Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

yaani RTD ilikuwa ni balaa.
Ukiachilia mbali watangazaji mahiri
pia pakawa na kipindi cha benki ya CRDB...
Jingle yake ilipigwa na Sikinde na kuna kipande murua anaunguruma Benovilla Antony anasema...

Watu binafsi na wakulimaa
Na wafanya biashara
Na vikundi vilivyoahinishwa
Mnaweza kukopa CRDB...

CRDB ni chombo
Kilichoundwa Madhubuti
Kinachotilia mkazo
Maendeleo ya Umma

Nani anamkumbuka mtangazaji aliyekuwa anaongoza kipindi hichi?
Kilikuwa kinaanza saa moja na robo mpaka saa moja na dakika 45 jioni.

Dah!
Gang Chomba, sikuelewielewi ati?
Au nawe ulikuwa mtangazaji?
 
Last edited by a moderator:
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.

1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala

2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana

3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............

4, Khalid Ponera- Zilipendwa

5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari

6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo

7. Siwatu Luwanda

8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)

10. Salim Seif Nkamba

12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu

13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi

14. Ahmed Jongo- Mpira

15. Christina Chokunogela

16. Dominic Chilambo- Mpira

17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana

Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa

Mbona simuoni marehemu mzee wangu, Donati Kaishe?
Au mlikuwa hamjazaliwa wakati anatangaza?
 
Mbona simuoni marehemu mzee wangu, Donati Kaishe?
Au mlikuwa hamjazaliwa wakati anatangaza?

Enzi zipi hizo? za kina Sarah Dumba au Sango Kipozi...

Kuna wale wa Mwanzoni wa miaka ya 2002 huyu alikuwa jirani na maeneo ya City centre Josephine Liumba ''Machepele''
 
Tuanze na timu ya RTD...
1. Siwatu Luanda
2. Salama Mfamao
3. christina Chikonogela
4. Eda Sanga
5. Deborah Mwenda
6. Aloisia Maneno
7. Sango Kipozi
8. Sarah Dumba
9. Betty Mkwasa
10. Halima Kihemba
11.Aloisia Isabula

SUB...
Domitila Urassa, Shida Masamba, Rsemerry Mkangara, Nyambona Masamba, Thekla Gumbo, Faudhiat Ismail Abood
 
Tuanze na timu ya RTD...
1. Siwatu Luanda
2. Salama Mfamao
3. christina Chikonogela
4. Eda Sanga
5. Deborah Mwenda
6. Aloisia Maneno
7. Sango Kipozi
8. Sarah Dumba
9. Betty Mkwasa
10. Halima Kihemba
11.Aloisia Isabula

SUB...
Domitila Urassa, Shida Masamba, Rsemerry Mkangara, Nyambona Masamba, Thekla Gumbo, Faudhiat Ismail Abood


Clouds mavi matupu.
Nao waweke kikosi chao
 
hawa walikuwa magwij mfano hamna namkumbuka kipindi cha jungu kubwa kila jumamosi ilikuwa na mtangazaji moja maarufu.jina imenitoka kidogo
 
Blandina mungezi yupo British Council, Dar es salaam. Alikuwa na sauti nzuri sana yule dada.
 
Kuna tetesi kua Sunday Shomary alikua aki-share love na Monica Mfumia.
 
Mmenikumbusha mbali, hadi machozi yamenilengalenga. Nakumbuka jinsi redio zilivyokuwa zinakoroma ukiwa vijijini. Wakati mwingine inabidi iwekwe juu ya jiwe au mti ili kupata mawimbi ya sauti vizuri. Basi wakati wa taarifa ya habari, hata kama mlikuwa na mkutano wa kijiji inabidi usitishwe kwanza musikilize baba wa Taifa kasema nini siku hiyo. Jamani, tumetoka mbali sana.
 
Back
Top Bottom