Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,984
- 103,357
Lissu alishinda kwa 56% wakati huo huo Nasari alikuwa na karibu na banda, je yeye Nasari hakuibiwa? Ni wazi Lissu alishinda kwa kura chache na umaarufu wake kwenye jimbo lake si mkubwa hivyo marudio yoyote ya uchaguzi si habari njema kwake.
CCM tayari wana wabunge wa kutosha wa kuweza kubadilisha sheria yoyote. Unahitaji 2/3 tu ya bunge kuweza kubadilisha Katiba ambayo CCM tayari wanayo hivyo hii hoja ni mfu kama sio cheap propaganda.
Unaweza ukaniambia ni wabunge wangapi wa ccm walishinda kihalali zaidi ya 70%?. Mbunge aliyepata kura nyingi kuliko wabunge wote ni sugu. Je hiyo ni tiketi ya kwamba uchaguzi ujao anashinda? Tuje kwa Magufuli, yeye alishinda kaa 58%, je hiyo ni ishara kwamba uchaguzi ujao anashindwa?
Ni kweli ccm wanazaidi ya 2/3 wanaweza kubadili chochote hilo sipingi, ila inatakiwa kusiwe na wabunge wengi wa upinzani wanaoweza kupinga hili kwa hoja kwani kuna umma ambao jambo hilo ni zito.
Ukitaka kujua kwamba lengo ni kubadilisha katiba ili akae madarakani zaidi angalia sheria ya vyama vya siasa. Anatunga sheria kwamba maamuzi yatoke kwenye taasisi/mahakama apewa mtu (msajili). Azaki za kiraia pia anageuzwa msajili kuwa yeye ndio msemaji wa mwisho badala ya taasisi na mahakama. Sababu hasa, vyama vya siasa na azaki ndio haswa huonyesha kupinga mambo kama hayo ya kuongeza muda wa kukaa madarakani. Hivyo ni rahisi yeye kuwaagiza wasajili kufuta chama au azaki bila kuwajibika pindi zitakapohoji hali hiyo.
Ogopa kiongozi mzalendo asiyetaka katiba ya wananchi, bali kutunga sheria za kulinda madaraka yake. Narudia tena, hakuna sheria wala nini kuhusu hatua hiyo ya Lissu, bali ni wale wale waliotaka kumtoa uhai wamerudi kwa sura ya sheria na taratibu fullstop.