Interested Observer
JF-Expert Member
- Mar 27, 2006
- 2,657
- 3,035
Rev. Kishoka,
Nafikiri ilipofikia kwa nchi yetu ni kutokumwamini mtu mpaka imeonekana wazi hana madhambi.
Kwa muda mrefu nimekuwa mtetezi wa prof. Mwandosya kwa kutumia knowledge ndogo niliyo nayo juu yake. Lakini baada ya kushuhudia yale yanayojitokeza juu ya madhambi ya serikali ya awamu ya tatu, naanza kuwa na wasiwasi na watu wote waliokuwa na nafasi muhimu kwenye hiyo serikali.
Njia pekee ya kurudisha imani kwa sisi wananchi ni kwa wahusika wote kuchunguzwa ipasavyo ili wale wazuri wawe cleared.
Mwanahabari anasema deal la radar lilifanyika wakati prof hayuko madarakani, hiyo ni kweli, lakini pesa zililipwa wakati yeye yuko madarakani. Pia yule Mhindi alilipwa commission yake mwaka 2001 wakati prof. Mwandosya ni waziri. Je wakati anatoa mgawo, yeye prof. hakuambulia kitu?
Kwenye suala la TTCL, mimi niliwahi kufuatilia karatasi kwa karatasi. Kule timeline inakataa na nina uhakika kwamba uhusika wake ulikuwa wa kubambikiziwa zaidi ya ukweli.
Ununuzi wa ndege ya rais ulikuwa chini yake, je huyo Mhindi hakumkatia kitu?
Mtanzania, people here think this prof is clean, Mmmmm, better ask Mo Ibrahim, how much he spent on the prof. You remember the Mwanza speed boat boats saga, how he went fists with Magufuli!! Open your minds, with CCM no clean fish, all rotten!