Tujikumbushe hili sakata la CPA seni, limefikia wapi? Mpaka sasa

Tujikumbushe hili sakata la CPA seni, limefikia wapi? Mpaka sasa

Think2

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
3,076
Reaction score
5,975
"Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Director of Finance and Administration) wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), CPA George Mahigu Seni, amesimamishwa kazi kwa kupinga mauaji ya watu wasio na hatia Oktoba 29.

CPA Seni anatuhumiwa kuchapisha maneno ya uchochezi kwenye WhatsApp group ya marafiki zake aliosoma nao SHYCOM. Mmoja kati ya classmates zake alichukua maneno hayo na kuyatuma ofisi ya Waziri Mkuu, na ndipo ikatolewa order ya Seni kukamatwa.

Maneno ya George Mahigu Seni kwenye group hilo ni kama ifuatavyo:

"Siasa ndiyo kila kitu Mtani. Kinacho sababisha yote haya hata kama hatutaki ni ukosefu wa Siasa Bora, Uongozi Bora na Demokrasia thabiti. Je ni sawa mwanamke anayekimbia kupigwa risasi mgongoni? Ni sawa kijana asiyekuwa na chochote mkononi kupigwa risasi? Kwamba ni sawa kufanya mauaji ya halaiki kinyama namna ile?

Je ni sawa kuwatoa vijana ndani wakiangalia mpira na kuwalaza chini na kuwapiga mmoja baada ya mwingine? Siungi mkono watu kuharibu mali za umma na mali binafsi. Siungi mkono hata kufanya fujo tu, lakini kwa picha ambazo zilionekana siku ya tarehe 30 kabla hata zileza CNN si sawa nguvu iliyotumika.

Mtani usilete siasa ktk issue serious. Mnakuwaje na shida ya maji kama mna mto, Rufiji, Ruvuma, Kagera, ziwa Rukwa, Victoria, Tanganyika, Nyasa, Eyas, nk. Mna mvua ya wastani kwa mwaka, baadhi ya maeneo maji yapo chini lakini bado nchi inakosa maji safi? Justify hapo mtan??"

Hoja hizo mbili za CPA Seni za kupinga mauaji ya Oktoba 29 na kukosoa nchi kukosa maji licha ya kuwa na vyanzo vingi, zilitosha kabisa kumuweka matatani. Polisi walimvamia Seni akiwa Arusha kikazi tarehe 15 Desemba 2025 na kumkamata, kisha kumsafirisha hadi Dodoma kwa mahojiano. Alishikiliwa mahabusu kwa siku kadhaa akanyang'anywa simu, computer na kulazimishwa kutoa password zake za social media. Alipigwa sana akilazimishwa amtaje anayemtuma. Hata hivyo alishikilia msimamo wake kuwa hajatumwa na yeyote bali alotoa mawazo yake tu.

Baada ya kuhojiwa aliachiliwa na aliporudi ofisini, aliambiwa na boss wake kwamba amepokea maelekezo kutoka juu kuwa asiende tena kazini hadi hapo atakapopewa maelekezo mengine. CPA Seni alipoomba barua ya kusimamishwa kazi hakupewa barua yoyote rasmi, bali alijibiwa "kihuni" kwamba akihitajika ataitwa.

Hapa ndipo tulipofika kama taifa. Serikali imeua watoto wetu na sasa inafukuza kazi yeyote anayekemea mauaji hayo. Lakini wale waliofanya mauaji ya kinyama wanapandishwa vyeo na kupongezwa."

RAFIKI YAKO NDIE ADII YAKO, MUNGU ATUJALIE MARAFIKI WEMA . AMEEN
 
Back
Top Bottom