Tujitokeze kuwatetea Prof Muhongo na Prof Tibaijuka

Tujitokeze kuwatetea Prof Muhongo na Prof Tibaijuka

Hujitambui wewe!!! Umepata mgao kiasi gani toka kwa Ruge? Kama huna la maana la kuandika kaa kimya.
 
umeeleweka...siasa zimewafisha macho wasomi, ila uwe unarudia kusoma ili u-edit "Angro- Economics" ndo nini! ukishindwa ku-summarise kitu, ujue hicho kitu hukijui vizuri bado- jipange ndo ulete hoja
 
Hatuhitaji uzuri wa CV ya mtu tunataka uwazi, uwajibikaji na matokeo mazuri kwenye jamii ya watanzania. Wasomi wengi wameungana na watawala kuifilisi nchi na kupotosha ukweli wa mambo.
 
Kiongozi haina haja ya kutafuna maneno na kujizungusha, prof muhongo na tibaijuka ni mafisadi na wanahusika moja kwa moja na uchotaji wa pesa ya umma/escrow........kama unabisha basi wewe unabishana na ripoti ya cag, tra na takukuru, na hakuna chombo kingine chochote kitakacho kupa habari ya ukweli juu ya suala la escrow zaidi ya hivyo
 
Kweli warudi darasani siasa hawaziwezi
wakashike chaki tu
 
Hao maprofesa ni wangese..taifa limewasomesha ili waje walikomboe taifa...maprofesosa wa nchi za ulaya, china na japani hua wanatumia usomi wao kuja kukomboa nchi zao na kufanya ziondokane na umasikini...ila hawa wa hapa kwetu wanatumia uprofesa wao na elimu yao kuliangamiza taifa na kuzidisha umasikini...sasa wana umuhim u gani m..vi hao?
wafie mbele huko
 
Wasomi wanatakiwa kubadilisha mambo,kurahisisha shughuri za maendeleo,wanatakiwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya jamii,prof. hakiwa hatoufautiani na wanasiasa wanojua kusoma na kuandika tu hana maana.
CCM imesheeni maprofesa na MaPhd kama Kapuya,Maghenbe n.k.. lakini hawajatumia elimu yao kubadilisha nchi hii zaidi tunashuhudia matendo yao ya aibu
 
Hatujapoteza isipokuwa tumemwagikiwa na kilichomwagika kina tabu kukipata tena,ila hawa ni wale waliombeza Mheshimiwa Othman Masud Mwanasheria Mkuu (Aliekuwa) wa Zanzibar hivi utampimaje huyu na hao ,hawa walisoma sio kwa ajili ya faida ya wengine katika maisha yao walisoma kupata cheo,hela na uluwah ! Baada ya kupata wamekuwa upande wa wanaoendeleza dhulma,je watu wa aina hiyo hata kama wangekuwa majenerali au majenereta faida yao kwa wananchi hupatikana kwa kuwanyonga na kuwakamua wananchi huku wakiwalisha maneno mazuri ya elimu yao ,mtu hufaliwa na kazi yake na sio elimu yake ,elimu inakuelekeza na kukujulisha ila kazi yako ndio itakayozaa matunda yakaonekana ,ya Othman Masud tumeiona ya hawa nayo tueiyona ,hawa kazi yao mbaya japo wana elimu ,mbona wasomi wapo wengi sana tu.

Yupo yule anetembezwa na mikasi kufungua makongamano na majumba ,sasa mtu kama yule na elimu aliyonayo ni wa kwenda kukata utepe kufungua jumba la sanaa ? Wacha yawakute utpo wengi wenye uprofesa hata huo wa kichina na hatuna kazi na tulienda kutafuta tunapigwa tarehe ,bora wakae pembeni huenda wengine tukaitwa kuanza kazi.
 
Kichwa cha habari na content ya maoni yako ni tofauti, ndio maana watu wengi wame critisize.Ila maoni yako ni sawia. Si vyema kuwafanya maprofesa kuwa wanasiasa.Angalia sasa walipoiweka Credibility ya wasomi wa kibongo!!

Watanzania Wenzangu

Maskhara, Utani, na ushabiki tafaadhali tuviweke kando. Kwa Umoja wetu tuungane sasa na kwa rasilimali za Nguvu Zetu tuwatetee na kuwanusuru Maprofessor wetu kwenye Lindi zito la kashfa ya Kujichotea mifedha tele kutoka kwenye account iliyofumanika ya Tegeta ESCROW. Tukea sakata hili lilipochukua kasi ukingoni mwa bunge hili, nimekuwa karibu na Redio yangu ya picha nikifuatilia nukta kwa nukta ya mijadala na majibizano yote hadi usiku kabisa wa Ijumaa saa sita kasoro ivi wakati kamanda wa Ukweli, Mtu asiye ogopa kitu chochote, Shujaa anayepenya kati ya Majambazi, majangili, wezi na walarushwa nene Mhe Mbowe, alipopigilia msumari kichwa cha bunge, wezi, wanafiki, wasiojitambua wakatawanyika hatimae vichwa vyenye akili vikaunda tena mapendekezo mapya makali zaidi yaliyo wasilishwa Jumamosi na hapana aliye pinga.

Ndugu zangu mapendekezo haya ni Mwiba, ni makali, ni Upanga ukatao kotekote. hata kama Raisi wetu asipo chukua hatua yoyote lakini tayari maprofessor wetu wameshavuliwa hadi nguo na vidude vya ndani kabisa, ni kidonda kwao na ukilema ambao kwa binaadam ngumu sana kupona. ni wengi wanaokumbwa na fagio hili ila sanasana niwasemee hawa wawili ili tuwateteee tetee lau itawasaidia.

Ndugu Watanzania, Mtu kuitwa professor sio kitu cha mchezo, nadhani wale wenye shahada moja au mbili hata tatu mnanielewa vilivyo. professor ni msomi, Bingwa wa usomi. Professor sio neno dogo la kutamkatamka, hawa ni watu Nguli, wamebobea kitaaluma na kuiva. professor sospeter M. Muhongo hakuna asichokijua kwenye mawe na miamba (Geology). professor anna kajumulo Tibaijuka kabobea kwenye Uchumi mzalendo (Angro-Economics). hawa watu si wa kubeza kwenye mizania ya Elimu.

sitaki kurudia historia lakini Itoshe kusema kwamba Nimeongea sana si kwenye magazeti nata michango yangu humu kumpigia kelele Raisi wetu kwamba watu hawa hawafai kuwaweka kwenye uwanja wa kisiasa. HAWAFAI, WATAHARIBIKAAAA..!, Hakuna aliye sikia, hadi tunafika hapa hii ni dharau, kiburi, na kutowajibika kwa washauri wa Rais wetu mpendwa. washauri hawa wamempotosha sana Raisi wetu kwenye Mengi, hawafai, wamemfanyia Uhaini mwingi hawa jamaa, kumshauri vibaya Raisi ni Kukiuka state policy, ni aina ya uhaini. hawa ndio Zigo lote la mavi wadondoshewe.[...We ulionawapi Ushauri kwamba Raisi wiki nyingi hayuko nchini kwa matibabu Marekani, huku nchi inafukuta na bunge linarindima, ni wazi raisi yuko well informed, kisha washauri wanamwandalia tamko la kuongelea safari yake tu na mbaya zaidi anasema ya Bungeni hayajui, hii ni Tafsiri mbaya sana, ni picha kwamba raisi akishapanda ndege hajui lolote kuhusu nchini yake, kwamba hata kama kuna mapinduzi yeye haelewi lolote, noooo no way hapa hawakumtendea vema Raisi. Angepaswa kutamka wazi kwamba Yanayoendelea Bungeni Yote ana taarifa nayo na taratibu zitachukua mkondo wake, that's a head of state statement, rather "i know nothing till reported and presented before me....!!?]. tuendeleee na Maprop wetu..

Ikumbukwe Tokea Juzikati Aprili 2012. prop Muhongo alipoteuliwa uwaziri wa umeme na mawemawe amekuwa na mlolongo wa Matukio na matamshi ambayo sikunyingi yalisha mnyima Legacy ya kuwa kwenye kiti cha Uwaziri huo wa Nishati na Madini. jamani Huyu Purely ni professor sio mwanasiasa ni jembe kitaaluma. Dawati la Utendaji ndilo linalo mfaa sio mchezo wa mdomoni.Mara Nyingi akiongea professor wetu huyu lazima ama atukane, ama akashifu watu, sio mara chache alishasema watanzania wavivu wa kufikiri (including yeye yaani mtu anajitukana hadi yeye), alishawahi kuwaita viongozi wa dini mambumbumbu, alishatoa matamshi yanayochochea kero iliyosababaisha vifo na vurugumai kubwa huko gesini Mtwara wote tunajua hili, uanasiasa wa professor huyu mapemaa Ulishaonekana ni Sumu na majanga. washauri wa Raisi wangeliona hili mapemaa na wangemuondoa na Kumwachia majukumu ya Utendaji tu. kali zaidi Juzi kwenye kikao Cha Bunge alikurupuka sana kuongea tu bila data,katia viingereza vingi vikamgomea, kila anachosema vijana wanampinga kwa data. nashangaa jamaa bungeni Yumo tu hatoki sio kwamba ana ngozi ngumu wakati mwingine network si bure zimeshakatika, we uone watu wanagaragaza CV nzito ya uprofessor kama bata aliye choka utakuwa na akili bado!!.

Washauri hawa wa raisi wetu wamesababisha maafa na Ulemavu kwa professor wetu huyu. kwenye fani za Ujenzi tunasema Mhandisi mwenye lezeni yake akisanifu majaengo yakaleta hitilafu kidogo hapana kungojea hadi yauwe wananchi ananyang'anywa leseni yake faster anabakia fundi mchundo, iweje raisi ashindwe mapema Kushauriwa amuondoe haraka waziri Huyu. Bora angepewa hata Ukatibu mkuu somewhere jamaa jembe kwenye kazi. Ulionawapi mtaalam huyu wa miamba ati leo anapiga dili za Udalali ofisini, what a life shame! Wengine hamjui hili kwamba Prof. Sospeter Muhongo alishatunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Kisomi ya Mfalme Napoleoni ijulikanayo kama 'Ordre des Palmes Académiques (Order of Academic Palms)' toka Serikali ya Ufaransa. Hii ni kutokana na mchango wake wenye ufanisi duniani katika medani za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Mtu huyu ni wa kuketi kwenye dawati akipanga ubunifu wa Teknolojia ya miamba atusaidie kuokoa mabilioni ya shiilingi yanayopotea kwenye wezi wa rasilimali zetu, ati tunaambiwa leo anapiga dili za wizi na udalali ofisini??!! Inaumaje..!

Nilikuwa sijabahatika Kumwona live professor Tinaijuka akiongea kwenye majukwaa ya kisiasa, nakumbuka Chadema walifanya Mkutano mkubwa Viwanja vya jangwani sikumbuki lini uliofana sana, baadae Chama hiki nacho kikajibu mapigo kwa kuwasombelea watu uwanjani. Kitu kikubwa kilichonivuta uwanjani ni kumsikia professor Anna Kajumulo Tibaijuka akiongea. nadhani wote mliokuwepo mlishuhudia low and speechless ever from the professor. What i learnt from that day Wasomi wa ukweli haipendezi kuwaharibu siasani. Can you imargine, professor Mzima by her name anakiri Kupokea Tsh1.67 billin, Tanzanian Money, no no hata kama sio Tanzanian money let say somebody kuku au bata flani from country code XXX amempatia tu, Tsh 1.67 ??!!, then brofessor anadai kazipeleka kwenye biashara ya shule not research inakujia mkichwa kweli?. anaropoka zinasaidia watoto wasio jiweza shuleni, but madam professor ada ya mwanafunzi kwenye shule yako ni 4.4million then inamaana maskini wa tanzania mtoto wake anasoma kwenye shule zenye ada staring from 4.4 . mambo ya kutisha kabisa.

Jambo nalosema ni kwamba wasomi wetu hawa wazuri Wameharibiwa na serikali Hii. Serikali imwavuruga, kuwachanganya, kuwadhalilisha kiasi hawajielewi. hivi nikisema Chama chetu hiki ni mashine ya Kuharibu wasomi ntakuwa nakosea?. Kati ya Maprofessor wanne kwenye serikali Nzima Nusu yake yaani wawili wawe majanga hii si hatari kubwa sana. hata hao wengine pindo za nguo zao hazijafunuliwa peupe tu..

Sijikiti sana kwenye dhima nzima ya Ukwibaji wa mashilingi hayo kwa sababu sidhani kama ni jambo geni kwenye serikali hii iliyojaa Uvundo wa kukwiba pasipo kukemeana. serikali ina matrillioni so watu wanachota tu kila kukicha, basi tu bahati mbaya hiyo imewadondokea hao. serikali hii mwizi ni mfalme maskini ni kibaka. Ukiiba kuku unafungwa miaka ya mfano na kadiri unavyoiba sana kifungo kinapungua na ukiiba mabilioni hadi ulinzi unapewa. tabia ya kuibia serikali haijaanza jana mnakumbuka Mwalimu alisema kipindiflan serikali yake watu walikuwa wanakwiba tuu, Mwasia mmoja kama leo akakwiba hadi akajisahau akaropoka "serikali Yote ya mwalimu iko mfukoni mwake" Mwalimu akastuka sana, he kumbe yeye na serikali yake wako kwenye mfuko wa mhindi mmoja, akakikarabati kiti chake cha uraisi sawia. Kwa sasa nchini ukikamatwa ukafikishwa kituoni, kisha wakakwambia vua viatu, toa ulivyokuwa navyo mfukoni, mwanaume ukatoa kitita burungutu msimbazi zimebabana za kutosha zikatua kwenye macho ya afande mwanaume utahudumiwa kama mfalme hapo kituoni. kila afande ataunda ubest na wewe. nchi hii ilishabadilika kuwa ya wenyenavyo, wasionavyo mtulie kimyaaaa ndio tafsiri ya amani yetu.

Tujitokeza sasa kuwatetea Wataalam wetu hawa, tuhakikishe wanatoka kwenye siasa na kwenye chama hiki kichafu, kisha tuhakikishe hela zilizo wazuzua wakalewalewa na kuwa kama wasiojitambua zitaifishwe haraka, warudi kwenye senceship yao kama wataalam, bado tunawahitaji sana, taifa hili bado changa, taifa maskini, wasomi ni lulu kwenye taifa hili. taifa gani lisilo linda wasomi wake hadi wanapata ukilema wa stress za maisha kiasi hiki???
 
Mto mada umeandika kwa umaridadi wa hali ya juu na ni ukweli mtupu. Wanajamii wameishia kusoma kichwa cha habari na kuanza kuropoka
 
Mivivu ya kusoma habari nzima inamshambulia tu mleta hoja bila kujua msingi wa habari yake, Kiukweli nimekupata vyema Kamanda TAMKO mada yako ni ya kiwango cha kiporofesa kabisa achana na hawa wasoma Heading na kutokomea bila kusoma the Main Thread. Big up sana

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Nadhani asilimia kubwa ya wanao comment hii mada aidha hawajaielewa au hawajaisoma yote..
Ahsante mtoa mada kwa pointi zenye kufikirisha
 
Back
Top Bottom