Tujengewe Chuo Kikuu mjini Singida kwa maendeleo ya mji

NJOLO

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
568
600
Mji wa Singida uko katika ya Inchi lakini kitu cha ajabu sana ni kwamba hakuna hata chuo kikuu kimoja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Pombe John Makufuli anapotangaza kuwa anatoa mikopo kwa zaidi ya Wanafunzi 100,000, kwa mwaka ni pesa nyingi sana inalipwa.

Katika pesa hii nyingi hakuna hata senti moja inatumika Singida kwa Wanafunzi kununua nyanya, ndizi, unga, mchele , vifaa vya madukani, stationary nk.

Kuna wakati Mama Salma Kikwete alifadhili wanafunzi 300 wa kike waliodhirika na ukimwi na Wakasababisha sehemu za masoko na mji kwa ujumla kuchangamka.

Baada ya wanafunzi hawa kumaliza chuo katika ngazi ya certificate, mjini ulipoa na hata sasa nyanya zinaoza sokoni kwa kukosa wateja.

Vyoo vikuu vingini vinarundikwa Dar, Dodoma, Iringa, Mbeya nk .

Kiongozi yeyote wa Kisiasa anayetaka kupata kura Singida katika uchaguzi ujao, atangaze nia ya kujenga chuo kikuu chenye wanafunzi zaidi ya 5000, uwanja wa ndege na Hospitali ya Rufaa.

Mji huu uko katikati ya nchi na kwa hiyo ni rahisi kufikika na mtu yeyote.
Haki huleta Amani.

Wengi
 
Sikia labda umekurupuka kuleta mada yako au hukufanya uchunguzi wa kina singida ina hospitali ya rufaa (nina marafiki zangu wanafanya kazi hapa), ina chuo kikuu cha TIA, Chuo kikuu huria ina vyuo vya kati pamoja na utumishi, cha udaktari na unesi pale mkoani , veta, kipo chuo cha madawa pale mjini, chuo cha IT na pia vipo vyuo vya ualimu viwili na uwanja wa ndege upo ila haujaendelezwa.
 
Mji wa Singida uko katika ya Inchi lakini kitu cha ajabu sana ni kwamba hakuna hata chuo kikuu kimoja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Pombe John Makufuli anapotangaza kuwa anatoa mikopo kwa zaidi ya Wanafunzi 100,000, kwa mwaka ni pesa nyingi sana inalipwa.

Katika pesa hii nyingi hakuna hata senti moja inatumika Singida kwa Wanafunzi kununua nyanya, ndizi, unga, mchele , vifaa vya madukani, stationary nk.

Kuna wakati Mama Salma Kikwete alifadhili wanafunzi 300 wa kike waliodhirika na ukimwi na Wakasababisha sehemu za masoko na mji kwa ujumla kuchangamka.

Baada ya wanafunzi hawa kumaliza chuo katika ngazi ya certificate, mjini ulipoa na hata sasa nyanya zinaoza sokoni kwa kukosa wateja.

Vyoo vikuu vingini vinarundikwa Dar, Dodoma, Iringa, Mbeya nk .

Kiongozi yeyote wa Kisiasa anayetaka kupata kura Singida katika uchaguzi ujao, atangaze nia ya kujenga chuo kikuu chenye wanafunzi zaidi ya 5000, uwanja wa ndege na Hospitali ya Rufaa.

Mji huu uko katikati ya nchi na kwa hiyo ni rahisi kufikika na mtu yeyote.
Haki huleta Amani.

Wengi
Mgombea TL anatokea singida.ni kipaumbele chake hicho.
 
Back
Top Bottom