Singida Ilitakiwa Kuwa Mji Mtamu

Singida Ilitakiwa Kuwa Mji Mtamu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,801
Reaction score
60,648
Singida ina potential kubwa sana ambayo bado haijatumika kikamilifu. Imagine katikati kabisa ya mji kuna view ya mabwawa mawili, hali ya hewa ya kawaida, mazingira yenye utulivu na maji yanayoweza ku-refresh akili. Kwa mipango mizuri ya mji, Singida ingeweza kuwa moja ya miji yenye kuvutia zaidi kuishi Tanzania.


Moja ya mawazo muhimu ni eneo la Shule ya Sekondari Mwenge ambalo lipo katikati ya mji na limechukua eneo kubwa sana. Badala ya kuendelea kuwa sekondari tu, serikali ingeangalia uwezekano wa kuligeuza kuwa chuo kikuu kikubwa. Hii ingeongeza population ya vijana, biashara, apartments, cafes, usafiri na mzunguko wa fedha mjini.


Zaidi ya hapo, eneo la hifadhi ya chanzo cha maji chini ya hospitali ya mkoa linaweza kubadilishwa kuwa sehemu nzuri ya mapumziko, walking areas na city attraction bila kuharibu mazingira. Singida ina nafasi ya kuwa mji wa kisasa wenye utulivu, mazingira mazuri na tourism ndogo ya ndani kama ikipewa maono sahihi ya urban planning.
 
Wapo wenye mawazo mazuri hata kuliko yako, na wameeshayaweka mezani tayari ila tatizo unapogundua nchi hii ina changamoto ya kuhujumu mawazo mazuri na ukiyasimamia unatolewa kwenye hiyo nafasi haraka sana. We pata picha. Kwani nchi hii hakuna watu wanaochukia kupokea rushwa maofisini. Mimi naamini wapo wengi. Ila kuwa mkurugezi harafu kataa kupokea rushwa wewe mwenyewe kwa kitengo chako na utende haki. Nakuhakikishia hautakaa mda lazima utatolewa haraka na sababu ni kwa vile hauko sawa na wao
 
Upo sahihi.Serikali imepafanya Singida kama mbuga ya wanyama iliyopo porini tu.Hapo ni aidha upite na ukiiangalia kwa mbali au ukae siku mbili na kurudi mjini.Kila mji haukosi potentialities lakini viongozi wenye maono wako wapi!?
rafiki viogozi wapo tena wengi sana tatizo ni mfumo wa utekelezaji. Mfano fatilia mchoro ya miradi mikubwa ya serikali halafu fatilia tena baada ya mradi, ramani na ubora kama vinaendana.
 
Upo sahihi.Serikali imepafanya Singida kama mbuga ya wanyama iliyopo porini tu.Hapo ni aidha upite na ukiiangalia kwa mbali au ukae siku mbili na kurudi mjini.Kila mji haukosi potentialities lakini viongozi wenye maono wako wapi!?
imagine soko la kimataifa la vitunguu wanataka kujenga kititimo huko wakati mwenge pale pako vzr sana yaani wanatanua mji ambao bado haujajaa..pale mwenge badala ya shule ilitakiwa iwe kitovu cha mji,,soko kuu hata bhalmshauri japo imejengewa karakana sio mbali na mji ila ilipaswa iwe mwenge ..hata stand mpya bado ingejengewa mwenge pale ingekuwa poa sana..hio shule ya advance ingehamishiwa hata mungumaji huko
 
Upo sahihi.Serikali imepafanya Singida kama mbuga ya wanyama iliyopo porini tu.Hapo ni aidha upite na ukiiangalia kwa mbali au ukae siku mbili na kurudi mjini.Kila mji haukosi potentialities lakini viongozi wenye maono wako wapi!?
na pale pana hela ukiona wachaga hawaondoki kwenye mji ambao sio wao jua kuna pesa..kwanini wachaga huwakuti manyara,lindi au kigoma ni kwa sababu washaona hakuna mzunguko
 
Ni mji wa kuvutia na kuonekana wote katika angle moja ukipiga picha pande zote za dunia unauona mji wote. Katikati ya mji panaboreshwa kwa kujengwa majengo mapya ya kisasa.
 
Ni mji wa kuvutia na kuonekana wote katika angle moja ukipiga picha pande zote za dunia unauona mji wote. Katikati ya mji panaboreshwa kwa kujengwa majengo mapya ya kisasa.
ni kamji fulani kazuri sana na hata ukituliza akili unatajirika kwa sababu vijiji vingi vinategemea kufunga mzigo mjini so pale town ndo maana kina mangi hawataki kuondoka wanyaturu tumebaki tunashangaa shangaa
 
Kuna watu kwa mionekano au uhalisia ukatambua kabisa wana ukwasi lakini hawaziweki kwenye mizunguko zifike kwa wengine na kuzalisha zaidi.Wanazo keki na wanatamani kuzila na hapohapo wanataka zibaki wazitazame zikiwa nzima.
Labda kama wewe ni mwenyeji wa singida na unavutia kwenu , lakini Singida kuizidi manyara labda kwenye idadi ya punda tu
 
Kama kuna hela , huo mzunguko ni kitu gani?
unajua nini kinafanya singida pawe na mzunguko mkubwa tarafa nyingi za sindiga DC zinategemea kufanya manunuzi ya jumla singida mjini na wao pia wana jitosheleza kwa vyakula kuleta singida mjini tofauti na manyara miji yako iko mbali na babati mingine inakwenda karibu na mkoa wa arusha
 
Back
Top Bottom