kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,512
- 2,730
Huwa sielewi, sijui tumelogwa? mbona hawa watu wakiisha toka kwenye system ndo huwa na mawazo mazuri? Nakumbuka Sumaye naye sikumoja aliwahi kusema, taifa haliwezi kuendela kama hatuuzi vitu nje ya nchi, kama tunanunua zaidi bila uuza then hatutakuwa na fedha za kigeni, aliendelea zaidi kwa kudai tujenge zaidi viwanda ili tupate vitu vya kuuza, ni huyu hyu aliyekuwa waziri mkuu wa muda mrefu kupita yeyote aliyewahi kukalia kiti hicho, swali, kwanini viongozi wengi wa magamba huwa wanaona kikwazo cha matatizo yetu mara baada ya kuachia madaraka?
Bila kujali historia yake huyo mzee (ambayo kwakweli huwa nasikia kichefu chefu, hasa baadhi ya kauri zake) aliyo yasema ndio ukweli, hivi mwaka 1988 pale kambi ya jeshi kibaha, wanajeshi wale (mainjinia) si waliweza kutengeneza Gari na wakalipa jina la Nyumbu? nakumbuka liliingia hadi kwenye maonesho ya sabasaba, enzi hizo maonesho yale yalikuwa na mvuto sana, hivi kama akina kingunge wangewaendeleza watu wale, leo situngekuwa tunatengeneza ndege? CDM, mkiingia madarakani 2015, endelezeni hili tafadhari!
Huwa ata mimi hii hali inaniweka ktk wakati mgumu sana kuwaelewa hawa viongozi,wanazungumza mipango mizur sn wakishatoka madarakani.