tindo nadhani umeamua kutonielewa au hujanielewa. CCM hawawezi kuruhusu mtu akae zaidi ya miaka 10 sababu kutatokea maasi na hayo maasi yataongozwa na inner circle ya CCM. Mtu kama January Makamba, Mwigulu nk wametulia sababu wanajua wana nafasi 2025. Watu wa aina hii wakijua hawana nafasi tena ujue hapo kuna maasi yanakuja.Nimekuuliza tena, kwanini anatengeneza sheria za kupora nguvu za maamuzi ya kitaasisi na kuwapa watu, naona unaishia kuzunguka tu. Nimerudia zaidi ya mara moja kuhusu nguvu zinazohamishwa kutoka mahakamani na kupewa watu kuwa final say. Sioni popote inapotoweka kwenye hilo. Nimekuambia hivyo ni viashiria vya wazi vya mtu huyu kujikita madarakani zaidi muda.
Nataka nikupe mfano mmoja mrahisi ili kukuonyesha hao ccm ikiwepo ww hawana nguvu dhidi yake, kuhusu maamuzi ya mtu, na wengi wao hawajausoma mchezo na wakiamka watakuwa wamechelewa. Mgombea wa ubunge wa ccm huwa anashindanishwa na wengine kupata mmoja, lakini nyakati za uchaguzi wa marudio maamuzi yalifanyika na genge dogo kupitisha wagombea waliotoka huko upinzani, wakapewa nafasi bila hata kukijua chama na wakapitishwa kibabe. Na kwenye hizo chaguzi zikafanyika rafu za wazi za kuvunja sheria ambazo leo mnasema maamuzi ya Lissu yamezitii hizo hizo, ili mgombea wa ccm atangazwe mshindi. Kama aliweza kufanya vile huku wanachama wakilalamika kichini chini, watamfanya nini hiyo 2025 akitanua goli? Kungekuwa na wanaccm wasafi ningekuelewa, lakini hawa wagombea ambao wakichomoza pua tu, Takukuru wanaambiwa wafuatilie skendo zao?
tindo nadhani umeamua kutonielewa au hujanielewa. CCM hawawezi kuruhusu mtu akae zaidi ya miaka 10 sababu kutatokea maasi na hayo maasi yataongozwa na inner circle ya CCM. Mtu kama January Makamba, Mwigulu nk wametulia sababu wanajua wana nafasi 2025. Watu wa aina hii wakijua hawana nafasi tena ujue hapo kuna maasi yanakuja.
Kwa lugha nyepesi, kuwepo ukomo wa madaraka kunaleta hali ya uvumilivu ndani ya CCM na nchi, CCM wanalitambua hili vyema na hivyo mawazo yako ya kufikirika kuwa Magu atajiongezea muda hayapo na hayawezekaniki.
"Sheria zimewekwa ili binadamu tuwe watu" basi tuzifuate na kuziheshimu ili tukamilishe utu wetu.Kuna tofauti kati ya binadamu na mtu. Sio kila binadamu ni mtu. Kila mtu ni binadamu. Wewe ni binadamu tu. Binadamu ni mnyama tu kama wanyama wengine. Sheria zipo binadamu wawe watu. Sheria inayomfanya mtu kuwa binadamu tu ni batili. Mashauri kwa Mbowe na Matiko alitumia vifungu vya sheria! Rumanyika alitumia nini? Tofauti kuu ni kwamba mmoja ni binadamu na mwingine ni mtu! Sheria zipo kuhudumia mtu.