Huyo mzee hana lolote! Si alikuwa madarakani mihula yote, alikuwa hayaoni hayo maarifa?
Samahani nimechagua tu kuku-quote wewe ila wengi wamekuwa na mawazo au mtizamo kama wako dhidi ya huyu mzee wetu Kingunge Ngombare Mwiru
Ni kweli kuwa mzee wetu huyu anahusika kwa sehemu kubwa sana kwa taifa letu hili kuwa hivi lilivyo leo kwa kuzingatia nafasi na heshima aliyokuwa amepewa tangu ujana wake alipojitokeza kuwa mtu maarufu hapa TZ na nadhani hadi nchi majirani zetu....., Nakumbuka jina Kingunge kuna wakati lilimaanisha mtu mzito/kigogo..., Mfano utasikiwa watu wanasema aaah!! jamaa yule bwana ni Kingunge kwelikweli.. au utasikia Kingunge wa Tanzania ni..., au Kingunge wa Kenya ni..., Uganda..., n.k. Hii yote nimeamua tu kuonyesha jinsi mzee wetu alivopata fursa ktk taifa letu. Kwa bahati mbaya kabisa inawezekana kuwa mzee wetu huyu kwa makusudi, au kutotambua hiyo fursa, au kwa kubanwa na mfumo au vinginevyo kabisa mawazo anayoyatoa hapo juu kama aliyatambua akiwa bado yungali na nguvu hayajalisaidia taifa letu kwamba sisi hatukuiga MAARIFA ya wazungu badala yake tumeiga LUGHA yao....kwa mujibu wa mzee Kingunge...
Pamoja na udhaifu wake huo, mimi naona nimshukuru mzee Kingunge kuwa hajataka kuondoka ktk taifa hili bila kutuachia kipande cha maneno haya ya hekima...kwamba tunatakiwa tuige MAARIFA ya wazungu ili tuendelee... Ni wajibu wetu badala ya kumbeza tuu tuchukue haya maneno yake na tuyafanyie kazi..tuweke strategic plans and action plans on how we can make these words BECOME true and reality ktk nchi yetu. Siyo sahihi sana kumpuuza kabisa mzee wetu huyu, huenda ametambua makosa yake na anaona basi atupe hayo yatusaidie. Hata mwalimu Nyerere alikiri kuwa wakti wake walifanya mazuri na makosa pia..akatushauri tuchukue mazuri tuyaendeleze na makosa yao iwe ni fursa ya kujifunza na kufanya marekebisho twende mbele...Ila akatushangaa pia kuwa tunaacha yale mazuri na tumeamua kuchukua makosa yao....
Mimi nataka niongezee kidogo ktk hayo maneno ya huyu mzee si kwamba tunaiga lugha ya wazungu na kupenda rangi yao tu..Sisi TUNADHANI ILI TUENDELEE TUNAHITAJI MISAADA YA HAWA WAZUNGU...na mbaya zaidi sisi tunadhani tunahitaji KUPIGA DEBE LA NGUVU KUZUNGUKA HUKU NA KULE ILI KUTAFUTA MISAADA YA WAZUNGU... Cha kushangaza kama mzee Kingunge alivosema HATUHANGAIKI KUTAFUTA HAYO MAARIFA YANAYOWAFANYA WAZUNGU WAWE NA MAENDELEO... aaaaah bali kwetu muhimu ni MISAADA eti tunajivuna na kusema MISAADA YA MASHARTI NAFUU.. Nadhani tunajidanganya wenyewe. Hivi hata ukipewa misaada kama huna MAARIFA itakufaa nini?
Kingine ambacho mzee hajakisemea ni kuwa SISI AU NISEME BADHI YETU (kwa bahati mbaya sana sasa ndo inaonekan ndo style ya viongozi wetu kuchangamkia uongozi) TUNATAMANI KUWA MATAJIRI BILA KUZALISHA... njia ambayo imechaguliwa ni ya kwa kupitia UFISADI... Hivi kuna msomi hapa anaweza niambia kuwa mtu anapoamua kufisadi fungu lililotengwa kwa project/program fulani hapo kweli anaelewa maana ya jambo analofanya? Hapo kweli mtu huyo ni msomi kweli.... Angalia yanayotokea sasa bungeni hivi hawa wabunge wetu wanajua kweli umaana wa wao kuwa viongozi. Fuatilia utagundua kuwa PESA ya serikali kwa ngazi zote ziko kwenye misukosuko mikubwa ya mbinu nyingi na kabambe watu wazifisadi na wafiche au wajipatie mitaji ya makampuni yao ya kishetani....
Kuna mamo mengi mzee wetu hakuyasema ila TUUUNGANE NAYE KTK HUO HUO UDHAIFU WAKE TUNAOUONA KUWA TUIGE YALE MAARIFA na siyo hizi harakati na mashindano tunayoyashuhudia ya kufisadi taifa letu kwa kila mbinu kwanza hata huyo FISADI kama anaona mbali hata hiyo pesa anayokwapua haifaidi..ni nyingi mno kwa mahitaji yake hapa TZ... ni lawama za bure na tamaa ya bure tu anajipatia... Pia ni ulofa wa hali ya juu na ndhani wazungu wanatushgaa na kutucheka sana... HIVI INAINGIA AKILINI KWELI TUNAPOKEA MISAADA TOKA KWA WAZUNGU AU TUNAIBA PESA YETU WENYEWE KISHA BAADHI WANAKWENDA FICHA KTK MABENKI YAO WAZUNGU HUKO ULAYA AU SIJUI USA HIVI WANADHANI HIYO PESA INAKAA TU BURE, INAKWENDA FANYA BIASHARAAA...NA HATA HAWA WATU WAKITAKA KUITUMIA NI KTK WOGOWOGA TU SASA RAHA HAPO IKO WAPI YA MTU KUWA NA MAPESA MENGI YA KIFISADI...Kwanini udharilike ukipita njiani watu wanakuona wewe ni FISADI, watoto wako wakitanua jamii inawaona ni za kifisadi... usituringie... na zaidi sana kuna CHUKI KUBWA SANA inajengeka sasa ktk jamii juu ya hao MAFISADI na watoto wao na wajukuu wa MAFISADI na hasa vijana..hapo hiyo si hatari huko mtaani jamani...
TUIGE MAARIFA na tuwe na MIKAKATI na MIPANGO KAZI na tuache KUTEGEMEA MISAADA haina tija kama hatuna MAARIFA... tuache UFISADI na tusiwe na TAMAA BILA KUZALISHA na tuache UVIVU tupambane na maadui wote wa maendeleo kwa kuchapa MZIGO/KAZI..
ASANTENI SANA