tujifunze matumizi ya "L" na "R" wana JF!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tujifunze matumizi ya "L" na "R" wana JF!!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kigarama, Oct 4, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama hapa ni nyumbani kwa wazamivu waliobobea katika kufikiri (Great thinkers) basi na matumizi ya lugha nayo yazingatiwe. Ingawa dunia nzima inajulikana kwamba lugha za asili huathiri lugha za pili, lakini hiyo hutokea zaidi kwenye utamkaji wa maneno na si kwenye uandishi wake.

  Sisi tujitahidi kuwa mfano wa matumizi bora ya herufi hizi mbili za "L" na "R". Tusiandike "Lafiki" badala ya "Rafiki" au "Jilani" badala ya "Jirani"
   
 2. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja.
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mimi hili jambo linaniudhi kweli kweli...imefikia mahali nikikuta mchangiaji kachanganya hizo herufi, basi post nzima inakosa ladha na huyo mchangiaji namweka kwenye "ignore list", that's how serious I view the whole issue.
   
 4. S

  Skype JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mimi kuna mijitu inanikera sana kwa kutumia neno "udhibitisho" badala ya neno "uthibitisho"
   
 5. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu, wengine mtawaua tu. Hivi kweli umwamvie mkurya atumie 'L' badala ya 'R' utamweza kweli? Au ukimwambia msukuma atumie 'R' badala ya 'L' si ni kumtafuta lawama tu? Hizo herufi hazimo kwenye lugha zao za asili, sasa waje wazipatie huku ukubwani, wataweza kweli? Tutapiga, tuue, mpaka tugalagaze, lakini sidhani Kama tutaweza kuwabadilisha.
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Fungua Chuo Cha kiswahi(r)i..........
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Eh basi na mi najuaga ya kwanza ndo sahihi kweli kiswahili kigumu
   
Loading...