Tujikumbushe wana Azania

Poa mwana ! enzi hizo Mchwampaka ! aliwakamata madogo wamewasha moto kiwanjani saa sita mchana wanaota! kumbe walikuwa wanakamua jani kiulaini walipomuona wakatupa vipisi kwenye moto!

Heri hao wana busara. Kuna wale waliokuwa wanakaa kwenye yale mapango kule mpakani na Jangwani. Hawa walimwambia Mchwa arudi alikotoka tena kinyumenyume. Hiyo kwata iliyotokea hapa ilikuwa ya aina yake. Hebu fikiria mzee mzima Mchwa akipiga ligwaride kinyumenyume mpaka maeneo ya bweni!Hii sidhani kama alimhadithia kaka!Hivi nani anaikumbuka na ile stori ya Mchwa kumwambia kaka kuwa ameriona rianafunzi rinatishia kumpiga kaka na bastora?
 
Wewe lazima utakuwa kwenye late 50's!! duh, mazee, wewe ni mkuda na mnoko flani hivi....hooooooovyo sana kujifanya siriasi wakati wote!!

tulia, upo kwenye web hapa! kama hupendi hizi za shule, basi nenda kwenye zile za EPA!! mijitu mingine bwana, buree ghali.:(:confused:

umeona ehhhh yaani halafu wanatu force na sie tuwe wa miaka ya 50's huko kama wao n kupenda habari wapendazo wao tu
 
Ha ha haaa...

Huwa kuna walimu wawili nawakumbuka sana:

1)Mwalimu Mosha - Huyu mwanzoni alijaribu kufundisha physics. Basi huwa alikuwa anauliza swali hilo hilo kila mwanzoni mwa kipindi "hivi mnajua kwa nini shillingi inazama lakini meli inaelea (lafidhi za kichaga)?" ...Halafu anafungua briefcase yake na kuanza kuuza pastpapers kwa muda wote wa kipindi uliobaki. Mwishowe walikuja kumbadilisha na kuanza kuanza kufundisha Civics. Yaani huko ndio ilikuwa mambo ya kuuza papers toka mwanzo mpaka mwisho wa kipindi.

2) Huyu mwalimu jina lake limenitoka kidogo. Alikuwa anafundisha physics. Yeye alikuwa akiingia darasani anakuja na sauti kali sana ya mkwara "Father = mother!".... akimaanisha F = MA (Force = Mass x Acceleration). Halafu anatoa mfano "mko kwenye basi mnakwenda temeke, dereva anafunga breki ya ghafla, na abiria wote wanasukumana kwenda mbele. Dereva anasimama, nyinyi mnang'ang'ania kutaka kuendelea na safari.".... halafu kwa sauti kubwa anasema "FORCE....FATHER = MOTHER"... anafunga Aboti lake....huyo anachukua zake time....kipindi kimeisha. ha ha ha

By the way, Mwl Mitimingi alipata nafasi ya kwenda kujiendeleza UDSM. Baada ya hapo sidhani kama alirudi kuendelea na ualimu.
 
na kulikua na wale maticha wawili walikua wanapatana kinyama even if wana vipindi vya mwanzo wako radhi wakose darasani but kwenda kuwaadabisha ma njuka wapya waliokuja late shuleni ambao hawakupata number...
i remember one day wakiwa darasa lingine wanachapa wachelewaji kupata sifa wao ndo walimu wakali azaboy,akatokea monitor wa form 1 nyingine akamwambia mmojawapo ya ma ticha kuwa ana kipindi kwao...ohh si ikawa vagi,yaani wewe mtoto unanifundisha mie kazi?kwani umeambiwa mie sijui kama nina kipindi kwenu??kesi ikahamia kwa mtoto wa watu maskini ya mzungu
 
1. Mwalimu Ibara (Hatibu) - ticha huyu alikuwa anatumia ibara/vifungu hewa vya Katiba kutoa adhabu za kiutani ila wanafunzi tulikuwa tunazitekeleza kweli mfano aliwakuta wanafunzi wanagombana akawapa adhabu ya kufagia darasa mpaka ligi kuu ya Tanzania na mwaka huo simba na yanga zilikacha kucheza mchezo wa ligi hivyo ligi haikuisha...

2. Mwalimu Miti Mingi - huyu na Mchwa Mpaka walikuwa damu damu katika harakati za kuvunja miiko ya HakiElimu na Kuleana ya 'Chapa Kazi Sio Mtoto', da Miti alikuwa na kasauti kaupole hako ila akikucharaza bakora ilikuwa balaa...

3. Mwalimu Mbaga - mzungu wetu huyu alikuwa mpole sana utadhani hua ila utundu ukizidi darasani alikuwa anaita walimu wakali watuchape ila ikifika fimbo ya pili utasikia mama wa watu anasema 'basi chapa tosha tosha'...

4. Mama Semhando - huyu mama alikuwa anatoa somo la Kiswahili la aina yake, ukiwa njuka lazima akutoe mbele ya darasa na akupe neno ulielezee mbele ya darasa...

5. Mwalimu Matley - da mwalimu wa namba huyu alituchapa sana huyu kidato cha kwanza ila akawa besti sana kidato cha pili, nakumbuka sana maswali yake ya vidoti...

6.Mwalimu Mashanga - kinara wa migomo ya walimu, aliitetemesha sana sirikali...

7. Mama Idi - huyu alikuwa my fevoriti maelezo zaidi baadae...

Hahahha!! Umenikumbusha mbali sana!!!!!!!!
Mwaliu Hatibu alimkuta mshikaji amekaa juu ya meza, akamwambia kipindi chote akiwa anafundisha jamaa akae kwenye meza na kuandika kwenye kiti! Halafu hatanii, lasivyo viboko! Mama Mbaga yeye alikua wa Historia, mwalimu safi sana. Binti yake alikua mzuri sana. Haahahha!!! Matley alikua na mikwara sana, akiingia darasani kidacho cha kwanza wakati ule du, Maswali ya nukta na ku-proove 1=2.
 
Eeeeee bwanaeee,Mchwampaka alikuwa noma kichizi;ila kuna mwalimu wangu alikuwa anatufundisha physics Mwl.Mosha alikuwa peace sana;tatizo lake ni kwamba alikuwa napenda sana kuvuta fegi mara anakohoa mara samahani kidogo kumbe anaenda kuongeza nguvu kwa madai yake huku hajui kama anajiua mwenyewe taratibu.
Kiboko ya wote kuna Mwl.Matey alikuwa anatufundisha ugonjwa wa Taifa,acha kabisa ukichemsha katika hilo somo mwenyewe unakosa amani kabla hata hujaonana nae alikuwa anachapa bakora vibaya,utasikia shika meza nyooka ukijitia hujui anakuondoa stand;watu wengi walikuwa wanamnyaa huyu mchizi ile mbayaaaaa.
Chama letu lidumu zaidi na zaidi maana yake tumetokea mbali Azania Boys hadi hivi sasa sijui ni nini vile maana wamechanganyika na mademu duh!

Azania imechanganyika na mademu? Hii kweli balaa! Yani hamna hata fleva tena ya chama letu!! Mimi nakumbuka kiunganishi mashuhuri cha mwalimu Mitimingi hasa, akiongea kiingereza. Badala ya kusema kiufasaha 'another thing' alikuwa akitumia sana neno 'anaza sing' , basi kwetu ikawa kila akija skuli balaza inakuwa tunamwita anaza sing.

Halafu kulikuwa na nunda fulani pale shule linaitwa "batman", sijui bado lipo maana nakumbuka kuna siku lilimzaba Mchwa bonge la kofi kwenye school baraza.I wonder litakuwa lina shughuli gani siku hizi.

Mwalimu Kijazi wa Biolojia sijui bado yuko au vipi. NIlikuwa nammaindi sana, sema basi tu!

Mwalimu Dathi yule mhindi, sijui bado yuko hai, alikuwa mzuri sana wa Chemistry. NIkimuona tena lazima nimpe zawadi.

"Azania, Azania, Azania our school, we look at you with pride, you are known far and wide, you are always our best, we will never forget you",
Wana wa Azania mnakumbuka hii school anthem??

BIla kumsahau Mheshimiwa sana, mwalimu Kente mzee wa Mabuga!!
 
Yah sio kama ni wabaguzi wa gender ila flava la chama limepungua maana hata huwezi kuita AZABOY tena maana ndio hivyo tena.

Hivi huyu batman unyemsemea ndio huyu aliyemaliza miaka ya 94/95 alikuwa anatembea na paketi ya embassy kwenye mfuko wa shati.

Mama dathi yah alikuwa makini kwenye kemia.
 
Ndio huyo bat man mwenyewe maze!! alikuwa nunda sana. Sijui yuko wapi siku hizi!!
 
-skonzi za njano zilikuwa tamu: kuna denti alikimbia na fuko zima la mikate ya darasa!
-ligi ya shule ilikuwa supa: kabla ya mechi lazima tupate ugali na nyama za moto hizo!
-timu ya shule ilikuwa kali: kulikuwa na mshambuliaji machachari 'kimti' & beki 'jagner'!
-dibeti zilikuwa inglishi richabo: kina wange'nge Seba Ndege, Nizar & Michael walitesa!
-walimu walikuwa wamepinda: kulikuja ticha 80% ya kipindi ni stori za 'zero distance'!
 
Wandugu naomba tujikumbushe miaka ile wale tuliopitia Azania sec .Mimi nilikuwa pale intake ya 1990-1993 na inaniwia vigumu kusahau ile experience ya watu kama mzee Meja,mkuu wetu Massawe,mzee Mchwampaka na wengineo bila kusahau kia dume
 
Mimi nimesoma enzi za Kwayu akiwa head master ,mama Massawe akiwa second mis. Mchompaka (MchwaMpaka) huyu alikuwa noma akiwa dicpline master na kanifundisha geography,Mkongo,Mitimingi,Mosha,mama wa kihindi Dath chemistry.........,
 
Nimekusoma mkuu wakati Kwayu anakuja sisi ndio tulikuwa tunamalizia basi wacha atutandike mijeledi maana sheria yetu ilikuwa hatuchomekei mashati na yeye anasema a smart guy has to tuck in his shirt basi tulikoma mkuu.Mama Massawe alikuwa bado hajawa second ila Mitimingi alikuwa mtaalamu mzur sana wa book keeping vipi na chips dume bado zilikuwepo
 
duh nikula hiyo kitu mpaka basi kulikuwa na jamaa pale barabarani alikuwa anaindwa kizika alikuwa anakaanga ogo la maana na chachandu ya ukweli ,pembeni alikuwa jamaa anauza juice ya ndimu tulikuwa tukimwita mkemia maana ilikuwa ikinoga ikichanganya anaitia na rangi yaaah.
Ila pia nilikuwa najichanganya kula chakula cha shule pia kwa jamaa wa hostel harage ugali aa.
 
jamani na mi nimo,nimepiga O'level na nimemaliza seven years ago,Kwayu akiwa headmaster! Muchwampaka kipindi hicho alishakuwa mpole baada ya kupiga mtoto wa watu na kumalizia nguvu za kiume! Tuliacha simba mmoja anaitwa Mulokozi,huyu tabu tupu..muchwampaka haoni ndani! Kipindi chetu kule 'msituni' waliweka "vimbweta" so tulikuwa tunakula stori na buku huko,alafu kulikuwa na mbu wana hasira..wakikung'ata..!! Kulikuwa na 'POGO' aka mihogo ya jamaa m1 alikuwa anaitwa "husein" na vidagaa vya kukaanga. Aisee,studying Azania was a wonderful experince in real life ya mtoto wa kawaida kabisa wa kibongo!
 
duh Mchwampaka ndio wamemtenda hivyi dah ,ila alikuwa kappitiliza yule bana!
 
yep nililikwa mitaa ya pale AZaboyz.....1998-2001..........i just end gettin a thrill when i remember those days.....R.I.P... wale makamanda waliotutoka....
 
makitaja Azania sijui najisikiaje, mdogo wangu alimaliza pale 2003 ila hizo bangi anazopuliza ni balaa, na anasema walikuwa wanavuta hadi class
 
makitaja Azania sijui najisikiaje, mdogo wangu alimaliza pale 2003 ila hizo bangi anazopuliza ni balaa, na anasema walikuwa wanavuta hadi class

That is another case kama ilikuwa haimpendi alitakiwa kuonja na kuachawatu wengi wamepitia huo mkondo nawajua rafiki zangu wengi sasa ni watu wakutumainiwa wamepitia huo mkondo ,anyway I 'm very proud to kupitia pale .
 
Pamoja ndugu, mi nimemaliza o-level 93 nilikue E, nakumbuka jinsi tulivyokua na mchakato wa kuchagua nembo ya kuweka kwenye mashati maana b4 hatukua na nembo, nakumbuka nilikua fine arts that time, mzee meja alikua kiboko mzee wa kupokea form ones na kuwapa tour ya shule I really enjoyed vichekesho vyake na darasa la yule teacher wa history Mr Kente na mavazi yake ya miaka ya 47.LOL nikipita na kuona ukuta ule uliozunguka ile shule nawaonea huruma, sisi tulikua tunapiga kitabu kwenye ma-tembe kule groundini na kula sana msosi wa jamaa wa boarding jioni.LOL Big up aza boys. aah nimesahau na macho ya mchwampaka noma unaweza ukadhani anaangalia pembeni kumbe anakucheki wewe, hahahaaaaa.
 
Sintosahau hili chama mazee,mi nilikuwa hapo from form one till form six.kipindi cha kina kwayu,mkongo,mchwampaka,maleko,matley.dath,charles,n.k.but it was a great experience being there meeen.One thing i remember about Azania is...you can be whoever you want to be...i mean ukitaka kuwa Kichwa unapiga div one point seven form four unaweza coz kuna watu wanastruggle sana katika books.
on the other hand ukiamua kupiga division zero pia unaweza coz kuna watu kazi yao ilikuwa kuvuta bangi na kufanya fujo tu.

Nakumbuka tuition za mchikichini a.k.a mbuzi area...
michezo ya UMISETA
Hostel za Azaboy
Misuli tuliyokuwa tunapiga na washkaji wote..

nakumbuka tuition ni muhimu kwa azania kuliko vipindi vya darasani,na ikija pepa ya taifa tulikuwa tunafumua kweli.

I can't forget azania coz imenifanya niweze kusoma shule katika mazingira yoyote yale.

Viva Azania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom