Tujiandae kwa hali mbaya ya bei za bidhaa na uhaba wa chakula, Serikali ichukue hatua kuelimisha wananchi

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Uchumi unajengwa na mambo makuu mawili tu uuzaji na ununuaji iwe bidhaa au huduma (Demand and Supply). Mnyororo huu ukiyumba wa uuzaji na ununuaji tegemea maafa makubwa sana kwenye uchumi wa nchi

Hali mbaya ya maisha ilishaonekana hata kabla ya vita na niliandika uzi huu

Madhara ya uchumi huwa yanachukua muda mrefu sana kuonekana kuanzia miezi sita na kuendelea, Ongezeko la bei za mafuta na bidhaa kwa sasa hii ni rasha rasha tu, Vita ikiendelea ya Russia na Ukraine kila kitu kitaongezeka bei kwa asilimia mia moja (100%)

Nchi za ulaya na Marekani ndio watoa misaada mikubwa Africa, Hizi nchi za ulaya na Marekani ndio wanaotusaidia pesa za kigeni kwa utalii na kutupatia mikopo na misaada mbalimbali kama wakati wa korona, Hizi nchi kwa sasa wanapambana na hali zao za maisha kudhibiti mfumuko wa bei.

Tanzania tutapata wapi pesa za kigeni ili kuweza kudhibiti thamani yetu ya shilingi?

Ni watalii gani wana raha ya kuja Afrika wakati gharama zao za kumudu maisha ulaya zinazidi kuongezeka?

Mafuta ya ndege bei zimepanda, Nauli zitaendelea kupanda Katika sekta ya usafirishaji na hii itazifanya bidhaa zetu tutakazo uza nje kuonekana ni ghali sana.

Malengo ya Putin bado hayajulikani na mwisho wa vita hii hakuna anayejua lengo lake kiuchumi, zimebaki Propaganda tu lakini uhalisia na mwisho wa hii vita ni siri kubwa.

Athari za uuzaji na ununuaji bidhaa tayari Tanzania umeshaanza kuonekana kwa kasi ya ajabu sana.

Serikali ijitahidi kutoa ruzuku kwa Makampuni ya uagizaji wa mafuta ili kufidia gharama zao za usafirishaji.

Serikali isipoingilia kati tutegemee maisha màgumu zaidi miezi mitatu ijayo.

Nini cha kufanya kwa Raia binafsi?

Raia tunapaswa kudhibiti sana matumizi yetu na kupunguza sana baadhi ya mambo yasiyo ya msingi

Raia tunapaswa hasa wenye familia kubwa kuanza kupambana kutafuta bidhaa za msingi kwa maisha ya kitanzania kama mchele, unga,Mafuta ya kupika, maharage na Dagaa na kuanza kuyahifadhi.
 
Midomoni wanaendelea kusema wanafungua nchi lakini kimsingi hapa ndani hali ya mwananchi wa kawaida inazidi kuwa mbaya.

Nashindwa kuelewa kama kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kasi ya kufungua nchi na hali ya maisha kuzidi kuwa mbaya, kama uhusiano huo upo basi bora nchi ifungwe tu.

Bidhaa mbalimbali zinazidi kupanda bei sokoni, huku namsikiliza Waziri Mkuu anawaambia wafanyabiashara wasipandishe bei kwasababu ya mfungo, anasahau bosi wake alishatuambia tukae sawa vita ya Ukraine na Urusi haita tuacha salama.

Naona kwa sasa nchi yetu iko kama inaongozwa na serikali mbili tofauti, serikali moja inajaribu kuzuia tatizo, nyingine inakuza tatizo, mpaka pale watanzania tutakapoamka na kusema sasa basi... wacha tuendelee kuteseka.
 
Hii sio serikali ya kuchukua hatua kwa chochote, hii ni serikali ya kutafta wa kumtupia lawama.

Rais ambae anaitwa mfariji mkuu wa nchi anasimama na kusema vitu vyote vitapanda bei na hii ni hali ya Dunia. Kwa maana nyingine anasema msiniulize wala kulalamika kwa chochote sio mimi ninaehusika.

Nchi nyingine hata zilizoendelea wanatoa ruzuku kupunguzia wanachi maumivu yeye anasema ruzuku haisaidii kitu chochote hivyo wananchi tukubali kukabiliana na hali yoyote inayokuja.

Sasa hivi kila kitu huyo mama anawalaumu warusi na Ukraine ndio wamesababisha, iwe mafuta ya magari, mafuta ya mboga, simenti, mabati, vioo vya madirisha, nondo, ushuru wa magari na bidhaa nyingine zote yeye anataka tuwalaumu Ukraine na vita yao.

Hii nchi sijui nani alitulaani.
 
Hii sio serikali ya kuchukua hatua kwa chochote, hii ni serikali ya kutafta wa kumtupia lawama.

Rais ambae anaitwa mfariji mkuu wa nchi anasimama na kusema vitu vyote vitapanda bei na hii ni hali ya Dunia. Kwa maana nyingine anasema msiniulize wala kulalamika kwa chochote sio mimi ninaehusika.

Nchi nyingine hata zilizoendelea wanatoa ruzuku kupunguzia wanachi maumivu yeye anasema ruzuku haisaidii kitu chochote hivyo wananchi tukubali kukabiliana na hali yoyote inayokuja.

Sasa hivi kila kitu huyo mama anawalaumu warusi na Ukraine ndio wamesababisha, iwe mafuta ya magari, mafuta ya mboga, simenti, mabati, vioo vya madirisha, nondo, ushuru wa magari na bidhaa nyingine zote yeye anataka tuwalaumu Ukraine na vita yao.

Hii nchi sijui nani alitulaani.
Vita Ndiyo Majibu Yao
 
Marais wa nchi nyingine wanapambana kushusha makali ya uchumi kudhorora halafu wewe unasema kuwa Tanzania tujiandae kuteseka?!Kajiandae wewe pamoja na mke wako!🐒🐒🐒
7UID.jpeg
IMG_20220404_100611_745.jpg
IMG_20220402_184504_432.jpg
AARD4K.jpeg
 
Kwa bidhaa zinazoagizwa nje tayari nyingi Bei zake zimepanda, zinazofuata ni bidhaa za ndani Hapo ndio tutashuhudia mfumuko wa Bei mkubwa sana. Hadi mwaka huu unaisha Hali itakuwa si njema. Tujiandae kisaikolojia na kiuchumi.

Watu waweke akiba ya kutosha ya bidhaa majumbani mwao na nidhamu ya matumizi maana kiwango kikubwa Cha fedha kitatumika kwenye mahitaji ya msingi ya kila siku kuliko kufanya uwekezaji wowote.
 
Zimbabwe, Venezuela, Iran wana mifumuko mikubwa ya bei kuliko iliyowahi tokea duniani ila wanaishi.
Hata sisi tutazoea

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetoa jibu jepesi kwenye jambo kubwa.Inaonekana wewe nikati ya watu ambao hawana uwezo wakutafuta altenative kwasababu tu jirani nayeye anatatizo kama lako.Huu sio wakati wakujilinganisha na mtu kwasababu kila nchi ina uchumi wake na mazingira yake.
 
Malengo ya Putin bado hayajulikani na mwisho wa vita hii hakuna anayejua lengo lake kiuchumi, zimebaki Propaganda tu lakini uhalisia na mwisho wa hii vita ni siri kubwa
Kuna siri kubwa sana. Ni kama Putin ameamua ku-sacrifice nchi yake kujaribu kuondoa hegemony ya Marekani katika uendeshaji wa uchumi duniani.

Ni kiasi gani atafanikiwa; muda utaongea.
 
Back
Top Bottom