Tujiandae kisaikolojia: Kama itathibitika pasi na shaka kuwa CHADEMA ilitumia ruzuku kinyume na sheria, Msajili atakifuta

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,958
141,951
Ni vema tukalielewa hili mapema wakati uchunguzi kuhusu matumizi ya ruzuku kwa vyama mbalimbali ukiendelea.

Wabunge wa Chadema wameeleza wazi kuwa matumizi ya ruzuku ndani ya chama hicho kwa muda mrefu yamekuwa ya "kienyeji" mno.

Tusisahau kuwa Mh. Komu aliwahi kuwa mtunza hazina wa Chadema na Dr. Mashinji aliwahi kuwa Katibu Mkuu.

Hivyo ikithibitika pasipo shaka kwamba ruzuku imekuwa ikiliwa na wajanja "wawili watatu" basi Msajili wa vyama ataifuta Chadema kutoka Daftari la vyama vya siasa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mbona huko mbali, waifute cdm hata leo. Wananchi walishaamka na haiwataki ccm. Hata zitumike mbinu chafu kiasi gani, lakini tumeshaamka. Ccm ni chama cha kizazi kilichopita, kizazi hiki sio cha ccm tena.
.
FB_IMG_1577352801250.jpg
 
Mbona huko mbali, waifute cdm hata leo. Wananchi walishaamka na haiwataki ccm. Hata zitumike mbinu chafu kiasi gani, lakini tumeshaamka. Ccm ni chama cha kizazi kilichopita, kizazi hiki sio cha ccm tena.
Kwa hiyo unataka kuthibitisha kuwa chadema ni chama cha wapi gaji kwa sasa kizazi hiki cha kina Mbowe kimepiga hela kama hizo ndio sifa za kizazi kipya jomba
 
johnthebaptist,

Tukijua hii itakuwa the last attempt ya CCM na serikali yake kuondoa upinzani halisi baada ya kila effort nyingine zote kukwama.

You can strike off the name CHADEMA from the Registrar of Companies Book, but never from the hearts of a new generation of Tanzanians seeking serious change. CCM is playing with fire!!
 
Mimi nadhani mngekuwa na busara mngehangaika kutatua kero za wananchi ili kuondoa fikra za mabadiliko.Leo mkiiua chadema kesho kitaibuka chama kingine upinzani upo kwenye mioyo ya watu na sio kwenye chama.

Kero za wananchi ni pamoja na kuzuia wizi wa ruzuku ya vyama ambavyo ni mali ya wananchi kwa kuwa vinapata ruzuku yao
Na wanafanya wizi katika pesa hiyo. Vipi bwashee hata picha tu huoni wala kuelewa?
 
Hao wananch wanao ipenda chadema wanakaa dunia Gani
Mbona huko mbali, waifute cdm hata leo. Wananchi walishaamka na haiwataki ccm. Hata zitumike mbinu chafu kiasi gani, lakini tumeshaamka. Ccm ni chama cha kizazi kilichopita, kizazi hiki sio cha ccm tena.
 
Tukijua hii itakuwa the last attempt ya CCM na serikali yake kuondoa upinzani halisi baada ya kila effort nyingine zote kukwama.

You can strike off the name CHADEMA from the Registrar of Companies Book, but never from the hearts of a new generation of Tanzanians seeking serious change. CCM is playing with fire!!
Washabiki wa chadema wataenda kwa Dovutwa au kwa hashim Rungwe
 
Ikithibitika niwezi wakifute tuu hatutaki taasisi za wiziwizi... Chadema inaendeshwa kiujanjaujanja tuu ndomana wasomi hawadumu Bali tuvijana tusela tusela tunaotumika kuchafua watu mfano msigwa dhidi ya kinana ama tumbili na werema!!
 
Kwa hiyo unataka kuthibitisha kuwa chadema ni chama cha wapi gaji kwa sasa kizazi hiki cha kina Mbowe kimepiga hela kama hizo ndio sifa za kizazi kipya jomba

Nasema hivi, msitafute visingizio vya kitoto wakati tunajua fika hamuwezi ushindani wa kisiasa. Mmeona uchaguzi ndio huu, hamna uhakika wa kukubalika kisiasa zaidi ya kushurutisha wananchi. Hivyo mnatumia ile 1.5t mliyopiga kuwapa hao takukuru wakabumbe ushahidi, ili muwatoe wanaokubalika na wananchi, mbaki bila ushindani. Kama mnaona jiwe hana uwezo wa kupambana kwa hoja, muwekani Mbatia au Lipumba wasiwe wamekula hela yenu bure.
 
Lolote linawezekana na wala ctoshangazwa,kama watu wapo tayari upotee kuna kubwa zaid ya hilo?
 
Ingelikuwa kosa la kiongozi wa taasisi fulani adhabu inapewa taasisi, naamini tusingekuwa na taasisi hata moja hadi sasa, ikiwemo CCM. Wahusika wakithibitika kuwa wana hatia wachukuliwe hatua za kisheria. Chama ni taasisi.
 
Back
Top Bottom