Tujihadhari na aina hii ya 'Matapeli'

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Tahadhari tumepewa

Habari zenu mabibi na mabwana. Polen na majukumu.

Napenda niwashirikishe jambo lililonikuta ili kukuokoa Wewe au mwingine.

Kuna wizi wa ajabu wa aina fulani ya madawa ya kupoteza ufahamu.

Jana nikiwa natoka kazini Muda wa jioni nikapita Mlimani City.

Baada ya kufika Mlimani City gafla nilisikia mtu akiniita Jina langu nilipogeuka nilimuona mtu akinichangamkia Sana na kuniuliza Habari za siku, uko wapi ziku hizi?

Nikawa nimepigwa na mshangao maana nikimuangalia simkumbuki kabisa anae nichangamkia.

Mara yule bwana akanisogelea na kuniambia hunikumbuki tulisoma wote?

Kabla sijamjibu mara akatokea mtu mwingine kama wanafahamiana wakachangamkiana kisha yule bwana akaanza kunitabulisha kwa huyu bwana alietukuta pale.

Gafla yule bwana akaniambia kuna mdudu kwenye jicho lako la kulia nilipotaka kutoa akaniambia samahani naomba nikutoe kama hutojali.

Kabla sijamruhusu akachukua kitambaa chake akanipangusa nacho kwenye jicho na puani.

Gafla nikaanza kujisikia vibaya na baada ya hapo sijajielewa tena mpaka nilipojikuta niko Hospital Rabisinia Dar.

Nikaelezwa kuwa nimepelekwa hapo na wasamaria wakiwa wameniokota maeneo ya Vikawe nikiwa sijitambui pembezoni mwa barabara.

Nilikuwa na pesa kama Tshs 320,000/_ walichukua pamoja na ATM card yangu ya CRDB Bank.

Cha ajabu nilipotoka hospitali nikaenda moja kwa moja bank nikawaelezea wakaniambia nikaripoti police.

Kabla hawaja iblock Ile card waliniangalizia balance wakakuta card imetoa pesa ATM mbili Jana na Leo sh milioni 2.

Tulipofatilia kwenye ATM mojawapo ya Jana yake ikakutwa aliezitoa hizo pesa ni mimi mwenye nikiwa na mtu alikuwa ameficha sura yake na kwenye ATM ya pili ikakutwa ni yule mtu aliyeficha sura yake.

So my Dear friend, usimruhusu mtu yeyote usiyemjua kukugusa au kukutoa kitu machoni.

Maana si kukuibia tu bali wanaweza kukulewesha na wakakufanye vitendo vya wakakuingilia vibaya wakakuambukiza hata magonjwa hatari.

Share na magroup mengine tuwaokoe ndugu zetu na mchezo huu mchafu.

Mungu akusaidie kutuma uwezavyo.
 
We umeamini hii story? Amewezaje kukumbuka namba yake ya siri alipotoa kwenye ATM ya kwanza wakati alikuwa hajitambui?
Wabongo noma. Hii habari nimepata kwenye Group la chama chetu.... Vema kuchukua tahadhari na kujifanya "Ujuaji mwingi '" Huyu muungwana ka Share ili watu wengine wawe makini lakini mnaanza kuhoji mara hii habari ya kutunga...
 
Back
Top Bottom