Tujifunze elimu ya Mantiki - Logic?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,693
40,700
Kuna tatizo katika uwezo wa watu wetu kujenga hoja zenye mantiki. Nadhani ipo haja ya kutoa semina ya bure tu juu ya Effective Arguing or something similar kwa sababu wakati mwingine nikiangalia TV n.k nashangaa watu wanaweza kushawishi watu wengine kwa hoja dhaifu zinazotolewa. Natamani LOGIC liwe somo la lazima kwa vyuo vyetu vikuu vyote.


Thats all I'm saying.. maana tunaweza kuingia Bungeni mwaka ni tukachoka!
 
Watu wajifunze pia kuwa WADADADISI na kuwa ba utamaduni wa KUHOJI mambo... Tuache kuchukulia kila kitu kirahisi rahisi tu bora liende!
 
kwa kweli....pia kusoma ni muhimu......tena siku hizi elimu ni "bure"...kama una internet then una elimu.....tumia vitu kama Google na Wikipedia.

Watu wengi ni washabiki tu, wavivu wa kufikiria na kudadisi....

Mi nitakuunga mkono mwanakijiji kwenye kutoa elimu hiyo
 
Kuna tatizo katika uwezo wa watu wetu kujenga hoja zenye mantiki. Nadhani ipo haja ya kutoa semina ya bure tu juu ya Effective Arguing or something similar kwa sababu wakati mwingine nikiangalia TV n.k nashangaa watu wanaweza kushawishi watu wengine kwa hoja dhaifu zinazotolewa. Natamani LOGIC liwe somo la lazima kwa vyuo vyetu vikuu vyote.


Thats all I'm saying.. maana tunaweza kuingia Bungeni mwaka ni tukachoka!

Mkuu nakumbuka enzi zile LOGIC lilikuwa ni somo kwenye hesabu form V, na pia kwenye additional mathematics forn III. Tatizo linakuwa application wengi huwa wanafikiria ni kujibia mtihani tu!
 
ya ndivyo tulivyo wa tz,hupewi know how ya jambo ila unachotakiwa ni kumaliza na kupewa degree,nadhani inatokana na mfumo wetu wa elimu tuliojiwekea tangu enzi hizo

mapinduziiii daimaaaaa
 
Watanzania wengi ukiongelea tu neno logic wanadhani ni maswala ya hisabati.... thats y hata thread yako imekosa wachangiaji wakidhani unataka kumwaga hisabati hapa JF
 
Watanzania wengi ukiongelea tu neno logic wanadhani ni maswala ya hisabati.... thats y hata thread yako imekosa wachangiaji wakidhani unataka kumwaga hisabati hapa JF

Ahaa! Bujibuji bana ina maana hujui kama hisabati ni tatizo sugu ulimwenguni??
 
watu wajifunze pia kuwa wadadadisi na kuwa ba utamaduni wa kuhoji mambo... Tuache kuchukulia kila kitu kirahisi rahisi tu bora liende!

ni kweli mkuu ni aibu unakuta zee zima na upara lake linashindwa kujenga hoja za msingi! Hii bora liende itatufikisha pabaya sana! Utasikia acha amalize miaka yake 5, simple like that! Kwanini usimwonye anapokosea unalidhika na utendaji mbovu! Plz tanzanian saidi nchi yako kwa faida ya kizazi kijacho.
 
Watanzania wengi ukiongelea tu neno logic wanadhani ni maswala ya hisabati.... thats y hata thread yako imekosa wachangiaji wakidhani unataka kumwaga hisabati hapa JF
kivipi uwongo halafu uwongo inakuwa kweli(F then F = T)
:lol:
 
kwa kweli....pia kusoma ni muhimu......tena siku hizi elimu ni "bure"...kama una internet then una elimu.....tumia vitu kama Google na Wikipedia.

Watu wengi ni washabiki tu, wavivu wa kufikiria na kudadisi....

Mi nitakuunga mkono mwanakijiji kwenye kutoa elimu hiyo
Hapo kaka umeongea pointi,:welcome: ktk ulimwengu wa sasa
 
Mkuu umegonga sehemu moja ambayo huwa inanisumbua sana ninapowasiliana na watu mbalimbali kwetu. Mwaka juzi tulikuwa tumegundua fedha fulani za USAID ambazo zingeweza kufanya kazi nzuri sana kwenye chuo fulani huko Tanzania; sheria ya congress inataka pesa zote za USAID zitumike 3rd world. Tulipowasiliana na chuo kile wakatujibu utumbo wa ajabu kweli bila hata kujua kuwa wanaongea na nani; ilikuwa ni aibu sana kwangu niliyeweka contact ile ila kwa bahati kwa bahati nzuri tulikuwa tumweka sample kubwa ya vyuo, hivyo tukawasliliana na chuo kingine kama hicho hicho huko Kenya ambao walitupa ushirikiano wa hali ya juu sana na mwishowe wakachukua zile pesa. Ingawa hazikuwa pesa nyingi sana ($160,000), lakini ilikuwa ni bora kuliko kutopata kitu. Faida yake kwetu sisi ilikuwa ni kuwa bosi wangu aliweza kwenda Kenya free; nilikuwa ninataka aende Tanzania.


Elimu ya mawasaliano ni ndogo sana kwa watu wetu. Watu wengi ni dhaifu sana wa kujenga hoja na kujibizana na wengine. Urithi tulioachiwa na Nyerere katika mawasliano haupo kabisa siku hizi.

Nadhani vyuo karibu vyote vya marekani vinafundisha soma la "Public Speaking" kama mojawapo ya general education courses ambazo ni lazima mwanafunzi alipitie kabla hajapata digrii yake bila kujali fani yake. Course hii pamoja na mambo mengine huwa inasisitiza logic kiasi kuwa matu unapoonegea na watu lazima mawazo yako yawe yamepangiliwa kwa utaratibu fulani ambao unamfanya msikilzaji apende kukusikiliza na kufahamu unaloongea bila kukosea. Course hii ya public speaking inafanana kidogo na course ya zamani iliyokuwa inatolewa pale UDSM ikijulikana kama Communication Skills ambayo ilikuwa ni lazima kila mwanafunzi aipitie bila kujali yuko kitivo gani. Kosa lilitokea baadaye ni kuwa wanafunzi wengi walikuwa wanaingia chuoni huku kiingereza kinawagonga sana na kusababisha waalimu wengi wa CSU wawe wanatumia muda mwingi kufundisha grammar na sentence structures zaidi ya logical flow of ideas.

Tukumbuke kuwa, kuwa na mawazo mazuri bila kujua namna ya kuyapitisha mawazo hayo kwa watu wengine ni sawa na kutokuwa na mawazo kabisa.
 
Logic huku kwetu bado. Logic kwa maana ya mantiki bado, logic kwa maana ya hisabati bado. Tunatatizwa na kutojua kuwa hatujui. Na hatudhani kuwa tunaweza kuwa hatujui. Kuna kundi kubwa sana linalojidhania ni la wasomi kwa kuangalia vyeti tu au vyuo. Kuna mtu anaweza kuwa very proud kusoma chuo fulani (niseme tu kwa muda fulani ilikuwa UDSM) bila kujali ametoka na kitu gani hapo chuo. Kuna watu wanajivuunia kuwa na PhD bila kupima PhD zao zinajitafsiri vipi katika maisha yao na maendeleo ya nchi. Kuna watu wanajivunia kufanya kazi ofisi fulani au kampuni maarufu bila kujali tija inayotokana na kazi zao.

Kuna kundi fulani la wasomi wa uhandisi wanahalalisha kutojua kiingereza au kujieleza kwa kisingizio kuwa wao si wanasiasa lakini ukiangalia uhandisi wao bado ni wa kushika vibendera kwenye tender za wachina. Wanaweza kutisha watu kuwa wamesoma uhandisi lakini ukiwauliza nini application ya Froude Number hawawezi kukwambia pamoja na kwamba ndiyo wanayoitumia kutisha watu....... tuna safari ndefu sana.

Binafsi nina interest na utengenezaji filamu. Huwa naangalia viwango vya wasanii na watengenezaji hapa TZ, viwango ni duni sana na wasanii wanaridhika kwa kuwa wanaandikwa na magazeti ya udaku na watu wanawanyooshea vidole mitaani. Katika mazingira haya ukiwakosoa kwa maana ya kuwafundisha wanaishia kukuuliza, "Kati yangu na wewe nani ni maarufu zaidi?"
 
Hilo ndio tatizo la watz wengi!Kwa mfano mdogo tu.Labda upo Kenya unakutana na mtu alafu ukahasi ni mtz,ukamwuliza wewe ni mtz?Lazima atakujibu tu,we umejuaje?Nyie watz wabishi!Mwogo sisi sio wabishi.Kiukweli hatupo makini katika kujbu hoja bali huwa tunaleta vioja na ushabiki uliopitiliza,kwa lengo la kufurahisha watu.Hii inatokana kuchukulia mambo yote kirahisi rahisi.Majibu mepesi kwa maswali magumu!
 
Back
Top Bottom