Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Hivi karibuni tumemsikia waziri Nape akieleza kuwa wale wote waliosema uwongo dhidi ya afya ya makamu wa Rais, atawachukulia hatua.
Mimi ni mtu ninayechukia sana uwongo, na hakika waongo wanastahili kuchukuliwa hatua.
LAKINI
Ili kutenda haki, na ili tuonekane tunachukia uwongo, tuanze kwanza kuchukua hatua dhidi ya viongozi waongo. Halafu ndiyo tushuke chini.
1) Waziri Nape, chukua hatua kwanza dhidi ya Mbarawa aliyeweza kuwadanganta wananchi na Bunge kuhususiana na IGA.
2) Waziri Nape chukua hatua dhidi ya Majaliwa aliyesema kuwa JPM alikuwa ofisini akichapa kazi wakati alikuwa kwenye hatua zake za mwisho za kupigania uhai wake.
3) Waziri Nape, chukua hatua dhidi ya Chalamila aliyesema kuwa JPM alimpigia simu, na akamwabia awasalimie wananchi wa Mbeya, wakati tayari JPM alikuwa marehemu.
4) Waziri Nape, chukua hatua dhidi ya January Makamba aliyesema baada ya matengenezo ya mitambo ya TANESCO, mgao wa umeme utakuwa historia.
Ukishamaliza kuchukua hatua dhidi ya hawa, tuje na hawa walioeneza kuwa Makamu wa Rais alikuwa mgonjwa mahtuti. Lakini hiyo itakuwa baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa ni kweli hakuwa hospitalini.
Baada ya hapo, Waziri Nape, weka utaratibu utakaowawezesha wananchi kutoa taarifa juu ya viongozi waongo, ili kila kiongozi atakayesema uwongo, achukuliwe hatua mara moja. Maana serikali imejaa viongozi waongo ambao wameugeuza uwongo kuwa sehemu ya sifa za kiongozi.
Usipofanya hayo, wewe ni mnafiki tu, huna chembe ya kuuchukia uwongo.