Ikithibitika CHADEMA ilihusika na uvunjifu wa amani, then inapaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Iwapo itathibitika pasipo shaka, (proven beyond reasonable doubt), kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika kupanga au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya uvunjifu au kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi toka ndani ya daftari la vyama vya siasa, (scraped from the book of political parties), mara moja na bila huruma yoyote!.

Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifyonyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.

Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia mara kwa mara, ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.

Katika maongezi yetu kuhusu hali ya siasa hali ya siasa nchini, niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana " proved beyond reasonable doubt!" by "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA walihusika kwa kujua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili wa vyama nchini, Jaji John Tendwa, atakuwa hana option nyingine, bali kukifuta rasmi Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini, yaani CHADEMA, toka ndani ya daftari la vyama vilivyosajiliwa, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo sheria ya vyama vya siasa inavyoelekeza kwa mujibu wa katiba ya nchi hii! ambayo yeye ameapa kuilinda.

Kwa kifupi amemaanisha iwapo chama cha siasa kitathibitika kufanya ugaidi, kitafutwa!.

Hata hivyo nikadadisi zaidi, iwapo tuhuma za ugaidi zatathibitika kufanywa na chama tawala CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Baada ya swali hilo, kwanza Msajili alisita kidogo na baadae kusema kuwa kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa ya ugaidi, au uvunjifu wa Amani, hatakifuta right away eti kwa sababu ni chama tawala!, kukifuta chama tawala ni kuvunja serikali iliyopo madarakani!, CCM kikifanya ugaidi, au uvunjifu wa Amani hata kivunja, bali atakipeleka mahakamani ili mahakama ndio itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!.

Hii inamaanisha as of now, Tanzania bado hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali iliyopo madarakani nje ya ballot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni serikali dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata chama hicho kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.

My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio ya double standards za mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kustahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake kwa kuvifuta, watu wakaishia kupiga kelele na kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki, waki vyama vingine, vikifanya makosa yale yale, vikiachwa eti kwa sababu ni chama tawala!.

Pia nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na baadhi ya wachangiaji ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa serikali na viongozi wa taifa hili!. Nilimwambia hiyo ndio maana halisi ya social forums, watu kujiachia watakavyo!.

Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha kwa watu wote wakiwemo viongozi wa kitaifa!.

Najua kuna wenzetu humu, kwao JF ni just their favorite past time na huja humu wakati hawana shughuli au kitu kingine chochote cha kufanya!, nawaomba mtuhurumie sisi ambao kwetu JF ni zaidi ya nyumbani kwetu, jf ni sebuleni kwetu, jf ni chumbani kwetu, jf ni kitandani kwetu, tunashinda JF, tunakula jf, tunalala JF, tunaamka JF, in short kwa sisi wengine wetu, jf ndio kila kitu kwetu, tunaiishi JF, yaani kwetu JF is our life that we are living for!.

Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.
May 14, 2013
NB. Hili ni bandiko la 2013, nimelikutwa limefungwa!, mode ukilifungua, itasaidia sana.
Nimeliibua baada ya kuona kama Chadema wanataka kutafutiwa sababu kwanza kwa kumtafuta MBOWE na kumfanya bangusilo wa kifo cha yule mwanafunzi, ili kuhalalisha udhalimu huu, wanaweza kuwatoa kafara majeruhi fulani, kisha kutumia rungu la sheria kumaliza mambo!.
Kisingizio cha kumhusisha MBOWE ni hoja ya kuandamana bila kibali hivyo kutaka kuigeuzia kibao Chadema ndio imesababisha.

Tunapaswa kufuata sheria, taratibu na kanuni.
Sheria ya maandamano inatoa uhuru wa vyama kuandamana bila kibali, ila sheria hiyo imetungiwa kanuni za kutoa taarifa kwa OCD 48hrs kabla ili akupatie ulinzi. Sasa kama tayari polisi walikuwepo, unatoa taarifa ya nini?.

Taratibu zinaruhusu kufanya maandamamo ya bila kibali kukitokea jambo lolote la dharura, sambamba na mikusanyiko ya bila vibali kukitokea dharura. Mazingira yenyewe ni kama haya niliyoyashuhudia hapa,
Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Kwanza MBOWE na Chadema hawajavunja sheria, ila wamekiuka kanuni kuandamana bila kibali, ila yale hayakuwa maandamano ya kupangwa, imetokea dharura, hawakutendewa haki, hivyo wamekuwa provoked na kulazimika kuandamana, kufuatia kwa nini CCM tuu ndio wapewe barua za utambulisho na wao wanyimwe?. Provocation ni defense before the court of law, mtu akiwa provocked, anaweza kufanya lolote hadi kuua, na kuachiwa, depending on the nature ya hiyo provocation, na bila maandamano yale, barua za utambulisho zisinge toka, zimekuja kutoka saa 5 usiku!.

Kufuatia mazingira hayo, then, hakukuwa tena na muda wa kufuata taratibu kuomba kibali, bali walikuwa na wajibu wa kufanya maandamano ya Amani, bila fujo wala vurugu yoyote!.

Jeshi la polisi nalo lina mandate ya kutuliza fujo, kwa kudhibiti maandamano yasiyo na kibali, ila yalihitaji busara itemize na sio kwa kutumia nguvu kubwa kuliko iliyohitajika, ila swali linabaki, kwa nini watumie risasi za moto?!. Usikute risasi ile haikufyatuliwa na polisi bali imefyatuliwa na watu wasiojulikana, kama wale wa shambulio la Lissu, na ilikuwa imelengwa kumpata mtu fulani!, ikamkosa, na kumpata malaika yule!.

Chadema shukuruni sana Mungu, maana ingempata mlengwa, saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine!.

P.
 
Aanze na kukifuta chama cha mabosi wake cha CCM, ambacho ndicho kilochosababisha kifo cha mwanafunzi ambaye hakuwa na hatia Akwilina, kutokana na Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni, ambaye hadi siku moja kabla ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni alikuwa hajatoa barua za viapo vya mawakala wa Chadema, wakati wiki nzima kabla alishatoa viapo vya CCM!
 
Mimi naona wafute vyote tu, ibaki ccm tu kwani ndivyo wanavyopenda ila kutenda wanaogopa, Kwani kuandamana sio haki kikatiba? Alafu walivyokua wanafiki eti tutagharamia mazishi ya Akwilina, Mara Tulikua tunampatia mkopo, mimi nilidhani walikua wanampa pesa maana mkopo mwisho wake unalipwa, poor this government
 
Mtafuta chama, I mean nembo na bendera lakini hamtokuwa na uwezo wa kufuta watu na kilichomo katika mioyo yao.

Mabasi yamepata ajali wakafuta kampuni, asubuhi gari lipo barabarani lina jina jingine.
Period.
 
mode naomba nirekebishia hii headline isomeke,
Ikithibitika Chadema Ilihusika na Uvunjifu wa Amani, Then Inapaswa Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!.
P.
What if ikibainika Mkurugenzi ndio kasababisha au Polisi itabidi nao Wafutwe? Pasco Hii story haijabalance, badala ya kuwa specific kwa CHADEMA ungeiweka tofauti kidogo! Kwa akili za mtoto mdogo CHADEMA hawawezi kuwa Wajinga kiasi hiki.

Why Wale Mananga WA CCM waongee ujinga vile? Kwa mfano, Polepole Anasema Polisi wamhoji Mbowe Halafu ghafla Mambosasa anajitokeza Anasema tunamtafuta Mbowe... Connect the dots!! Tunafanya Siasa za kijinga saaana! Ila next time huenda Hali ikawa mbaya saaana aiseee! Mungu asaidie
 
Wafute Chadema na Upinzani kwa Ujumla na ikiwezekana Wafunge Mitandao ya Kijamii ili wasikumbane na Ukosoaji aina yoyote Tuone kama Maendeleo waliyoshindwa kuleta Zaidi ya miaka 50 kama watafanikiwa.Niwashauri tu,Wasitumie Kiburi na Jeuri kufanya Mambo ambayo yatasababisha Amani yetu ipotee.Vyeo hivi hawatadumu nazo milele na pia Hata Madikteta nao hufariki.Wamwogope Mungu
 
Najua kuna wenzetu humu, kwao JF ni just their favorite past time na huja humu wakati hawana shughuli au kitu kingine chochote cha kufanya!, nawaomba mtuhurumie sisi ambao kwetu JF ni zaidi ya nyumbani kwetu, jf ni sebuleni kwetu, jf ni chumbani kwetu, jf ni kitandani kwetu, tunashinda JF, tunakula jf, tunalala JF, tunaamka JF, in short kwa sisi wengine wetu, jf ndio kila kitu kwetu, tunaiishi JF, yaani kwetu JF is our life that we are living for!.
Wasalaam.
Pasco
Paskali, Miye binafsi NAIPENDA JF na ni chanzo changu PEKEE cha habari za KITAIFAna za KIMATAIFA. Ninaiheshimu. Ninashukuru kusoma kuwa viongozi wetu wa Ki Taifa husomaga JF. Niwaombe, wenye ID feki na za kweli, WASIWE na Dabo standadi. Wasitoe maamuzi yanayoibua HASIRA, CHUKI na VISASI......
 
Back
Top Bottom