Mwaandaji.
SOKA, HJ,
0718478250.
Mahakama kuu ya Gambia imemuhukumu adhabu ya kifo mkuu wa idara ya usalama wa taifa wa zamani wa Gambi pamoja na wakurugenzi wengine wanne wa idara ya usalama wa taifa. Wote watano wamehukimwa kunyongwa hadi kufa kwa kumteka kiongozi wa chama Cha upinzani kwa Siri 2016 kisha kumuua na kumzika kwenye kaburi la Siri lisolo na alama
Mfichua Siri kwa jina X aliimbia mahakama namna wakurugenzi wa idara ya usalama wa taifa walivyomteka kwa Siri na kumtesa na kumuua mwenyekiti wa chama kikuu Cha upinzani Ebrima Solo Sandeng kisha kumzika kwa Siri kwenye kaburi ambalo halina alama. Mahakama ilijiridhisha kwa kufukua maiti na kuipima na kuthibitisha pasipo shaka
Mfichua Siri ambaye naye alikuwa afisa usalama wa taifa ambaye alichukizwa na unyama huo wa mabosi zake kwani mkti wa upinzani hakuwa tishio la usalama wa taifa bali ilikuwa amri ya kiutendaji kutoka kwa Rais wa kipindi hicho Dikteta Yahya Jammeh ambaye aliitoroka nchi na yupo mafichoni baada ya kushindwa uchaguzi 2016
Jaji kumba sillacamara alikataa utetezi wa wakurugenzi hao wa UJASUSI kuwa walitumwa na Rais, kwani jaji alisema idara ya usalama wa taifa Gambia haiko juu ya Sheria.
Pia usalama wa taifa wa Gambia unalindwa na katiba ya Gambia na Sio nje ya hapo, watu wote ni sawa mbele ya sheria
Wakurugenzi wa idara ya usalama wa taifa wanne pamoja na mkurugenzi mkuu idara ya usalama wa taifa walikuwa na wajibu wa kulinda maisha ya watu na Sio kuwaua kisa siasa kinyume na Sheria.
Baada ya hukumu hiyo Jana jumatano 13/7/2022, watuhumiwa walipelekwa gerezani kusubiri kunyongwa hadi kufa.
Mahakama za Africa mashariki zinajifunza nini kuhusu maamuzi haya kuhusu uonevo wa baadhi ya vyombo vya dola kuteka watu na kuwaua?
Jaji wa mahakama kuu Kumba Sillah-Camara, katika hukumu yake amemkuta mkuu wa zamani wa Intelijensia nchini humo, Yankuba Badjie, na makosa ya kumuua Ebrima Solo Sandeng,mwanasiasa wa chama upinzani cha United Democratic Party,mwaka wa 2016.
Wengine waliokutwa na hatia ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa mipango katika kitengo cha Intelijensia wakati huo Sheikh Omar Jeng, Babucarr Sallah, Lamin Darboe na Tamba Mansary.
Sandeng, alipotea siku chache baada ya maandamano dhidi ya utawala wa Jammeh ya Aprili 2016. Alifariki baada ya kuwa kizuizini kwa siku mbili kutokana na majeraha aliopata baada ya kupigwa na kuteswa mikononi mwa vyombo vya usalama.
Haruna Susso, afisa mwengine wa intelijensia na Lamin Sanyang, mhudumu wa afya hawakutwa na hatia katika kesi hiyo.
Kesi hiyo ilioanza mwaka wa 2017 ilikuwa kesi peke ambao ilikuwa ingali inasikilizwa na mahakama ya nchini humo kufuatia tuhuma za visa vya uhalifu wa kibinadamu wakati wa utawala wa Jammeh.
Hukumu hii inakuja wakati huu Jammeh akiwa mafichoni nchini Equatorial Guinea, aliko kimbilia usalama wake mwaka wa 2017 baada ya kupoteza katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2016 dhidi ya Adama Barrow.
Mwaka wa 2017 Barrow alifanya mageuzi katika idara ya usalama wa taifa ambapo ilibadilishwa jina kutoka kwa NIA ambapo sasa inajulikana kama (SIS).
SOURCE:
**Mahakama kuu Gambia
**Voice of America
**Writers