Tujitokeze kuwatetea Prof Muhongo na Prof Tibaijuka

Tujitokeze kuwatetea Prof Muhongo na Prof Tibaijuka

Mimi nimekupata na kukuelewa sawia!

Bahati mbaya sana wana forum wengi wameishia kusoma heading tu na kutoa negative judgement kwa hoja yako nzuri kwa kukutukana tu bila sababu.

Nadhani na nafikiri ujinga wetu watanzania ndo uko hapa................kwenye maandishi!!

Back to the topic;

CCM ni tanuru la kuharibu na kuua wasomi wetu. Unamjua Professor anayeitwa Jumanne Maghembe, waziri katika moja ya wizara za serikali hii ya Jakaya (nadhani Wizara ya Maji)? Huyu jamaa huwa mnamwonaje katika arguments zake katika occasions flaniflani? Yaani mimi humwona kama ---- flani hivi na ndipo hapo unaweza kuamini kuwa siasa za CCM zilishamfanya huyu na wasomi wetu wengi kama wajinga flani hivi!!

All in all tunaye Professor mwingine wa kichina.......Prof. Jakaya Mrisho Kikwete. Let see his professsorship inputs katika serikali yake na Taifa hili. Lakini nionavyo mimi ni majanga makuu!!
 
Kweli ukitaka kumtawala mtanzania tengeneza mkataba. Atasoma kichwa cha habari tu atasaini. Uvuvi wa kusoma na kuchambua yaliyomo vinatumaliza na mwisho wa siku tunabakia kutukana kama wehu
 
Hivi wewe mleta mada una malezi ya pande mbili kweli??
Yaani unataka kutushawishi kujiunga na wewe kutetea ujinga? Mungu akulaani aisee yaani huna aibu? Watanzania wanateseka huko hospital, wanafunzi wanashindwa kusoma kwa sababu ya kodi za watu kuishia mikononi mwa hawa mafisadi na bado unataka kuwatetea??
Najua unakula kwa raha kabisa kupitia hawa mafisadi ila kumbuka hii nchi ni yetu sote mwisho wa siku mungu atawahukumu kwa wizi wenu na unafiki mliujaza mioyoni.

Sina chama wala sishabikiagi hizo siasa zenu ila najari watu kunufaika na rasilimali za taifa.

Masikini wee, yaani wewe huna tofauti na wale wanaoambiwa kwenye mtihani attempt no question halafu wewe ukajibu yote... Acha uvivu, soma habari yote ndiyo u-comment
 
profesa mwandosya,dr.mwakyembe,dr.kingwagala,dr.tizeba,dr.mary nagu,dr.kawambwa,dr.ndugulile,profesa jumanne maghembe,prof.tibaijuka,mhongo nk
 
Hata mimi ni proffesor
 

Attachments

  • 1417374601977.jpg
    1417374601977.jpg
    49 KB · Views: 168
kaka nina uhakika watu hawajakusoma, wameona tittle tu na kukomenti nadhani wengi humu hawapendi maelezo mareefu! ila umenena
 
TAMKO hili uliloliandika hapa, si kwa level ya I.Q zetu, utapata matusi ya kutosha,


Bring Back Our Money..
 
Last edited by a moderator:
Kweli ukitaka kumtawala mtanzania tengeneza mkataba. Atasoma kichwa cha habari tu atasaini. Uvuvi wa kusoma na kuchambua yaliyomo vinatumaliza na mwisho wa siku tunabakia kutukana kama wehu

Kusoma ni tatizo zito sana kwa watanzania, wanapenda dot..dot.. lakini sio mbaya jamvi hili ni kama Nyavu za kokoro, wakubwa kwa wadogo, vinavyoliwa na visivyoliwa, wajinga na werevu.. tuvumiliane tu..by the way wajinga hawaandikiwi sentensi bali werevu na makini.
 
embu Chapa Nalo Jr, kasinge, MAHORO, mchemsho, aminiusiamini, Puro, Sikonge, Manjagata, mckenzie, The Red Pen, mnyakwetu, Pakawa natoka hapa, Mingoi

na wengine haraka geuzeni mje Huku jamvini mrekebishe rubbish mlizo andika, nyie ndio vinara wa kulifanya jamvi hili lionekane kama kijiwe cha wahuni na mataahira, wavivu wa kusoma na kuwaza. Huna haki ya Kuccoment kama hujasoma maada. hulazimishwi!!watanzania wengine ni mizigo tu ndio hawa prop aliwaita wavivu wa kufikiri na kusoma. ukiona maada ndefu unavuka unaiacha nani kakulazimisha kwani?
 
Last edited by a moderator:
watanzania wenzangu

maskhara, utani, na ushabiki tafaadhali tuviweke kando. Kwa umoja wetu tuungane sasa na kwa rasilimali za nguvu zetu tuwatetee na kuwanusuru maprofessor wetu kwenye lindi zito la kashfa ya kujichotea mifedha tele kutoka kwenye account iliyofumanika ya tegeta escrow. Tukea sakata hili lilipochukua kasi ukingoni mwa bunge hili, nimekuwa karibu na redio yangu ya picha nikifuatilia nukta kwa nukta ya mijadala na majibizano yote hadi usiku kabisa wa ijumaa saa sita kasoro ivi wakati kamanda wa ukweli, mtu asiye ogopa kitu chochote, shujaa anayepenya kati ya majambazi, majangili, wezi na walarushwa nene mhe mbowe, alipopigilia msumari kichwa cha bunge, wezi, wanafiki, wasiojitambua wakatawanyika hatimae vichwa vyenye akili vikaunda tena mapendekezo mapya makali zaidi yaliyo wasilishwa jumamosi na hapana aliye pinga.

Ndugu zangu mapendekezo haya ni mwiba, ni makali, ni upanga ukatao kotekote. Hata kama raisi wetu asipo chukua hatua yoyote lakini tayari maprofessor wetu wameshavuliwa hadi nguo na vidude vya ndani kabisa, ni kidonda kwao na ukilema ambao kwa binaadam ngumu sana kupona. Ni wengi wanaokumbwa na fagio hili ila sanasana niwasemee hawa wawili ili tuwateteee tetee lau itawasaidia.

Ndugu watanzania, mtu kuitwa professor sio kitu cha mchezo, nadhani wale wenye shahada moja au mbili hata tatu mnanielewa vilivyo. Professor ni msomi, bingwa wa usomi. Professor sio neno dogo la kutamkatamka, hawa ni watu nguli, wamebobea kitaaluma na kuiva. Professor sospeter m. Muhongo hakuna asichokijua kwenye mawe na miamba (geology). Professor anna kajumulo tibaijuka kabobea kwenye uchumi mzalendo (angro-economics). Hawa watu si wa kubeza kwenye mizania ya elimu.

Sitaki kurudia historia lakini itoshe kusema kwamba nimeongea sana si kwenye magazeti nata michango yangu humu kumpigia kelele raisi wetu kwamba watu hawa hawafai kuwaweka kwenye uwanja wa kisiasa. Hawafai, wataharibikaaaa..!, hakuna aliye sikia, hadi tunafika hapa hii ni dharau, kiburi, na kutowajibika kwa washauri wa rais wetu mpendwa. Washauri hawa wamempotosha sana raisi wetu kwenye mengi, hawafai, wamemfanyia uhaini mwingi hawa jamaa, kumshauri vibaya raisi ni kukiuka state policy, ni aina ya uhaini. Hawa ndio zigo lote la mavi wadondoshewe.[...we ulionawapi ushauri kwamba raisi wiki nyingi hayuko nchini kwa matibabu marekani, huku nchi inafukuta na bunge linarindima, ni wazi raisi yuko well informed, kisha washauri wanamwandalia tamko la kuongelea safari yake tu na mbaya zaidi anasema ya bungeni hayajui, hii ni tafsiri mbaya sana, ni picha kwamba raisi akishapanda ndege hajui lolote kuhusu nchini yake, kwamba hata kama kuna mapinduzi yeye haelewi lolote, noooo no way hapa hawakumtendea vema raisi. Angepaswa kutamka wazi kwamba yanayoendelea bungeni yote ana taarifa nayo na taratibu zitachukua mkondo wake, that's a head of state statement, rather "i know nothing till reported and presented before me....!!?]. Tuendeleee na maprop wetu..

Ikumbukwe tokea juzikati aprili 2012. Prop muhongo alipoteuliwa uwaziri wa umeme na mawemawe amekuwa na mlolongo wa matukio na matamshi ambayo sikunyingi yalisha mnyima legacy ya kuwa kwenye kiti cha uwaziri huo wa nishati na madini. Jamani huyu purely ni professor sio mwanasiasa ni jembe kitaaluma. Dawati la utendaji ndilo linalo mfaa sio mchezo wa mdomoni.mara nyingi akiongea professor wetu huyu lazima ama atukane, ama akashifu watu, sio mara chache alishasema watanzania wavivu wa kufikiri (including yeye yaani mtu anajitukana hadi yeye), alishawahi kuwaita viongozi wa dini mambumbumbu, alishatoa matamshi yanayochochea kero iliyosababaisha vifo na vurugumai kubwa huko gesini mtwara wote tunajua hili, uanasiasa wa professor huyu mapemaa ulishaonekana ni sumu na majanga. Washauri wa raisi wangeliona hili mapemaa na wangemuondoa na kumwachia majukumu ya utendaji tu. Kali zaidi juzi kwenye kikao cha bunge alikurupuka sana kuongea tu bila data,katia viingereza vingi vikamgomea, kila anachosema vijana wanampinga kwa data. Nashangaa jamaa bungeni yumo tu hatoki sio kwamba ana ngozi ngumu wakati mwingine network si bure zimeshakatika, we uone watu wanagaragaza cv nzito ya uprofessor kama bata aliye choka utakuwa na akili bado!!.

Washauri hawa wa raisi wetu wamesababisha maafa na ulemavu kwa professor wetu huyu. Kwenye fani za ujenzi tunasema mhandisi mwenye lezeni yake akisanifu majaengo yakaleta hitilafu kidogo hapana kungojea hadi yauwe wananchi ananyang'anywa leseni yake faster anabakia fundi mchundo, iweje raisi ashindwe mapema kushauriwa amuondoe haraka waziri huyu. Bora angepewa hata ukatibu mkuu somewhere jamaa jembe kwenye kazi. Ulionawapi mtaalam huyu wa miamba ati leo anapiga dili za udalali ofisini, what a life shame! Wengine hamjui hili kwamba prof. Sospeter muhongo alishatunukiwa tuzo ya kimataifa ya kisomi ya mfalme napoleoni ijulikanayo kama 'ordre des palmes académiques (order of academic palms)' toka serikali ya ufaransa. Hii ni kutokana na mchango wake wenye ufanisi duniani katika medani za sayansi, teknolojia na ubunifu. Mtu huyu ni wa kuketi kwenye dawati akipanga ubunifu wa teknolojia ya miamba atusaidie kuokoa mabilioni ya shiilingi yanayopotea kwenye wezi wa rasilimali zetu, ati tunaambiwa leo anapiga dili za wizi na udalali ofisini??!! Inaumaje..!

Nilikuwa sijabahatika kumwona live professor tinaijuka akiongea kwenye majukwaa ya kisiasa, nakumbuka chadema walifanya mkutano mkubwa viwanja vya jangwani sikumbuki lini uliofana sana, baadae chama hiki nacho kikajibu mapigo kwa kuwasombelea watu uwanjani. Kitu kikubwa kilichonivuta uwanjani ni kumsikia professor anna kajumulo tibaijuka akiongea. Nadhani wote mliokuwepo mlishuhudia low and speechless ever from the professor. What i learnt from that day wasomi wa ukweli haipendezi kuwaharibu siasani. Can you imargine, professor mzima by her name anakiri kupokea tsh1.67 billin, tanzanian money, no no hata kama sio tanzanian money let say somebody kuku au bata flani from country code xxx amempatia tu, tsh 1.67 ??!!, then brofessor anadai kazipeleka kwenye biashara ya shule not research inakujia mkichwa kweli?. Anaropoka zinasaidia watoto wasio jiweza shuleni, but madam professor ada ya mwanafunzi kwenye shule yako ni 4.4million then inamaana maskini wa tanzania mtoto wake anasoma kwenye shule zenye ada staring from 4.4 . Mambo ya kutisha kabisa.

Jambo nalosema ni kwamba wasomi wetu hawa wazuri wameharibiwa na serikali hii. Serikali imwavuruga, kuwachanganya, kuwadhalilisha kiasi hawajielewi. Hivi nikisema chama chetu hiki ni mashine ya kuharibu wasomi ntakuwa nakosea?. Kati ya maprofessor wanne kwenye serikali nzima nusu yake yaani wawili wawe majanga hii si hatari kubwa sana. Hata hao wengine pindo za nguo zao hazijafunuliwa peupe tu..

Sijikiti sana kwenye dhima nzima ya ukwibaji wa mashilingi hayo kwa sababu sidhani kama ni jambo geni kwenye serikali hii iliyojaa uvundo wa kukwiba pasipo kukemeana. Serikali ina matrillioni so watu wanachota tu kila kukicha, basi tu bahati mbaya hiyo imewadondokea hao. Serikali hii mwizi ni mfalme maskini ni kibaka. Ukiiba kuku unafungwa miaka ya mfano na kadiri unavyoiba sana kifungo kinapungua na ukiiba mabilioni hadi ulinzi unapewa. Tabia ya kuibia serikali haijaanza jana mnakumbuka mwalimu alisema kipindiflan serikali yake watu walikuwa wanakwiba tuu, mwasia mmoja kama leo akakwiba hadi akajisahau akaropoka "serikali yote ya mwalimu iko mfukoni mwake" mwalimu akastuka sana, he kumbe yeye na serikali yake wako kwenye mfuko wa mhindi mmoja, akakikarabati kiti chake cha uraisi sawia. Kwa sasa nchini ukikamatwa ukafikishwa kituoni, kisha wakakwambia vua viatu, toa ulivyokuwa navyo mfukoni, mwanaume ukatoa kitita burungutu msimbazi zimebabana za kutosha zikatua kwenye macho ya afande mwanaume utahudumiwa kama mfalme hapo kituoni. Kila afande ataunda ubest na wewe. Nchi hii ilishabadilika kuwa ya wenyenavyo, wasionavyo mtulie kimyaaaa ndio tafsiri ya amani yetu.

Tujitokeza sasa kuwatetea wataalam wetu hawa, tuhakikishe wanatoka kwenye siasa na kwenye chama hiki kichafu, kisha tuhakikishe hela zilizo wazuzua wakalewalewa na kuwa kama wasiojitambua zitaifishwe haraka, warudi kwenye senceship yao kama wataalam, bado tunawahitaji sana, taifa hili bado changa, taifa maskini, wasomi ni lulu kwenye taifa hili. Taifa gani lisilo linda wasomi wake hadi wanapata ukilema wa stress za maisha kiasi hiki???

Embu chapa nalo jr, kasinge, mahoro, mchemsho, aminiusiamini, puro, sikonge, manjagata, mckenzie, the red pen, mnyakwetu, pakawa natoka hapa, mingoi

na wengine haraka geuzeni mje huku jamvini mrekebishe rubbish mlizo andika, nyie ndio vinara wa kulifanya jamvi hili lionekane kama kijiwe cha wahuni na mataahira, wavivu wa kusoma na kuwaza. Huna haki ya kuccoment kama hujasoma maada. Hulazimishwi kusoma!!

hakikaki mr.raisi hata mimi sijamwelewa alimaanisha nini kusema kuwa hana taarifa.
 
Last edited by a moderator:
Hawana elimu ya siasa, hawamuogopi Mungu wao. Hawajitambui wamekariri vitabu tu.
 
Kichwa cha habari na content ya maoni yako ni tofauti, ndio maana watu wengi wame critisize.Ila maoni yako ni sawia. Si vyema kuwafanya maprofesa kuwa wanasiasa.Angalia sasa walipoiweka Credibility ya wasomi wa kibongo!!

Unajua hata serikali yenyewe haipendi kusoma negative statement concerning them, wakiziona popote wanaziruka faster, ukitaka waisome lazima uiweke kinamna ionekane tamflan kinywani mwao na wakiianza kuisoma wanajikuta wanameza makavu that's the only brilliant way to send a direct sms.
 
Tugawieni na sie hayo mabilioni ndio tuwateee,,pumbavu zenyuuu
 
Back
Top Bottom