Tujiulize hivi hizi juhudi kubwa za kuwatoa kwa hila wabunge wa Chadema nia yake ni nini?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,485
30,157
Hakika siyo siri tena kuwa serikali ya utawala wa awamu ya tano inafanya juhudi kubwa sana kuwafuta kwa hila wabunge wa upinzani, hususani Chadema

Tumeona wabunge wa Chadema "wakinunuliwa" ili wahame kutoka Chadema na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuleta maendeleo

Hata hivyo juhudi hizo ni kinyume kabisa na faksafa anayoitangaza Rais mwenyewe kwenye majukwaa ya kisiasa, kuwa maendeleo hayana chama

Tumeshuhudia wabunge kadhaa wa Chadema wakihama chama chao cha Chadema na kujiunga na CCM na kupitishwa "automatically" kuwa wagombea tena wa ubunge

Tumeona pia juhudi kubwa za hawa wakereketwa wakubwa wa CCM, maDED waliopigwa chini na mahakama kuu, kuwa hawastahili kuendelea kusimamia chaguzi zozote za hapa nchini, wakiwatangaza wagombea hao waliohamia CCM wakipita bila kupingwa!

Kumekuwepo pia na juhudi kubwa "kuwapunguza" kwa hila mbalimbali wabunge wa Chadema waliochaguliwa na wananchi wao kwenye majimbo yao

Tulianza kuona hizi hila zikifanywa kumwondoa kwenye ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari

Lakini lililostua dunia mzima, ni huu uamuzi wa majuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa Ndugai wa kumvua ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa madai kuwa ni mtoro na yeye Spika, hajui Tundu Lissu alipo!

Hivi ni nani katika dunia hii asiyejua Tundu Lissu alipo, isipokuwa yeye Spika peke yake??

Kila mtu anafahamu namna Tundu Lissu alivyomiminiwa risasi zaidi ya 38 kwenye gari lake, kwenye makazi ya viongozi wa serikali, tena mchana kweupe, na risasi 16 kumuingia mwilini mwake

Lakini kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, amemuokoa na kifo, ambacho hao watesi wake walikuwa wamekipanga kwa Lissu

Miongoni ya watu waliokwenda kumwona Dodoma hospital, alikokimbizwa baada ya kupata majetaha hayo, alikuwa ni Spika mwenyewe

Kutokana na hali aliyokuwa nayo, ilibidi uamuzi wa dharula uchukuliwr siku hiyo ya tarehe 7/9/2019 wa kumuhamishia hospitali ya Agakhan jijini Nairobi, huku Spika mwenyewe akiunga mkono uamuzi huo

Sasa ninachojiuliza iweje leo Spika Ndugai, adai kuwa hajui akipo, Mheshimiwa Tundu Lissu??

Ni dhahiri hizi ni njama za wazi za serikali hii ya utawala wa awamu ya tano, ya kutaka kuwapungiza wabunge hao waliochagiliwa na wananchi katika majimbo yao

Swali la msingi ambao sisi wananchi tunajiuliza ni hilo, hivi hizi juhudi kubwa sana xinazofanyika na Bunge letu la kuwapungiza wabunge wa kuchaguliwa na wananchi, lengo lake halisi ni nini??

Naomba mwenye kujua lengo hilo anijuze na Mimi ili nielewe
 
Kuthibitisha kuwa hizi ni hila za serikali hii ya awamu ya tano ni kuwa mbona wabunge wa CCM hawafanyiwi kama wanavyofanyiwa wabunge wa Chadema??

Tujiulize yuko wapi mbunge wa CCM, Nimrod Mkono wa Musoma vijijini??

Huyu mbunge ni zaidi ya mwaka mmoja sasa, watanzania hatujui aliko, mbona Spika Ndugai hachukui hatua alizomchukulia Mbunge Lissu, ambaye kila mtu katika dunia hii anajua kuwa yupo nchini ubelgiji akitibu majeraha makubwa, baada ya kumimiwa risasi zaidi ya 38 kwenye gari lake na watu wasiojulikana??

Mbona utekelezaji wa sheria wa serikali hii ya utawala wa awamu ya ya tano una "double standards" za hali ya juu??
 
Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba Bunge ni taasisi na siyo mtu binafsi. Kama ni taasisi basi ina taratibu na sheria zake. Spika kujua Tundu Lissu alipo hakufanyi sheria na taratibu za Bunge kuvunjwa au kutofuatwa. Tundu Lissu alipomiminiwa risasi hakuna aliemfukuza ubunge, kila mtu aliona hali tete aliyonayo na Bunge lilishiriki kwa namna moja au nyingine kuokoa uhai wake akiwa Dodoma. Japo chama chake baadae kiliamua kufuata utaratibu mwingine wa matibabu yake.

Kilichopelekea Bunge kuchukua hatua sasa, siyo tu kutojua Lissu alipo bali hata taarifa rasmi ya maendeleo ya matibabu yake haijulikani. Mara kadhaa Lissu ameombwa kufuata taratibu za kisheria kuhusu kutoa taarifa ya hali ya matibabu yake kwa muajiri wake lakini kutokana na kiburi amegoma kufanya hivyo. Badala yake amekua akilitaka Bunge kama linahitaji taarifa hiyo, likaombe kwa madaktari wanaomtibu. Sasa, hii ni dharau kubwa sana kwa taasisi kubwa kama ya Bunge.

Kiutaratibu mtumishi yoyote awe wa umma au sekta binafsi, anapoumwa au kuwa na dharura ya matibabu hasa ya muda mrefu, anapaswa yeye ndo atoe taarifa kwa muajiri wake na siyo muajiri kuanza kutafuta taarifa zake. Isitoshe matibabu ya Lissu hayagharamiwi na bunge hivyo ni ngumu kujua kama huyu mtu amepona au bado anaumwa. Hasa ukizingatia pia mwenendo wake, siyo kwamba yupo hospitali amelazwa mahututi kama ilivyokua mwanzo bali anaonekana akisafiri nchi mbalimbali na kufanya mahojiano na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii. Hii inaleta tafsiri kwamba Afya yake imeimarika kwa kiasi kikubwa kuweza kutekeleza majukumu yake ya kibunge. Lakini hajawahi kuonekana bungeni wala kutoa taarifa yoyote.

Jambo lingine la kushangaza, watu wengi wamekua wakilaumu Lissu kufukuzwa ubunge kwa kuangalia sababu moja tu ya kutotoa taarifa za maendeleo matibabu yake. Lakini wanaiacha kwa makusudi sababu nyingine ya msingi ambayo imetajwa kikatiba nayo ni kutotoa taarifa ya Mali na Madeni kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ukisoma ibara ya 71 (1)(c)(d) ya Katiba inasema wazi kabisa kwamba mbunge atakoma ubunge au ataacha kiti chake endapo (c) atakosa kuhudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika na (d) itathibitishwa amevunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Yote haya Lissu ameenda kinyume nayo, Sasa kwanini asipoteze ubunge wake? Yeye ni nani mpaka awe juu ya Sheria na Katiba.
 
Hakika siyo siri tena kuwa serikali ya utawala wa awamu ya tano inafanya juhudi kubwa sana kuwafuta kwa hila wabunge wa upinzani, hususani Chadema

Tumeona wabunge wa Chadema "wakinunuliwa" ili wahame kutoka Chadema na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuleta maendeleo

Hata hivyo juhudi hizo ni kinyume kabisa na faksafa anayoitangaza Rais mwenyewe kwenye majukwaa ya kisiasa, kuwa maendeleo hayana chama

Tumeshuhudia wabunge kadhaa wa Chadema wakihama chama chao cha Chadema na kujiunga na CCM na kupitishwa "automatically" kuwa wagombea tena wa ubunge

Tumeona pia juhudi kubwa za hawa wakereketwa wakubwa wa CCM, maDED waliopigwa chini na mahakama kuu, kuwa hawastahili kuendelea kusimamia chaguzi zozote za hapa nchini, wakiwatangaza wagombea hao waliohamia CCM wakipita bila kupingwa!

Kumekuwepo pia na juhudi kubwa "kuwapunguza" kwa hila mbalimbali wabunge wa Chadema wa kuchaguliwa na wananchi wao kwenye majimbo yao

Tulianza kuona hizi hila zikifanywa kumwondoa kwenye ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari

Lakini lililostua dunia mzima, ni huu uamuzi wa majuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa Ndugai wa kumvua ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa madai kuwa ni mtoto na yeye Spika, hajui Tundu Lissu alipo!

Hivi ni nani katika dunia hii asiyejua Tundu Lissu alipo, isipokuwa yeye Spika peke yake!

Kila mtu anafahamu namna Tundu Lissu alivyomiminiwa risasi zaidi ya 38 kwenye gari lake, kwenye makazi ya viongozi wa serikali, tena mchana kweupe

Lakini kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, amemuokoa na kifo, ambacho hao watesi wake wakikuwa wamekipanga kwa Lissu

Miongoni ya watu waliokwenda kumwona Dodoma hospital, alikokimbizwa baada ya kupata majetaha hayo, alikuwa ni Spika mwenyewe

Kutokana na hali aliyokuwa nayo, ilibidi uamuzi wa dharula uchukuliwr siku hiyo ya tarehe 7/9/2019 wa kumuhamishia hospitali ya Agakhan jijini Nairobi, huku Spika mwenyewe akiunga mkono uamuzi huo

Sasa ninachojiuliza iweje leo Spika Ndugai, adai kuwa hajui akipo, Mheshimiwa Tundu Lissu??

Ni dhahiri hizi ni njama za wazi za serikali hii ya utawala wa awamu ya tano, ya kutaka kuwapungiza wabunge hao waliochagiliwa na wananchi katika majimbo yao

Swali la msingi ambao sisi wananchi tunajiuliza ni hilo, hivi hizi juhudi kubwa sana xinazofanyika na Bunge letu la kuwapungiza wabunge wa kuchahiliwa na wananchi, lengo lake halisi ni nini??

Naomba mwenye kujua lengo hilo anijuze na Mimi ili nielewe
Tunatakiwa kubaki na chama kimoja tu...
Tunatakiwa kuwa na wabunge wasiohoji chochote kinachostahili kuhojiwa...
Tunatakiwa kuitikia wimbo wowote tunaoimbishwa hata kama hatujui kiitikio chake...
Daah mambo ni mengi muda mchache...
 
Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba Bunge ni taasisi na siyo mtu binafsi. Kama ni taasisi basi ina taratibu na sheria zake. Spika kujua Tundu Lissu alipo hakufanyi sheria na taratibu za Bunge kuvunjwa au kutofuatwa. Tundu Lissu alipomiminiwa risasi hakuna aliemfukuza ubunge, kila mtu aliona hali tete aliyonayo na Bunge lilishiriki kwa namna moja au nyingine kuokoa uhai wake akiwa Dodoma. Japo chama chake baadae kiliamua kufuata utaratibu mwingine wa matibabu yake.

Kilichopelekea Bunge kuchukua hatua sasa, siyo tu kutojua Lissu alipo bali hata taarifa rasmi ya maendeleo ya matibabu yake haijulikani. Mara kadhaa Lissu ameombwa kufuata taratibu za kisheria kuhusu kutoa taarifa ya hali ya matibabu yake kwa muajiri wake lakini kutokana na kiburi amegoma kufanya hivyo. Badala yake amekua akilitaka Bunge kama linahitaji taarifa hiyo, likaombe kwa madaktari wanaomtibu. Sasa, hii ni dharau kubwa sana kwa taasisi kubwa kama ya Bunge.

Kiutaratibu mtumishi yoyote awe wa umma au sekta binafsi, anapoumwa au kuwa na dharura ya matibabu hasa ya muda mrefu, anapaswa yeye ndo atoe taarifa kwa muajiri wake na siyo muajiri kuanza kutafuta taarifa zake. Isitoshe matibabu ya Lissu hayagharamiwi na bunge hivyo ni ngumu kujua kama huyu mtu amepona au bado anaumwa. Hasa ukizingatia pia mwenendo wake, siyo kwamba yupo hospitali amelazwa mahututi kama ilivyokua mwanzo bali anaonekana akisafiri nchi mbalimbali na kufanya mahojiano na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii. Hii inaleta tafsiri kwamba Afya yake imeimarika kwa kiasi kikubwa kuweza kutekeleza majukumu yake ya kibunge. Lakini hajawahi kuonekana bungeni wala kutoa taarifa yoyote.

Jambo lingine la kushangaza, watu wengi wamekua wakilaumu Lissu kufukuzwa ubunge kwa kuangalia sababu moja tu ya kutotoa taarifa za maendeleo matibabu yake. Lakini wanaiacha kwa makusudi sababu nyingine ya msingi ambayo imetajwa kikatiba nayo ni kutotoa taarifa ya Mali na Madeni kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ukisoma ibara ya 71 (1)(c)(d) ya Katiba inasema wazi kabisa kwamba mbunge atakoma ubunge au ataacha kiti chake endapo (c) atakosa kuhudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika na (d) itathibitishwa amevunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Yote haya Lissu ameenda kinyume nayo, Sasa kwanini asipoteze ubunge wake? Yeye ni nani mpaka awe juu ya Sheria na Katiba.
Kuna tofauti kati ya binadamu na mtu. Sio kila binadamu ni mtu. Kila mtu ni binadamu. Wewe ni binadamu tu. Binadamu ni mnyama tu kama wanyama wengine. Sheria zipo binadamu wawe watu. Sheria inayomfanya mtu kuwa binadamu tu ni batili. Mashauri kwa Mbowe na Matiko alitumia vifungu vya sheria! Rumanyika alitumia nini? Tofauti kuu ni kwamba mmoja ni binadamu na mwingine ni mtu! Sheria zipo kuhudumia mtu.
 
Lissu kiburi chake kimemponza, uwezo wa kutoa taarifa alikuwa nao na alikuwa anajua anatakiwa afanye hivyo ila kwa maksudi tu ili kuonyesha kibri na kutojali amegoma kuwasilisha taarifa zake.

Kama mtu ana uwezo wa kufanya media tour kutoka bara moja hadi jingine, nchi mbalimbali Ulaya kwa nini ashindwe tu kuandika barua ya status ya maendeleo yake?
 
Uko sahihi sana, basi ni sawa kwa wale wengine wanaosema kutokusakwa kwa walimoshambulia Lissu ni kibri cha mkulu kwani ndio mshukiwa mkuu?
 
Hilo la kwako, mimi nachojua Lissu kibri chake tena cha kitoto ndio kimesababisha ubunge wake kukoma. Kuna kitu watanzania hawajifunzi, kuheshimu mamlaka, mamlaka ipo kisheria hata kama una tofauti na wahusika wanaongoza heshimu tu hiyo taasis na taratibu zake, kibri muda wote huishia kudondosha wanaojiamini wana uwezo mkubwa.

Lissu alishinda ubunge wake 2015 kwa 56% tu, wakati ambao upepo wa Lowasa ulikuwa unawapa support kubwa. Kwa upepo wa saivi, uwezekano wa kudondoshwa kwenye chaguzi za marudio ni kubwa, acheze karata zake kwa umakini.
 
Lissu kiburi chake kimemponza, uwezo wa kutoa taarifa alikuwa nao na alikuwa anajua anatakiwa afanye hivyo ila kwa maksudi tu ili kuonyesha kibri na kutojali amegoma kuwasilisha taarifa zake.

Kama mtu ana uwezo wa kufanya media tour kutoka bara moja hadi jingine, nchi mbalimbali Ulaya kwa nini ashindwe tu kuandika barua ya status ya maendeleo yake?
Pole sana, unataka kulazimisha watu kumsujudia binadamu mwingine?
 
Kufuata utaratibu sio kusujudia, ni nini kilichawafanya viongozi wa CHADEMA kushindwa kutoa taarifa? Lissu ameweza kufanya ziara bara kwa bara, nchi kwa nchi ila eti hana uwezo wa kutoa taarifa bungeni????
Vipi zile makala alizokuwa anaandika kila wakati, alikuwa amepona? Hata jana amemjibu Spika kwa makala ila akiambiwa aandike barua nyumbu wake wanakuja juu eti mgonjwa hana uwezo wa kuandika barua, kibri ndio kimemuangusha.
 
Ni shetani tu ndio hawezi kujua lisu yupo wapi maana walikuwa wamepanga kumwondolea uhai wake
Ni kweli kabisa

Hadi hivi leo baada ya miaka 2 hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa na Polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashitaka hayo ya kumminia risasi Lissu!

Nia ya hawa watu ni kutaka kukitokomeza chama kikuu cha upinzani cha Chadema, kabla ya 2020, kama alivyojiapiza Mkulu kukifanya!
 
Hilo la kwako, mimi nachojua Lissu kibri chake tena cha kitoto ndio kimesababisha ubunge wake kukoma. Kuna kitu watanzania hawajifunzi, kuheshimu mamlaka, mamlaka ipo kisheria hata kama una tofauti na wahusika wanaongoza heshimu tu hiyo taasis na taratibu zake, kibri muda wote huishia kudondosha wanaojiamini wana uwezo mkubwa.

Lissu alishinda ubunge wake 2015 kwa 56% tu, wakati ambao upepo wa Lowasa ulikuwa unawapa support kubwa. Kwa upepo wa saivi, uwezekano wa kudondoshwa kwenye chaguzi za marudio ni kubwa, acheze karata zake kwa umakini.

Uko sahihi sana kuhusu kuheshimu mamlaka ila sio mamlaka kuheshimu walio tofauti nao kiitikadi.

Unasema Lissu alishinda kwa aslimia 56% tena akiwa anabebwa na upepo wa Lowasa. Kwa taarifa yako hizo asilimia 56% ni za halali tena baada ya kufanyika hujuma ili ashindwe. Na pia nataka uache upotoshaji kwamba Lissu au cdm walibebwa na upepo wa Lowassa. Kwa taarifa yako Lowwsa yeye ndio alibebwa na upepo wa cdm, kama alikuwa na nguvu hiyo na sio chama, angeenda TLP tuone huo upepo.

Kuhusu uchaguzi wa hiyo 2020, ukweli ni kuwa hakutakuwa na uchaguzi bali uchafuzi, kwa rais kutumia madaraka yake kupitisha wanaccm kwa lengo la kujaza wanaccm ili kulitumia bunge kumuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya 10yrs.
 
Kufuata utaratibu sio kusujudia, ni nini kilichawafanya viongozi wa CHADEMA kushindwa kutoa taarifa? Lissu ameweza kufanya ziara bara kwa bara, nchi kwa nchi ila eti hana uwezo wa kutoa taarifa bungeni????
Vipi zile makala alizokuwa anaandika kila wakati, alikuwa amepona? Hata jana amemjibu Spika kwa makala ila akiambiwa aandike barua nyumbu wake wanakuja juu eti mgonjwa hana uwezo wa kuandika barua, kibri ndio kimemuangusha.

Kufuata utaratibu ni kama rais alivyowapokea Makada wa ccm katika kamisheni ya jeshi huko Arusha? Au kunya naye kuku, akinya Bata kaharisha? Mikutano na shughuli zote za vyama vya kisiasa ziko wazi kwenye sheria, je hii sheria ya kuzuia shughuli za vyama inatoka wapi?

Ni hivi, hilo suala la kushambuliwa kwa Lissu liko wazi, huo uamuzi wa sasa ni muendelezo wa nia hiyo hiyo iliyotumika kumshambulia. So hakuna geni hapo.
 
Uko sahihi sana kuhusu kuheshimu mamlaka ila sio mamlaka kuheshimu walio tofauti nao kiitikadi.

Unasema Lissu alishinda kwa aslimia 56% tena akiwa anabebwa na upepo wa Lowasa. Kwa taarifa yako hizo asilimia 56% ni za halali tena baada ya kufanyika hujuma ili ashindwe. Na pia nataka uache upotoshaji kwamba Lissu au cdm walibebwa na upepo wa Lowassa. Kwa taarifa yako Lowwsa yeye ndio alibebwa na upepo wa cdm, kama alikuwa na nguvu hiyo na sio chama, angeenda TLP tuone huo upepo.

Kuhusu uchaguzi wa hiyo 2020, ukweli ni kuwa hakutakuwa na uchaguzi bali uchafuzi, kwa rais kutumia madaraka yake kupitisha wanaccm kwa lengo la kujaza wanaccm ili kulitumia bunge kumuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya 10yrs.
Lissu alishinda kwa 56% wakati huo huo Nasari alikuwa na karibu na banda, je yeye Nasari hakuibiwa? Ni wazi Lissu alishinda kwa kura chache na umaarufu wake kwenye jimbo lake si mkubwa hivyo marudio yoyote ya uchaguzi si habari njema kwake.

CCM tayari wana wabunge wa kutosha wa kuweza kubadilisha sheria yoyote. Unahitaji 2/3 tu ya bunge kuweza kubadilisha Katiba ambayo CCM tayari wanayo hivyo hii hoja ni mfu kama sio cheap propaganda.
 
Kuthibitisha kuwa hizi ni hila za serikali hii ya awamu ya tano ni kuwa mbona wabunge wa CCM hawafanyiwi kama wanavyofanyiwa wabunge wa Chadema??

Tujiulize yuko wapi mbunge wa CCM, Nimrod Mkono wa Musoma vijijini??

Huyu mbunge ni zaidi ya mwaka mmoja sasa, watanzania hatujui aliko, mbona Spika Ndugai hachukui hatua alizomchukulia Mbunge Lissu, ambaye kila mtu katika dunia hii anajua kuwa yupo nchini ubelgiji akitibu majeraha makubwa, baada ya kumimiwa risasi zaidi ya 38 kwenye gari lake na watu wasiojulikana??

Mbona utekelezaji wa sheria wa serikali hii ya utawala wa awamu ya ya tano una "double standards" za kupitiliza??
Nimrod Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Butiama ... Musoma vijijini ni Sospeter Muhongo.
 
Back
Top Bottom