MIDFIELD
JF-Expert Member
- May 27, 2013
- 1,944
- 703
Heshima kwenu Great Thinkers.
Kwa muda sasa, kumekuwa na matukio kadhaa yanayohusisha majambazi kuvamia vituo vya polisi na kuua askari pamoja na kuondoka na silaha. Hali hii toka mwaka jana imejitokeza Mkuranga zaidi ya mara mbili au tatu ktk vituo tofauti, Rufiji, Ushirombo n.k. Cha kushangaza, hali hii imeanza kujitokeza hata kwa wananchi wanaojiita wenye hasira kali kuvamia vituo vya polisi na kuchoma moto au kuharibu mali kama ilivyojitokeza juzi huko Bunju, lakini siyo bunju tu, kuna sehemu zingine sikumbuki vizuri kwa mnaokumbuka mtatukumbusha, wananchi kuvamia vituo vya polisi.
Sasa tujiulize ni tafsiri gani tunaipata kwa matukio haya. Je, watu sasa hatuhitaji huduma za polisi! Je, ni ugaidi unaanza kujitokeza katika nchi yetu!! Je, hawa wanaosema wanahasira kali ni kweli au ni wahalifu chini ya kivuli cha wananchi wenye hasira kali!! Je, sisi kama wananchi wenye mapenzi mema na nchi yetu tunachukuliaje mambo haya na wajibu wetu ni nini? Na je, ni nini mwisho wa haya mambo!!
Karibuni tujadili kwa pamoja.