Tujikumbushe kauli hii ya Mzee KINGUNGE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe kauli hii ya Mzee KINGUNGE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijakazi, Jul 30, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Maoni ya Mzee Kingunge alipoulizwa kwa nini anafikiri Afrika bado iko nyuma!

  Alisema

  " Wakati wazungu walipofanikiwa na mapinduzi ya viwanda waasia wakajiuliza (wajapani) hivi ni nini siri ya mafanikio yao (yani wazungu) wakagundua kwamba siri yao iko kwenye maarifa, wakajifunza maarifa na wakatoka, wakaja wakorea wakajiuliza swali hilo wakagundua kwamba ni maarifa wakaiga wakatoka, wataiwani na wasingapore hivyo hivyo na sasa wachina nao wamegundua siri ya wazungu ni maarifa wameiga wanatoka ila Afrika akasema TUNAFIKIRI SIRI YA MAFANIKIO YA MZUNGU IKO KWENYE LUGHA YAKE NA RANGI YAKE kwa hiyo tunafanya kila tuwezalo kuwekeza katika hayo mambo mawili na ndio kilichotufikisha hapa tulipo"

  Hayo ni maneno ya Mzee Kingunge, nini maoni yako, unaafiki naye?
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwenye suala la maarifa yupo sahihi.

  Nyerere alisema "umasikini wa mawazo ndio umasikini mbaya san
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Yeye alifanya nini kama sio kuiga kuva manguo ya kichina

  [​IMG]
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wao si ndio wasisi, wamefanya nini kuwekeza katika maarifa hadi sasa wanamiaka 100+++.lol!
   
 5. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ameshazeeka huyo apumzike sasa!
   
 6. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimependa hayo maneno, yanafanana na hali halisi.
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu mzee mpaka leo bado ni mbunge wa kuteuliwa na Rais?
   
 8. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kingunge amekata shauri ama ameokoka?Sababu ninazo:
  Kingunge kasoma Russia yaani USSR tena Taasisi ya Heshima iitwayo Patrice Lumumba.Huyu ana uhuru wa kutuambia yeye binafsi kaiga nini USSR.
  Huyu ni aina ya wapanga mikakati wakubwa wa CCM na Serikali yake kwa miaka mingi.Wakati CCM ikiwekeza kwenye lugha na rangi ya wakoloni alikuwa wapi?
  Kingunge NGOMBALE Mwiru aidha sasa kachoka mno kimawazo ama vijana wanaotawala hawamjali tena ndiyo maana anabwatuka.
  Huyu hataki kusema kuwa kuna mdudu UFISADI anayetafuna na kudumaza maendeleo kwa sababu hata yeye alionja asali pale Ubungo Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani.Hana jipya!
   
 9. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mjinga anapumua ujinga tu
   
 10. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Sasa si ameshakupa jibu? na yeye si ni mwafrika kwa hiyo anaangukia humo humo!Kwa hiyo swali lako halina mantiki!
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Aliwahi kuwa mshauri wa marais waliomtangulia mbona hakuweza kutoa ushauri ili na sisi tuwe kama hao aliowataja. Hizi ni busara za kujipendekeza ambazo hazisaidii kwa sasa.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ameongea ili iweje........akufurahishe ama vipi?
   
 13. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Labda! mimi sijui, nimenukuu tu alichokisema!
   
 14. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huyo mzee hana lolote! Si alikuwa madarakani mihula yote, alikuwa hayaoni hayo maarifa?
   
 15. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Kwa hili inawezekana Mzee Kingunge yuko sawa. Si unaona baadhi ya dada zetu siku hizi wanavyokimbilia kuzaa na wazungu hata vibabu ili wapate watoto machotara na kuwaweka kwenye blogs kuwa ndio watoto wanaovutia. Hao hao dada zetu wanajichukia kupita kiasi mpaka inafikia kujichubua na kuharibu ngozi zao nzuri za kiafrika kwa kutaka kuwa wazungu..inasikitisha sana. Mzee Kingunge might have a point there.
   
 16. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Umesema kweli hata uwezo wake wa kufikiri umepungua kabisa,maneno haya hakustahili kuyasema yeye kwani ni lipi alilowezesha kufikia maarifa,wakati wake na Nyerere kulikuwa na vyuo vikuu vingapi?.na sasa amezeeka kaachana na siasa vipo vingapi.nani anayejaribu kufikia maarifa.
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  mbona yeye mwenyewe anapenda rangi nyeupe kama wale watu wa maeneo ya ziwa victoria, mwanzo nilifikiri mzee atakuwa mtu wa musoma au mwanza kumbe nanjilinji kilwa
   
 18. b

  bensonlifua92 Member

  #18
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Samahani nimechagua tu kuku-quote wewe ila wengi wamekuwa na mawazo au mtizamo kama wako dhidi ya huyu mzee wetu Kingunge Ngombare Mwiru

  Ni kweli kuwa mzee wetu huyu anahusika kwa sehemu kubwa sana kwa taifa letu hili kuwa hivi lilivyo leo kwa kuzingatia nafasi na heshima aliyokuwa amepewa tangu ujana wake alipojitokeza kuwa mtu maarufu hapa TZ na nadhani hadi nchi majirani zetu....., Nakumbuka jina Kingunge kuna wakati lilimaanisha mtu mzito/kigogo..., Mfano utasikiwa watu wanasema aaah!! jamaa yule bwana ni Kingunge kwelikweli.. au utasikia Kingunge wa Tanzania ni..., au Kingunge wa Kenya ni..., Uganda..., n.k. Hii yote nimeamua tu kuonyesha jinsi mzee wetu alivopata fursa ktk taifa letu. Kwa bahati mbaya kabisa inawezekana kuwa mzee wetu huyu kwa makusudi, au kutotambua hiyo fursa, au kwa kubanwa na mfumo au vinginevyo kabisa mawazo anayoyatoa hapo juu kama aliyatambua akiwa bado yungali na nguvu hayajalisaidia taifa letu kwamba sisi hatukuiga MAARIFA ya wazungu badala yake tumeiga LUGHA yao....kwa mujibu wa mzee Kingunge...

  Pamoja na udhaifu wake huo, mimi naona nimshukuru mzee Kingunge kuwa hajataka kuondoka ktk taifa hili bila kutuachia kipande cha maneno haya ya hekima...kwamba tunatakiwa tuige MAARIFA ya wazungu ili tuendelee... Ni wajibu wetu badala ya kumbeza tuu tuchukue haya maneno yake na tuyafanyie kazi..tuweke strategic plans and action plans on how we can make these words BECOME true and reality ktk nchi yetu. Siyo sahihi sana kumpuuza kabisa mzee wetu huyu, huenda ametambua makosa yake na anaona basi atupe hayo yatusaidie. Hata mwalimu Nyerere alikiri kuwa wakti wake walifanya mazuri na makosa pia..akatushauri tuchukue mazuri tuyaendeleze na makosa yao iwe ni fursa ya kujifunza na kufanya marekebisho twende mbele...Ila akatushangaa pia kuwa tunaacha yale mazuri na tumeamua kuchukua makosa yao....


  Mimi nataka niongezee kidogo ktk hayo maneno ya huyu mzee si kwamba tunaiga lugha ya wazungu na kupenda rangi yao tu..Sisi TUNADHANI ILI TUENDELEE TUNAHITAJI MISAADA YA HAWA WAZUNGU...na mbaya zaidi sisi tunadhani tunahitaji KUPIGA DEBE LA NGUVU KUZUNGUKA HUKU NA KULE ILI KUTAFUTA MISAADA YA WAZUNGU... Cha kushangaza kama mzee Kingunge alivosema HATUHANGAIKI KUTAFUTA HAYO MAARIFA YANAYOWAFANYA WAZUNGU WAWE NA MAENDELEO... aaaaah bali kwetu muhimu ni MISAADA eti tunajivuna na kusema MISAADA YA MASHARTI NAFUU.. Nadhani tunajidanganya wenyewe. Hivi hata ukipewa misaada kama huna MAARIFA itakufaa nini?

  Kingine ambacho mzee hajakisemea ni kuwa SISI AU NISEME BADHI YETU (kwa bahati mbaya sana sasa ndo inaonekan ndo style ya viongozi wetu kuchangamkia uongozi) TUNATAMANI KUWA MATAJIRI BILA KUZALISHA... njia ambayo imechaguliwa ni ya kwa kupitia UFISADI... Hivi kuna msomi hapa anaweza niambia kuwa mtu anapoamua kufisadi fungu lililotengwa kwa project/program fulani hapo kweli anaelewa maana ya jambo analofanya? Hapo kweli mtu huyo ni msomi kweli.... Angalia yanayotokea sasa bungeni hivi hawa wabunge wetu wanajua kweli umaana wa wao kuwa viongozi. Fuatilia utagundua kuwa PESA ya serikali kwa ngazi zote ziko kwenye misukosuko mikubwa ya mbinu nyingi na kabambe watu wazifisadi na wafiche au wajipatie mitaji ya makampuni yao ya kishetani....

  Kuna mamo mengi mzee wetu hakuyasema ila TUUUNGANE NAYE KTK HUO HUO UDHAIFU WAKE TUNAOUONA KUWA TUIGE YALE MAARIFA na siyo hizi harakati na mashindano tunayoyashuhudia ya kufisadi taifa letu kwa kila mbinu kwanza hata huyo FISADI kama anaona mbali hata hiyo pesa anayokwapua haifaidi..ni nyingi mno kwa mahitaji yake hapa TZ... ni lawama za bure na tamaa ya bure tu anajipatia... Pia ni ulofa wa hali ya juu na ndhani wazungu wanatushgaa na kutucheka sana... HIVI INAINGIA AKILINI KWELI TUNAPOKEA MISAADA TOKA KWA WAZUNGU AU TUNAIBA PESA YETU WENYEWE KISHA BAADHI WANAKWENDA FICHA KTK MABENKI YAO WAZUNGU HUKO ULAYA AU SIJUI USA HIVI WANADHANI HIYO PESA INAKAA TU BURE, INAKWENDA FANYA BIASHARAAA...NA HATA HAWA WATU WAKITAKA KUITUMIA NI KTK WOGOWOGA TU SASA RAHA HAPO IKO WAPI YA MTU KUWA NA MAPESA MENGI YA KIFISADI...Kwanini udharilike ukipita njiani watu wanakuona wewe ni FISADI, watoto wako wakitanua jamii inawaona ni za kifisadi... usituringie... na zaidi sana kuna CHUKI KUBWA SANA inajengeka sasa ktk jamii juu ya hao MAFISADI na watoto wao na wajukuu wa MAFISADI na hasa vijana..hapo hiyo si hatari huko mtaani jamani...

  TUIGE MAARIFA na tuwe na MIKAKATI na MIPANGO KAZI na tuache KUTEGEMEA MISAADA haina tija kama hatuna MAARIFA... tuache UFISADI na tusiwe na TAMAA BILA KUZALISHA na tuache UVIVU tupambane na maadui wote wa maendeleo kwa kuchapa MZIGO/KAZI..

  ASANTENI SANA
   
 19. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #19
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huwa sielewi, sijui tumelogwa? mbona hawa watu wakiisha toka kwenye system ndo huwa na mawazo mazuri? Nakumbuka Sumaye naye sikumoja aliwahi kusema, taifa haliwezi kuendela kama hatuuzi vitu nje ya nchi, kama tunanunua zaidi bila uuza then hatutakuwa na fedha za kigeni, aliendelea zaidi kwa kudai tujenge zaidi viwanda ili tupate vitu vya kuuza, ni huyu hyu aliyekuwa waziri mkuu wa muda mrefu kupita yeyote aliyewahi kukalia kiti hicho, swali, kwanini viongozi wengi wa magamba huwa wanaona kikwazo cha matatizo yetu mara baada ya kuachia madaraka?

  Bila kujali historia yake huyo mzee (ambayo kwakweli huwa nasikia kichefu chefu, hasa baadhi ya kauri zake) aliyo yasema ndio ukweli, hivi mwaka 1988 pale kambi ya jeshi kibaha, wanajeshi wale (mainjinia) si waliweza kutengeneza Gari na wakalipa jina la Nyumbu? nakumbuka liliingia hadi kwenye maonesho ya sabasaba, enzi hizo maonesho yale yalikuwa na mvuto sana, hivi kama akina kingunge wangewaendeleza watu wale, leo situngekuwa tunatengeneza ndege? CDM, mkiingia madarakani 2015, endelezeni hili tafadhari!
   
 20. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Walichukua zabuni ya kukusanya ushuru Ubungo terminal
   
Loading...