Tujuzane

Tujuzane

jimmykunchi

Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
33
Reaction score
10
Wasalaam wana MMU...

Mimi ni MUPYA humu, lakini sio mgeni! Sijui hata kama hiyo ina make sense lakini ndo hivyo. Nasema sio mgeni kwasababu nimekua nikija humu kwa lengo la kujifunza kutoka kwenu toka nilipojiunga September. Katika pitapita zangu nimegundua mengiiii...vile vile baadhi wa members wamekua common machoni mwangu, so nimeshazizoea hizo usernamez zao.

Yeah yeah...najua tayari wapo walioanza kusema hii sio sehemu ya kutuandikia mambo yako binafsi moyoni mwao sahivi...but c'mon, I know! Just bear with me.

I'm on my early 20s kwahiyo wanaonizidi humu ni wengi tu lakini najitahidi hii post isichore mduara kwa watu wa rika fulani tu.

Nataka kuitumia ile 'U' ya kwenye 'MMU' tuongee kama marafiki kwenye hili suala zima la kumuhukumu mtu usiyejuana nae. Naongelea kumuhukumu mtu kwa kumsema kutokana na neno au tendo alilolifanya (i mean giving your opinion the hard way, to be more specific).

Unajua mimi, wewe na yule tumekulia na kulelewa katika mazingira tofauti tofauti. Tumejikuta tukiwa na tabia pamoja na maana za maneno kama 'kitu cha ajabu' na 'kitu cha kawaida' tofauti tofauti. Hivyo basi kutokana na hiyo misingi tumejikuta tukijengeka na kuwa watu wa aina flani kitabia. Sasa akitokea mtu (a stranger) akafanya au kusema kitu cha ajabu kwako mkiwa kwenye mkusanyiko fulani halafu wewe ukaamua kumjia juu hapo hapo bila kujali kuwa yeye kapitia yapi hadi kufika hapo alipo ni sawa??
-Au tuwe tunawafumbia macho tu kwasababu hatujui lolote kuhusu mambo waliopitia??
-Au tuwe tunawajia taratibu kwa kuwa sio kosa lao kukosa malezi uliyopata wewe??
-Je, "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu" na uwezo wa kila mwanadamu wa kawaida kutambua jema na baya vinatupa haki ya kuwanyoosha papo hapo wavukao mipaka from our point of view??

*Ningetoa mfano lakini nimehisi ntachukua muda wako mwingi hapa. Nadhani hicho kimetosha kukujengea picha ya ninachokiongelea na naamini mifano tunayo vichwani mwetu as tumeshakutana nayo.

Tujuzane maoni yako juu ya hilo...
 
Mwanzo mzuri kijana.
cc nani na nani?
 
Gazeti lako zuri,, ngoja niendelee kunywa chai yng baridi itaniua..
 
Nadhani asilimia kubwa ya jamii ni waumini wa dini maana yake wanaamiki uwepo wa mungu na kufuata yale aliyotuamuru tufuate pamoja na kulelewa katika mazingira tofauti bado dini zetu zinamfunzo sawa juu ya matendo mabaya na mema ndo maana ukifanya kitu cha ajabu lazima jamii ikushangae na kukujia juu kwa imani ya kuwa unafanya makusudi na si kwamba haujui au ndo ulivyozea sidhani kama kuna jamii inaruhusu lugha ya matusi sasa ukitumia hiyo lugha usidhani kama kuna mtu atakujia kwa upole maana tunaamini unaishi katika jamii hii hii ambayo hiyo lugha haihitajiki,suala la asiyefunza na mama hufunza na ulimwengu maana halisi sidhani kama ilikuwa kwa mama mzazi kwa mtazamo wangu nadhani ni kwa jamii uliyokulia,kuna watu wamezaliwa tu then wazaz wao wakawa wamepoteza dunia sasa kwa hao wangkuwa na sababu kuwa mbona mimi sina mama so ni ruhusa kufanya lolote haiko hivyo ndo maana hata hapa ukiongea ujinga kila mtu atakujia juu maan ni sehemu ya jamii.
 
080106-0050.jpg
 
mimi sijaona chochote kipya ulicho andika, labda ungeweka huo mfano wako ndo ingekuwa na maana kidogo
 
Too long sijamaliza kusoma ,wakunisamaraizia pls.
 
Cha muhimu ni kutoa msaada,
Kuonya,
Kuelekeza,
Kufafanua,
Kuelewesha,
Na
Kurekebisha kwa USAHIHI
mtu aliye fanya jambo lisilo kubalika ktk jamii...🙂🙂
 
I typed it on pc it looked fine..didn't know its that long.
I'm using a phone right now and i got to agree with you its way too long..!!
 
Back
Top Bottom