Tujitokeze kuwatetea Prof Muhongo na Prof Tibaijuka

Tujitokeze kuwatetea Prof Muhongo na Prof Tibaijuka

Mimi sikubali kuwatetea kama walishiriki kuchukua wakati mimi nahangaika na huduma mbovu za maji, umeme, mpango miji etc. Hivi mtu kupewa tani 1.6 (yaani 1.6 billion) unadhani mchezp enhee
 
Hata mimi ni proffesor

Andrea Chenge ni noma kweli!!

Zile za Mkombozi bank walizogawiwa kwa wire transfer akavuta Tshs. 1.6bn na za kule Stanbic Bank za kubeba kwa magunia, Lumbesa, viroba na kisha kuzipakia kwenye matipa na mikokoteni akavuta. Na hatujui huko alivuta Bilioni ngapi!!

Halafu jamaa ndani ya Jumba Tukufu la Bunge la wananchi anapewa nafasi ya "Ku - formulate appropriate phrase" ya kumwelekeza JK namna ya kuwachukulia hatua wezi!!

Hivi ni vituko vya serikali ya CCM.................wizi wa kimfumo mpaka Rais Jakaya Kikwete mwenyewe mwizi......na mwizi aliyeko ndani ya Bunge kwa kilekile walichokiiba anampendekezea mwizi aliyeko magogoni namna ya kuchukua hatua!!
 
mpumbavu hata umtwange katika kinu upumbavu wake hauta mtoka.

mkuu TAMKO,chukua like za kianalojia 1000 kwa uzi wako. kuna tafiti nafanya na katika uzi wako hakika nimepata kujua hali halisi ya tafiti yangu,watanzania wengi ambao wanajiaminisha kuwa wao ni ''vichwa'' kupita wengine ukweli ni kwamba wao ni ''vilaza'' wa mwanzo kabisa,na hasa hasa humu JF, wengi wetu ni vilaza wa kupindukia.kama mtu unashindwa kusoma kahabari kafupi kama haka,je kama ukiteuliwa kuwa mwakilishi wa kwenda kuingia mkataba wa jambo fulani na ukakutana na nyaraka za mkataba huo zenye kurasa 1000 itakuwaje!!!???hawa ndio wale wanao weka saini kwa kuangalia ''kichwa cha habari'', ''utangulizi'', ama ''table of contents''.hatuwezi kuwa vichwa ama ''wasomi walioelimika'' kama tutakuwa watu wa kukurupuka na kuogopa kutumia mufa wetu kwa kusoma kwa umakini na kutafakari kwa umakini mkubwa sana.
 
KUTAPA TAPA TU...HII NDO BONGO NA BONGO INA WENYEWE KUMQ BQBQKO:teeth::teeth:
 
ni ukweli usiopingika kwamba wasomi wetu hawa wenye level za uprofesa na udaktari wa falsafa,wanaharibiwa sana na siasa wakishaingia huko.mimi naamani siasa tuwaachie wana siasa kwani kuna wanasiasa wengi tu ambao hawana madigirii na wanafanya vyema sana katika nyanja hiyo (mfano ni Mh. Mbowe)
 
jf watu hawasomi habari yote ila wanachangia kutokana na heading ya post..

Wengi wamehamaki bila sababu kwa kuwa tu hawakusoma habari yote.

Tuache uvivu wa kutokusoma na tuache haraka ya kucomment wakati hujasoma. Ni aibu.
Mtoa mada ameweka vizuri kabisa lakini watu wamekurupuka balaa.
 
Daaah.. Tatizo ni elimu au hulka..? Yaani uzi huu unasomwa na kutafsiriwa tofauti na maana yake halisi..! Na tunajiita GT humu ndani..! Au wengi wa walio-comment humu ni wa darasa la nne la sasa hivi..? Yaani TAMKO umeleta uzi uliojitosheleza ambao umetuonyesha tatizo tulilonalo sio kwa escrow peke yake.. Bali hata uwezo wa members kusoma na kuelewa mada iliojificha..
 
Last edited by a moderator:
Kwani aliyesema wao watakufa wakiwa mawaziri ni nani, taaluma zao bado zinahitajika hususani kwenye vyuo vikuu na ambako ndiko walikotokea la hawataki kurudi vyuoni basi waamue kuwa consultants kazi inawafaa sana hiyo lakini kwenye siasa inatosha watapakwa matope mpaka washangae.
 
Kama Umepokea Mgao ili uje kutetea hapa UMETOKOTA. Pesa zao kula maana ni jasho letu ila KAWAAMBIE WALIOKUTUMA kuwa HAWASAFISHIKI HATA KWA HERPIC POWER...

Jamani someni kwanza kabla hamjajibu. Bahati mbaya makala imekuwa ndefu sana, jitahidini kusoma yote kisha mtoe maoni yenu, la hamwezi iacheni bila kutolea maoni yoyote kwani mnaonesha uvivu wenu wa kusoma,
mnajiaibisha bure.
 
Imagine wewe ni mwanafunzi. Mbele yako kasimama profesa mwongo anamwaga lekcha. Lazima utakua unajiuliza mara mia mia kama anachosema ni kweli au ni uwongo.
 
Wakati nikipata elimu ya i-iv nilikuwa nafikiri prof ni mtu mwenye akili kuliko binadamu wengine. Cha kushangaza kumbe dawa ya prof mpeleke kwenye siasa anakuwa taahira mazima. Hivyo hatuna muda wa kutetea mataahira.
 
Kwa jinsi ambavyo mh. Waziri amepambana kuisafisha TANESCO hadi kuchukiwa na watu waasiolitakia mema taifa , lakini bado akaonesha kutotetereka, nashauri ateuliwe kuwa waziri mkuu katika uchaguzi mkuu utakaofqnyika oktoba, 2015 ili jitihada zake za kusimamia rasilimali za nchi zipate nguvu zaidi.
 
Kwa jinsi ambavyo mh. Waziri amepambana kuisafisha TANESCO hadi kuchukiwa na watu waasiolitakia mema taifa , lakini bado akaonesha kutotetereka, nashauri ateuliwe kuwa waziri mkuu katika uchaguzi mkuu utakaofqnyika oktoba, 2015 ili jitihada zake za kusimamia rasilimali za nchi zipate nguvu zaidi.

Naona baado mnaendelea danganya tuu
 
Back
Top Bottom