Tujikumbushe wana Azania

Ahaa Kweli hiyo stori ya Mchwa-Mpaka ilikuwepo tehe tehe tehe

Huyu alikuwa discipiline master matata sana kipindi chake ,alikuwa na kigugumizi pia bigwa wa reverse stori zake ukihadithiwa unaweza kudhani ni za kubuni ila ni amini na kweli maana alinifundisha Geoghaphy.Ilikuwa akimwita head master wa Azania enzi hizo Mr.Kwayu kaka!.

Habari yake nyingine nayokumbuka ni baada mechi ya mpira kuisha jioni kunako Pugu na giza ukingia alimkimbizwa na kuchapa bakora sana ila cha ajabu hakuhadithia kesho yake alibaki kumsifia kipa wetu kuwa "alikuwa anapiga mpira kisha anadoka huku akionyesha kudaka ndio kupiga na kupiga ndio kudaka" alikuwa bigwa wa reverse hakika.

Namkumbuka Mwl.Mkongo alikuwa safi sana,kulikuwepo na walimu walevi kama Mushi wa Physcics,.........kulikuweko na Huyu aliyekuwa anaitwa primus ,na Tokyo kwa kupenda kuvaa suruali za chata la tokyo ahaaaaaaaaa.Kulikuwepo na Hatibu nadhani huyu alikuwa anapenda sana michezo.Tulikuwa na mama huyu wa kihindi (Dhasi)alikuwa mzuri sana kwenye chemistry bila kusahau mama Shija mzuri mno kwenye chemistry alikuwa akifundisha A'level.Kulikuwa na mama kiarabu pia akifundisha Math.

Kuna yeyote anakumbuka maneno haya
msuli kitanda,msuli tamaa,sodoma ,gomora,masaki,mirembe
Nakumbuka kipindi chetu tulikuwa na umoja sana pale,we have a lot of funy things also kuna watu nimewakumbuka sijuhi wako hapi kuna haja kutafutana .

Namkumbuka Nyau huyu alikua anafundisha Biology, kipindi hicho alitokea tambaza baada ya tambaza kufungwa kwa muda, kuna Robort huyu alikua anatukimbiza hadi muhimbili, kuna Ryoba alikua poa sana, tokyo namkumbuka sana alikua mshakaji kweli vipi mnaukumbuka mti mawazo pale nje ya hostel?
 
Eeeeee bwanaeee,Mchwampaka alikuwa noma kichizi;ila kuna mwalimu wangu alikuwa anatufundisha physics Mwl.Mosha alikuwa peace sana;tatizo lake ni kwamba alikuwa napenda sana kuvuta fegi mara anakohoa mara samahani kidogo kumbe anaenda kuongeza nguvu kwa madai yake huku hajui kama anajiua mwenyewe taratibu.
Kiboko ya wote kuna Mwl.Matey alikuwa anatufundisha ugonjwa wa Taifa,acha kabisa ukichemsha katika hilo somo mwenyewe unakosa amani kabla hata hujaonana nae alikuwa anachapa bakora vibaya,utasikia shika meza nyooka ukijitia hujui anakuondoa stand;watu wengi walikuwa wanamnyaa huyu mchizi ile mbayaaaaa.
Chama letu lidumu zaidi na zaidi maana yake tumetokea mbali Azania Boys hadi hivi sasa sijui ni nini vile maana wamechanganyika na mademu duh!

sasa hvi hakuna mademu mkuu
 
Wewe lazima utakuwa kwenye late 50's!! duh, mazee, wewe ni mkuda na mnoko flani hivi....hooooooovyo sana kujifanya siriasi wakati wote!!

tulia, upo kwenye web hapa! kama hupendi hizi za shule, basi nenda kwenye zile za EPA!! mijitu mingine bwana, buree ghali.:(:confused:

Hahahahahaaaaa
 
kwa wale tuliosoma juzijuzi mnamkumbuka mwalimu Chambala wa civics,mzee wa utani akifundisha civics usipocheka kwenye mifani yake bac wewe noumaa. naskia mchwa mpaka alifariki.
 
Azania of today Azania yesterdayyy,Azania,forever,we will always sayy,you are known far and wide you are always our Guide, We will never forget you. hicho ndo kipande cha wimbo wa shule.kuna watu walimaliza hawaujui wimbo wa shule na wengine walikua wanategeshea sehemu za kumalizia tu"We will never forget you" so funny moments
 
Azania of today Azania yesterdayyy,Azania,forever,we will always sayy,you are known far and wide you are always our Guide, We will never forget you. hicho ndo kipande cha wimbo wa shule.kuna watu walimaliza hawaujui wimbo wa shule na wengine walikua wanategeshea sehemu za kumalizia tu"We will never forget you" so funny moments

hahahahaaaa
 
1. Mwalimu Ibara (Hatibu) - ticha huyu alikuwa anatumia ibara/vifungu hewa vya Katiba kutoa adhabu za kiutani ila wanafunzi tulikuwa tunazitekeleza kweli mfano aliwakuta wanafunzi wanagombana akawapa adhabu ya kufagia darasa mpaka ligi kuu ya Tanzania na mwaka huo simba na yanga zilikacha kucheza mchezo wa ligi hivyo ligi haikuisha...

2. Mwalimu Miti Mingi - huyu na Mchwa Mpaka walikuwa damu damu katika harakati za kuvunja miiko ya HakiElimu na Kuleana ya 'Chapa Kazi Sio Mtoto', da Miti alikuwa na kasauti kaupole hako ila akikucharaza bakora ilikuwa balaa...

3. Mwalimu Mbaga - mzungu wetu huyu alikuwa mpole sana utadhani hua ila utundu ukizidi darasani alikuwa anaita walimu wakali watuchape ila ikifika fimbo ya pili utasikia mama wa watu anasema 'basi chapa tosha tosha'...

4. Mama Semhando - huyu mama alikuwa anatoa somo la Kiswahili la aina yake, ukiwa njuka lazima akutoe mbele ya darasa na akupe neno ulielezee mbele ya darasa...

5. Mwalimu Matley - da mwalimu wa namba huyu alituchapa sana huyu kidato cha kwanza ila akawa besti sana kidato cha pili, nakumbuka sana maswali yake ya vidoti...

6.Mwalimu Mashanga - kinara wa migomo ya walimu, aliitetemesha sana sirikali...

7. Mama Idi - huyu alikuwa my fevoriti maelezo zaidi baadae...

Haha haha haaaa! umenikumbusha sana HATIBU _ "Nipe sababu kuu kumi zenye mantiki kwanini niiikuchape ukianza na neno kwakuwa" ilikuwa si mchezo, hapo mzee sababu hujachomekea kaa! hapo anaangalia kama anasinzia vile
 
azania of today azania yesterdayyy,azania,forever,we will always sayy,you are known far and wide you are always our guide, we will never forget you. Hicho ndo kipande cha wimbo wa shule.kuna watu walimaliza hawaujui wimbo wa shule na wengine walikua wanategeshea sehemu za kumalizia tu"we will never forget you" so funny moments

nakumbuka enzi hizo akina dr. Sebastian ndege wanaimbisha
 
Haha haha haaaa! umenikumbusha sana HATIBU _ "Nipe sababu kuu kumi zenye mantiki kwanini niiikuchape ukianza na neno kwakuwa" ilikuwa si mchezo, hapo mzee sababu hujachomekea kaa! hapo anaangalia kama anasinzia vile

Hahahaaaaa
 
da mimnakumbuka enzi za mkongo, chavila na ticha fulan alikuwa aki2fundisha history hiv sijui nani vile ye alikuwa akiingia darasani vijana 2lkuwa 2 na a ngalia makalio 2 maana alikuwa ameumbika kidizain. na mwalimu fulan alikuwa akiitwa t makinge ni ticha fulun mfupi lakin anafundisha geography safi sana.hivi ngoziye yupo maana nakumbuka alikuwa mgonga lebel we2 yaan akikukuta huna lebel anakufoce upige lebel hata kwa mkopo
 
da mimnakumbuka enzi za mkongo, chavila na ticha fulan alikuwa aki2fundisha history hiv sijui nani vile ye alikuwa akiingia darasani vijana 2lkuwa 2 na a ngalia makalio 2 maana alikuwa ameumbika kidizain. na mwalimu fulan alikuwa akiitwa t makinge ni ticha fulun mfupi lakin anafundisha geography safi sana.hivi ngoziye yupo maana nakumbuka alikuwa mgonga lebel we2 yaan akikukuta huna lebel anakufoce upige lebel hata kwa mkopo

Hahahahahaaaa Ngozie head master now mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom