Tujenge Utamaduni wa Kuwajibika na Kutenda Haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujenge Utamaduni wa Kuwajibika na Kutenda Haki

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Sooth, Apr 19, 2011.

 1. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Mnapokuwa kwenye mtumbwi na mmoja wenu akawa anatoboa mtumbwi, mkimwacha aendelee, wote mtazama majini. Mliokuwa mnaangalia na aliyekuwa anatoboa.

  Uwajibikaji mahali pa kazi ni duni hasa ktk taasisi za serikali. Kuna sababu nyingi kama kipato kisichokidhi mahitaji, kukosekana kwa vitendea kazi, n.k. Lakini pia kuna uvivu na tamaa tu. Fikiria askari wa barabarani anayechukua rushwa kutoka kwa konda au nesi anaechukua hongo kwa mgonjwa, je konda na mgonjwa ndo wana hela zaidi yao? Ni tamaa tu. Wasiowajibika na kutenda haki mahali pa kazi wanatoboa Jahazi ambalo hata wao wamepanda.

  Loliondo kwa babu wameenda mawaziri na majaji na watu wengine wa kada mbalimbali za juu. Hawa ni watu ambao kwa nafasi zao wangeweza kufanya mabadiliko makubwa ktk maisha yetu watanzania, ila kwasababu ya uvivu, ushabiki wa itikadi na ubinafsi, tupo hapa tulipo. Sisi na wao, wote tunaelekea Loliondo, ktk kuthibitisha jinsi mfumo wetu wa afya (unaosimamiwa na serikali) ulivyoshindwa. Kwa kidogo tunachopata, tunaweza kubadili maisha yetu na ya vizazi vijavyo kama tukiwajibika na kutenda haki mahali petu pa kazi.
   
Loading...