Inawezekana kweli shule mtu anayosoma na mazingira yake kwa namna fulani yana shape personality za watu!. unajua siyo siri pale ilboru vijana ni hardworking, wanasaidiana na kuheshimiana ile mbaya!. mfano mimi nilipokuwa ilboru pale form five, yaani form six anaheshimika vibaya sana, tena sometimes hata wewe kama ni form five yaani kuingia katika room za form six unakua unajistukia stukia.
halafu kuna ishu ya kuheshimiana, yaani ni vigumu kuona mtu wa kidato cha juu anamyanyasa mtu wa kidato cha chini.
kuna ustaarabu pia katika mambo mengi, mfano kuna kupanga msitari katika kupata chakula, ni aibu kutibua msitari ili uwatangulie waliokutangulia.
wakati wa shida kuna kusaidiana mno, sometimes kuna kukopeshana mkate "slice kwa slice", unanikopa slice mbili ninakulipa slice mbili.
Halafu Ilboru suala la imani ni suala lenye umuhimu wa kipekee, almost kila jioni baada ya kupata "Ng'ande",utawaona vijana haooo taratibu wanajikongoja katika vyumba vyao vya ibada, baada ya lisaa limoja au mawili hivi utawaona vijana hao wanajikongoja kwenda kupiga misuli!
Motto ya Ilboru ni "EDUCATION FOR SERVICE"