kwa mke wangu ndiyo furaha yangu....
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nimependa maneno yako Roulette... They are constructive na nimeshindwa kuelewa why wahehamisha the thread from its original position, enways labda hapa imeonekana more appropriate....

  I deeply believe kua kukaribisha furaha pia ni rahisi kama wale walokuzunguka (hasa your loved ones and close friends are happy).... Kuna watu ambao they are not good at expressing themselves kabisa thou they do need wakaribu (for believe me you - everybody needs someone once in a while). Wanadamu tukiwa wakujali... Kujijali yalo ya msingi na kujali wa karibu yako in what ever condition or circumtances hutujenga kuweza karibisha furaha... Sio furaha tu ilokuzunguka you as an individual but as a whole.... You, Your Loved ones na Ndugu na jamaa.... Ni muhimu mno.
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimependa sana adaptation strategy yako ila ningekushauri ujaribu kujifunza ni vitu gani vinamfurahisha mwenzio, ndio uvifanye kua vyanzo vya furaha yako pia. Kama vile unaweza kusoma kwa AshaDii (thank you dear kwa mchango) furaha sio kupokea tu, furaha ni kutoa pia na ndio maana ya upendo. Ukimpenda mtu na ukampa furaha, furaha yake inatosha kwa kukufanya uwe happy. Na kuna wakati unakuta kuna kitu hujafurahia sana kukifanya na matokeo yake ya palepale hayakukufurahisha ila ukiona mtu umpendae kafurahi sana na hicho kitu unajazwa na furaha pia.

   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  It was like nilimsoma Ze burner but wanted to know you Opinion first... Nimeipenda... BUT Roulette i think hapa kwa huyu jamaa tatizo ni kubwa... I believe kua mtu yeyote aniudhi... na mtu yeyote asinielewe BUT not my better half... I can feel ni nini anasema... Imagine unarudi home yule ambae ndo wakukuongezea furaha, daima hakuna kitu waweza fanya ambalo ni bora kwake... Waweza kua depressed believe me. Na naamini no matter how hard atake kukaribisha furaha ni kazi bure kama kwanza hatatatua tatizo alonalo na Mkewe... Yawezekana kweli Ze burner anakosea... OR yawezekana The wife ndo matatizo yapo hapo.... Ila tu kweli anahitaji ku-apply nguvu ya ziada kuweza karibisha na kupata hio furaha... What do you think kuhusu hili??

  Ze burner umewahi keti na mkeo mkaongea hili jambo?
   
 8. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Self-realization, the awareness of one's nature and the development of one's talent, is the surest path to happiness( Ideas of The Great Philosophers). Uhappiness and frustration are caused by unrealized potential of a person leading to failed goals and poor life!! According to Aristotle, "when a person acts in accordance with his nature and realizes his full potential, he will do good and be contented."
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Russian barikiwa kwa hii post. Binafsi Katika maisha yangu siku zote hupigania kuwa na furaha.
   
 10. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mhh! Mkuu usimwache mama watoto akasirike bana. Jitahidi awe na furaha, ili furaha yake iwe ni sehemu ya furaha yako pia.
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Aisee RR umenikumbusha jambo, kuna kipindi nilikuwa naipa furaha kipaumbele lakini katika siku hizi za karibuni mambo yananiendea taratibu na naona furaha yangu ina-decline siku hadi siku :(

  Will do something to recover my Furaha aisee!!!
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  you are what you think.....
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
 14. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hi Tanmo. Nafurahi kuona kua at least wewe uikua umesha amua kuipa furaha kipaumbele, kwa hiyo zoezi la kurudisha furaha katika maisha yako halitakua ngumu sana. Naamini kitu kingine cha kufahya ni
  8. Shirikiana na watu wenye kuipa furaha yao (na yako) kipaumbele (I love the sound of this word...). Jaribu kuhepuka watu wenye hasira na uzuni au malalamiko, na kama hawahepukiki waambie kuhusu uamuzi wako wa kua mwenye furaha kila wakati na wakaribishe kuijunga na wewe katika hilo zoezi.
   
 15. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Thanks The Finest... I like it when she says...
  I've lived to be
  The very best
  I want it all
  No time for less
  I've laid the plans
  Now lay the chance
  Here in my hands

  Give me one moment in time
  When I'm more than I thought I could be
  When all of my dreams are a heartbeat away
  And the answers are all up to me
  Give me one moment in time
  When I'm racing with destiny
  Then in that one moment of time
  I will feel
  I will feel eternity

  You're a winner for a lifetime
  If you seize that one moment in time
  Make it shine
   
Loading...