TAMKO
JF-Expert Member
- Oct 11, 2011
- 1,090
- 763
Watanzania Wenzangu,
Maskhara, Utani, na ushabiki tafaadhali tuviweke kando. Kwa Umoja wetu tuungane sasa na kwa rasilimali za Nguvu Zetu tuwatetee na kuwanusuru Maprofessor wetu kwenye Lindi zito la kashfa ya Kujichotea mifedha tele kutoka kwenye account iliyofumanika ya Tegeta ESCROW. Tukea sakata hili lilipochukua kasi ukingoni mwa bunge hili, nimekuwa karibu na Redio yangu ya picha nikifuatilia nukta kwa nukta ya mijadala na majibizano yote hadi usiku kabisa wa Ijumaa saa sita kasoro ivi wakati kamanda wa Ukweli, Mtu asiye ogopa kitu chochote, Shujaa anayepenya kati ya Majambazi, majangili, wezi na walarushwa nene Mhe Mbowe, alipopigilia msumari kichwa cha bunge, wezi, wanafiki, wasiojitambua wakatawanyika hatimae vichwa vyenye akili vikaunda tena mapendekezo mapya makali zaidi yaliyo wasilishwa Jumamosi na hapana aliye pinga.
Ndugu zangu mapendekezo haya ni Mwiba, ni makali, ni Upanga ukatao kotekote. hata kama Raisi wetu asipo chukua hatua yoyote lakini tayari maprofessor wetu wameshavuliwa hadi nguo na vidude vya ndani kabisa, ni kidonda kwao na ukilema ambao kwa binaadam ngumu sana kupona. ni wengi wanaokumbwa na fagio hili ila sanasana niwasemee hawa wawili ili tuwateteee tetee lau itawasaidia.
Ndugu Watanzania, Mtu kuitwa professor sio kitu cha mchezo, nadhani wale wenye shahada moja au mbili hata tatu mnanielewa vilivyo. professor ni msomi, Bingwa wa usomi. Professor sio neno dogo la kutamkatamka, hawa ni watu Nguli, wamebobea kitaaluma na kuiva. professor sospeter M. Muhongo hakuna asichokijua kwenye mawe na miamba (Geology). professor anna kajumulo Tibaijuka kabobea kwenye Uchumi mzalendo (Angro-Economics). hawa watu si wa kubeza kwenye mizania ya Elimu.
sitaki kurudia historia lakini Itoshe kusema kwamba Nimeongea sana si kwenye magazeti nata michango yangu humu kumpigia kelele Raisi wetu kwamba watu hawa hawafai kuwaweka kwenye uwanja wa kisiasa. HAWAFAI, WATAHARIBIKAAAA..!, Hakuna aliye sikia, hadi tunafika hapa hii ni dharau, kiburi, na kutowajibika kwa washauri wa Rais wetu mpendwa. washauri hawa wamempotosha sana Raisi wetu kwenye Mengi, hawafai, wamemfanyia Uhaini mwingi hawa jamaa, kumshauri vibaya Raisi ni Kukiuka state policy, ni aina ya uhaini. hawa ndio Zigo lote la mavi wadondoshewe.
We ulionawapi Ushauri kwamba Raisi wiki nyingi hayuko nchini kwa matibabu Marekani, huku nchi inafukuta na bunge linarindima, ni wazi raisi yuko well informed, kisha washauri wanamwandalia tamko la kuongelea safari yake tu na mbaya zaidi anasema ya Bungeni hayajui, hii ni Tafsiri mbaya sana, ni picha kwamba raisi akishapanda ndege hajui lolote kuhusu nchini yake, kwamba hata kama kuna mapinduzi yeye haelewi lolote, noooo no way hapa hawakumtendea vema Raisi. Angepaswa kutamka wazi kwamba Yanayoendelea Bungeni Yote ana taarifa nayo na taratibu zitachukua mkondo wake, that's a head of state statement, rather "i know nothing till reported and presented before me....!!?]. tuendeleee na Maprop wetu..
Ikumbukwe Tokea Juzikati Aprili 2012. prop Muhongo alipoteuliwa uwaziri wa umeme na mawemawe amekuwa na mlolongo wa Matukio na matamshi ambayo sikunyingi yalisha mnyima Legacy ya kuwa kwenye kiti cha Uwaziri huo wa Nishati na Madini. jamani Huyu Purely ni professor sio mwanasiasa ni jembe kitaaluma. Dawati la Utendaji ndilo linalo mfaa sio mchezo wa mdomoni.
Mara Nyingi akiongea professor wetu huyu lazima ama atukane, ama akashifu watu, sio mara chache alishasema watanzania wavivu wa kufikiri (including yeye yaani mtu anajitukana hadi yeye), alishawahi kuwaita viongozi wa dini mambumbumbu, alishatoa matamshi yanayochochea kero iliyosababaisha vifo na vurugumai kubwa huko gesini Mtwara wote tunajua hili, uanasiasa wa professor huyu mapemaa Ulishaonekana ni Sumu na majanga. washauri wa Raisi wangeliona hili mapemaa na wangemuondoa na Kumwachia majukumu ya Utendaji tu.
Kali zaidi Juzi kwenye kikao Cha Bunge alikurupuka sana kuongea tu bila data,katia viingereza vingi vikamgomea, kila anachosema vijana wanampinga kwa data. nashangaa jamaa bungeni Yumo tu hatoki sio kwamba ana ngozi ngumu wakati mwingine network si bure zimeshakatika, we uone watu wanagaragaza CV nzito ya uprofessor kama bata aliye choka utakuwa na akili bado!!.
Washauri hawa wa raisi wetu wamesababisha maafa na Ulemavu kwa professor wetu huyu. kwenye fani za Ujenzi tunasema Mhandisi mwenye lezeni yake akisanifu majaengo yakaleta hitilafu kidogo hapana kungojea hadi yauwe wananchi ananyang'anywa leseni yake faster anabakia fundi mchundo, iweje raisi ashindwe mapema Kushauriwa amuondoe haraka waziri Huyu.
Bora angepewa hata Ukatibu mkuu somewhere jamaa jembe kwenye kazi. Ulionawapi mtaalam huyu wa miamba ati leo anapiga dili za Udalali ofisini, what a life shame! Wengine hamjui hili kwamba Prof. Sospeter Muhongo alishatunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Kisomi ya Mfalme Napoleoni ijulikanayo kama 'Ordre des Palmes Académiques (Order of Academic Palms)' toka Serikali ya Ufaransa.
Hii ni kutokana na mchango wake wenye ufanisi duniani katika medani za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Mtu huyu ni wa kuketi kwenye dawati akipanga ubunifu wa Teknolojia ya miamba atusaidie kuokoa mabilioni ya shiilingi yanayopotea kwenye wezi wa rasilimali zetu, ati tunaambiwa leo anapiga dili za wizi na udalali ofisini??!! Inaumaje..!
Nilikuwa sijabahatika Kumwona live professor Tibaijuka akiongea kwenye majukwaa ya kisiasa, nakumbuka Chadema walifanya Mkutano mkubwa Viwanja vya jangwani sikumbuki lini uliofana sana, baadae Chama hiki nacho kikajibu mapigo kwa kuwasombelea watu uwanjani.
Kitu kikubwa kilichonivuta uwanjani ni kumsikia professor Anna Kajumulo Tibaijuka akiongea. nadhani wote mliokuwepo mlishuhudia low and speechless ever from the professor. What i learnt from that day Wasomi wa ukweli haipendezi kuwaharibu siasani.
Can you imargine, professor Mzima by her name anakiri Kupokea Tsh1.67 billin, Tanzanian Money, no no hata kama sio Tanzanian money let say somebody kuku au bata flani from country code XXX amempatia tu, Tsh 1.67 ??!!, then brofessor anadai kazipeleka kwenye biashara ya shule not research inakujia mkichwa kweli?. anaropoka zinasaidia watoto wasio jiweza shuleni, but madam professor ada ya mwanafunzi kwenye shule yako ni 4.4million then inamaana maskini wa tanzania mtoto wake anasoma kwenye shule zenye ada staring from 4.4 . mambo ya kutisha kabisa.
Jambo nalosema ni kwamba wasomi wetu hawa wazuri Wameharibiwa na serikali Hii. Serikali imwavuruga, kuwachanganya, kuwadhalilisha kiasi hawajielewi. Hivi nikisema Chama chetu hiki ni mashine ya Kuharibu wasomi ntakuwa nakosea?. Kati ya Maprofessor wanne kwenye serikali Nzima Nusu yake yaani wawili wawe majanga hii si hatari kubwa sana. hata hao wengine pindo za nguo zao hazijafunuliwa peupe tu..
Sijikiti sana kwenye dhima nzima ya Ukwibaji wa mashilingi hayo kwa sababu sidhani kama ni jambo geni kwenye serikali hii iliyojaa Uvundo wa kukwiba pasipo kukemeana. serikali ina matrillioni so watu wanachota tu kila kukicha, basi tu bahati mbaya hiyo imewadondokea hao. serikali hii mwizi ni mfalme maskini ni kibaka.
Ukiiba kuku unafungwa miaka ya mfano na kadiri unavyoiba sana kifungo kinapungua na ukiiba mabilioni hadi ulinzi unapewa. tabia ya kuibia serikali haijaanza jana mnakumbuka Mwalimu alisema kipindiflan serikali yake watu walikuwa wanakwiba tuu, Mwasia mmoja kama leo akakwiba hadi akajisahau akaropoka "serikali Yote ya mwalimu iko mfukoni mwake" Mwalimu akastuka sana, he kumbe yeye na serikali yake wako kwenye mfuko wa mhindi mmoja, akakikarabati kiti chake cha uraisi sawia.
Kwa sasa nchini ukikamatwa ukafikishwa kituoni, kisha wakakwambia vua viatu, toa ulivyokuwa navyo mfukoni, mwanaume ukatoa kitita burungutu msimbazi zimebabana za kutosha zikatua kwenye macho ya afande mwanaume utahudumiwa kama mfalme hapo kituoni. kila afande ataunda ubest na wewe. nchi hii ilishabadilika kuwa ya wenyenavyo, wasionavyo mtulie kimyaaaa ndio tafsiri ya amani yetu.
Tujitokeza sasa kuwatetea Wataalam wetu hawa, tuhakikishe wanatoka kwenye siasa na kwenye chama hiki kichafu, kisha tuhakikishe hela zilizo wazuzua wakalewalewa na kuwa kama wasiojitambua zitaifishwe haraka, warudi kwenye senceship yao kama wataalam, bado tunawahitaji sana, taifa hili bado changa, taifa maskini, wasomi ni lulu kwenye taifa hili. taifa gani lisilo linda wasomi wake hadi wanapata ukilema wa stress za maisha kiasi hiki?