Tujikumbushe uhusiano wa Kikwete, Rostam, Ngeleja na Rweyemamu kwenye suala la DOWANS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe uhusiano wa Kikwete, Rostam, Ngeleja na Rweyemamu kwenye suala la DOWANS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 15, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Wenye data za uhakika kuhusu uhusiano wa hao jamaa wamwage hapa.

  Kuna tetesi kwamba rostam ndiye aliyebeba fungu la kampeni za kumweka madarakani jk na ndiyo maana alipewa cheo cha mweka hazina wa ccm. Ngereja alikuwa mwanasheria wa vodacom ambayo rostam ana hisa kubwa. Kwa hiyo, nguvu inayomweka ngereja kwenye uwaziri tena wa nishati na madini ni rostam aziz ili alinde maslahi yake. Tukumbuke kuwa rostam ndiye anayemiliki mitambo mikubwa ya kuchimbia madini kwenye migodi kadhaa nchini.

  Salva rweyemamu ndiye aliyefanya mipango ya rostam kuuziwa Habari Corporation ili kuvunja mtandao wa kuikosoa serikali ili ifanye mambo yake kwa amani. Baada ya kuuzwa, salva na mwenzie gideon shoo walianzisha kampuni ya ushauri wa mambo ya habari na akaingia mkataba na rostam wa kuilinda kampuni ya richmond dhidi ya mtazamo hasi mbele ya wananchi kwani tayari kelele zilikuwa tayari zimeanza kusikika mitaani kuhusu uhalali wa kampuni hiyo. Inasemekana hata wakati majenereta ya kufua umeme yalipokuwa yanaingia nchini, salva ndiye aliyeratibu ziara ya wanahabari kutoka vyombo mbalibali kwenda uwanja wa ndege kushuhudia.

  Baada ya jk kuingia madarakani alimteua salva rweyemamu kuongoza kurugenzi ya habari ya ikulu na hadi sas ndiye anashikilia cheo hicho. Lengo likiwa lilelile la kulinda maslahi ya wakubwa wakiongozwa na RA.

  Katika mtiririko huu, ndugu zangu mnaweza kuona kwa nini baadhi yetu tunasema siku zote kwamba RA ndiye kiongozi mkuu wa nchi hii. Ndiye anayeamua nani awe waziri na wa wizara gani kwa maslahi yake na mafisadi wengine akiwemo na jk mwenyewe. Watanzania milioni zaidi ya 40 tunachezewa na kikundi kidogo tu cha watu. Wananchi maelfu kwa maelfu wanateseka vijijini na mijini kwa sababu ya uhuni unaofanywa na watu hawa wachache.

  Suala la Dowans ni miongoni mwa michezo mingi michafu inayochezwa na kikundi hiki kidogo kwa gharama na mateso ya wananchi. Wananchi tuzidishe kelele, tusikubali kuilipa Dowans.
   
 2. J

  Jukwaani Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa una point hapo umenena.

  Na ninachojiuliza inakuwaje tuna kuwa na msemaji Kimhindi cha bombey?? Huyo Rostam anatakiwa ajui mwisho wa uovu wake umefika na kama JK hata liona hili ni kwamba anataka hapa pageuke sudan na wasidhani tutawaacha hata kama watatoroka nchi.

  Wametuibia vya kutosha sasa tutajiongoza wenyewe. Wadufi wakubwa tena hawana adabu kabisa. Jamani hamasisheni watu wasome Jamii Forums watoe mawazo na ikiwezekana yarushwe hata kwa ku hijuk mitandao yao.
   
 3. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii nguvu na uvurugaji alio nao Rostam kwa uhai wa taifa letu ni hatari sana. Nchi ipo utumwani, chini ya mateka yake, na ni yeye Rostam anaamua kesho kifanyike nini ktk serikali ya JK. Hii ni hatari mno kwa uhai na ustawi wa taifa.

  Hii inanikumbusha mhindi mmoja kwa jina Kamlesh Patneh, aliyesababisha tafrani kwa Kenya kwa scandal ya Goldenberg, skendo ya utapeli mkuu wa deal za dhahabu Kenya, na hadi alipodakwa, mamia ya wakenya walimwagika mitaani wakimwagika machozi ya furaha na mayowe.

  Rostam alitakiwa awe ameshakamatwa. Ikiwezekana CHADEMA iitishe maandamano, kuomba interpol, CIA au hata Mossad vitusaidie kumkamata tapeli na fisadi huyu wa Iran anayejifanya katokea Tabora! Bila shaka uranium yetu ameshaiwahi, sasa inapelekwa Iran kwao kama ile ya Congo! inauma sana.
   
 4. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Bila kusahau kuwa rostam hawezi fanya kitu hadi apate kile Mwalimu nyerere alichokiita dodoki. Tuanza na dodoki rastam atabaki na nani?
   
 5. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Rostam ndiyo mfadhili wa system tanzania...so u cant do anything :love:
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ina maana hata bajet anapanga yeye?
   
 7. p

  peterslayer Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Word on the street ati Ngeleja alikua nyoka wa Rostam? In the sense kama employee? Kwamba kawekwa na network ili ku seal deal ya malipo ya dowans/ richmond settlement.
   
Loading...