Tujiulize maswali haya juu ya uporaji wa SILAHA

Tujiulize maswali haya juu ya uporaji wa SILAHA

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Hii hali ya polisi kuporwa silaha vituoni inatisha sana kwa sasa.
Hapa kuna maswali machache nimejiuliza bila majibu

1.Ni kwanini waporaji hupendelea vituo vya mjini tu?Hususani Dar na Pwani

2.Kwa nini waporaji hawajishughulishi na vituo vya wilayani huko mkoani,Ingali kwao inakuwa rahisi kutoroka?

3.Kwa nini wanatumia riski kubwa kupora hizo silaha ukizingatia tetesi zilizopo zipo silaha haramu zinauzwaga kwa bei rahisi?

Hili ni jambo la kufanyia utafiti na uchunguzi wa kina,Inawezekana nyuma ya huu uharamia lipo jambo kubwa limejificha.
 
Natamani waje wamarekani wachunguze hili tukio la ukonga lilenickitisha sn
 
Kibo10

1. Mijini watu ni wengi na hivyo ni rahisi kujichanganya na watu wema na wasijulikane. Vituo vya mijini pia vina silaha nyingi zaidi na pengine za kisasa zaidi kuliko mikoani.

2. Wilayani na vijijini ni rahisi sana kujua wageni. Hata magari huwa ni machache na hivyo kufanya tracing inakuwa rahisi sana kama kuna uhalifu umetokea. Na hata uchache wa watu unafanya utambuzi wa wageni na kutiliwa mashaka kuwa rahisi sana. Dar, kwa mfano, sio ajabu kukuta shughuli mbalimbali zikiendelea usiku kucha na hivyo kukutana na watu usiku sio jambo la kutilia mashaka sana kama ilivyo kwa sehemu nyingine.

3. Hizo silaha haramu mara nyingine zinakuwa incomplete. Hizo za vituoni ni complete na wanaweza kuzipata pamoja na risasi zake. Mara nyingi matukio haya huambatana na wahusika kupata habari za ndani kuhusu nani ni nani, wapi ni wapi, na timing. Kwa tukio kama la jana, siwezi kushangaa kama kuna baadhi ya polisi wakawa wanahusika. Kama unavyosema, risk ni kubwa kwa hivyo ili wawe tayari kuibeba ni lazima kuwe na uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kupata wanachohitaji.
 
Last edited by a moderator:
yani kwa namna yoyote ile hawapolic wanajuana kabisa huwezi toka uko umedhamiria eti kuiba sila na ku uwa tena kirahisi namna hi bila kuwa na mikono ya police tena mpaka wanajua hi ni store ya sila. kikawaida sio raisi msitufanye tukose amani nyie mapolice. mana nyie mna vamiwa sisi rai tutaponaje sasa kwa hali hiyo?
 
Nakubaliana nawe point ya 3 ni risk ya kupora silaha kituo cha police na kuua police na raia, kwa kitu ambacho mtaani kinapatikana haileti maana, nami huwa najiuliza hilo swali!
may be hawajui silaha zilipo but pro yeyote lazima ajue na hawezi kuwa amateur na bado akaenda kuua na kuiba kituo cha police! Aisee bado sipati jibu!
 
Kibo10

1. Mijini watu ni wengi na hivyo ni rahisi kujichanganya na watu wema na wasijulikane. Vituo vya mijini pia vina silaha nyingi zaidi na pengine za kisasa zaidi kuliko mikoani.

2. Wilayani na vijijini ni rahisi sana kujua wageni. Hata magari huwa ni machache na hivyo kufanya tracing inakuwa rahisi sana kama kuna uhalifu umetokea. Na hata uchache wa watu unafanya utambuzi wa wageni na kutiliwa mashaka kuwa rahisi sana. Dar, kwa mfano, sio ajabu kukuta shughuli mbalimbali zikiendelea usiku kucha na hivyo kukutana na watu usiku sio jambo la kutilia mashaka sana kama ilivyo kwa sehemu nyingine.

3. Hizo silaha haramu mara nyingine zinakuwa incomplete. Hizo za vituoni ni complete na wanaweza kuzipata pamoja na risasi zake. Mara nyingi matukio haya huambatana na wahusika kupata habari za ndani kuhusu nani ni nani, wapi ni wapi, na timing. Kwa tukio kama la jana, siwezi kushangaa kama kuna baadhi ya polisi wakawa wanahusika. Kama unavyosema, risk ni kubwa kwa hivyo ili wawe tayari kuibeba ni lazima kuwe na uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kupata wanachohitaji.

Majibu yako hayaridhishi! Majambazi sio rahisi kukosa silaha za kufanyia uhalifu. Na hawana tabia ya kuvamia vituo vya polisi kuiba silaha! Kuna siri kubwa nyuma ya huu uvamizi! Hakika sio majambazi wa kawaida.
 
yani kwa namna yoyote ile hawapolic wanajuana kabisa huwezi toka uko umedhamiria eti kuiba sila na ku uwa tena kirahisi namna hi bila kuwa na mikono ya police tena mpaka wanajua hi ni store ya sila. kikawaida sio raisi msitufanye tukose amani nyie mapolice. mana nyie mna vamiwa sisi rai tutaponaje sasa kwa hali hiyo?

Polisi wooote wako kaunta wakisubiri kodi ya hiari; maana yake kwa nje hakuna ulinzi wa kituo! Sijawahi ona hata kidogo ulinzi wa namna hii!
 
yani kwa namna yoyote ile hawapolic wanajuana kabisa huwezi toka uko umedhamiria eti kuiba sila na ku uwa tena kirahisi namna hi bila kuwa na mikono ya police tena mpaka wanajua hi ni store ya sila. kikawaida sio raisi msitufanye tukose amani nyie mapolice. mana nyie mna vamiwa sisi rai tutaponaje sasa kwa hali hiyo?
Kuvamia kitua cha polisi Tanzania ni rahisi sana sana. Vituo vingi havikujengwa kitaalam na inavyotakiwa. Huwezi kujenga kituo cha polisi kama bar na stoo ya silaha kama godown la kuwekea bia halafu watu wapate ugumu kuvamia. Nenda nchi nyingine uone vituo vya polisi vilivyojengwa ndio utajua namaanisha nini. BTW hawa wavamizi sio majambazi wa kawaida. Mnakumbuka walitaka kumnyang'anya silaha mwanajeshi aliyekuwa kwenye lindo? (yule aliyepewa nishani). Kuna kikundi kipo kimeshapata mafunzo sasa kipo kwenye hatua ya pili... na kitakopofika hatua ya tatu ndio itakuwa hatari sana sana
 
Mimi nahisi ni hasira tu za hayo majambazi labda walishateswa kwenye hicho kituo kwa makosa mbalimbali waliyofanya siku za nyuma sasa wameamua kulipiza kisasi

Vimevamiwa vituo vingapi? Wamevamiwa askari wangapi wakiwa na silaha ili wazipore? Hakuna mwanajeshi aliyevamiwa akiwa kwenye lindo?
 
hawa si majambazi wa kawaida .hawa ni magaidi kabisa na lengo lao si tu kupata siraha bali pia kuleta hofu.

Kwenye IHL tunaita ''Intimadation/terrifying acts''
Kutakuwa siri nzito tunaomba uchunguzi ufanyike maana hatujui usalama wetu wananchi wa kawaida ukoje
 
Nikipata muda nitaandika niyajuayo kuhusu uvamizi huu uliokithiri,tatizo ni kuwa wananchi wakijua ukwel huwa tuna-panic hivyo kufanya hatua ya kwanza/lengo la kwanza la hawa wadudu kutimia
 
Kwenye IHL tunaita ''Intimadation/terrifying acts''
Kutakuwa siri nzito tunaomba uchunguzi ufanyike maana hatujui usalama wetu wananchi wa kawaida ukoje

ni kweli mkuu.usalama wa taiga wako dodomaaaaa
 
Kwa hali ya usalama ilivyo sasa hivi,Wananchi lazima tulipe jeshi letu la polisi ushirikiano wa kutosha.La sivyo maisha yetu na mali yatakuwa hatarini sana.
Kwangu mimi binafsi toka tukio la kituo cha Staki shari limetokea ni kama nimeathirika kisaikolojia maana hata nikiona bodaboda pembeni ya gari langu ninapokuwa kwenye foleni ninapata msituko sana.
Imenibidi kwa kweli nirudi nyumbani mapema kwa hofu,Moyo wangu hauna amani tena.
Ni lazima tuungane kulaani na kusaidia taarifa zozote zitakazo saidia watu kama hao kukamatwa ili roho za wasamaria wema na polisi wetu zisiendelee kupote bila sababu"Ni hatari"
 
Back
Top Bottom