Tujadili: Pre-ndoa... Plan B aka 'BIMA'

Tujadili: Pre-ndoa... Plan B aka 'BIMA'

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,501
Nakumbuka sana mafundisho ya dini nikiwa secondary kuhusu Urafiki, Uchumba na Ndoa; tuliambiwa (na kweli ina make sense) kuwa ni vizuri kuwa na marafiki wengi, lakini mchumba ni mmoja na kipindi cha uchumba maana yake unakuwa umefungwa (huwezi kuruhusu mchumba mwingine in case umemkubali wa kwanza); hiki ni kipindi cha kuchunguzana tabia kabla ya kujifunga moja kwa moja kwenye ndoa.

Lakini kwa sasa idadi kubwa ya watu (hasa wadada) walioko kwenye uchumba wana kuwa na bima au plan B au mpango wa kando. Hali hii ikija kugundulika mara nyingi hupelekea muhusika kukosa yote hata kama alikuwa anapenda kuolewa.

Sasa wana jamvi naomba tujadili kuhusu:-
  • ulazima au umuhimu wa plan B
  • Kiini cha tatizo hasa ni nini?
  • Nini kifanyike ili hii hali isiendelee?

cc lara 1, amu, Paloma, Nicas Mtei, Eiyer, Evelyn Salt na walioko kwenye ndoa watuambie waliolewa/oa na plan A au B gfsonwin, @fp, snowhite, Dark City, Mtambuzi, Wiyelele Kaizer hata wale walio kwenye complicated situation kama The Boss, KIKUNGU SnowBall Kongosho et el karibuni.
 
Last edited by a moderator:
Usijiondoe mwaya, sijajua status yako ndio maana nimeshindwa kukuweka sehemu yoyote ili nisikuvunjie heshima. pls changia bwana.
Bahati mbaya kuna mambo mengine hayahitaji kuwa na 'plan B'
Mfano katika hili la mahusiano, ukiwa na plan B tuu jina litakalo kufaa bila kupepesa macho ni MALAYA.
Ni kama muumini wa dini flani eti awe na kadini kengine pembeni just incase! Mmh!! Hapana.
The only plan B katika hilo ni kujiondoa kama huyo unayemtegemea hakufai, au ameku'disapoint unakuwa singo kwa muda then ndio upate mwengine.
 
Unajua concept ya ndoa nayo katika dunia ya utandawazi hii imekuwa ngumu sana kuijadili.

Kwanza waliowafundisha mafunzo hayo ya uchumba ni watawa au watu wenye ndoa zao?? Nataka kupima uzoefu wao wa hali halisi. Mtu anayekufundisha theory ya kuogelea wakati si mwogeleaji ni ngumu sana kujua changamoto za swimming pool, bahari, mto na ziwani. Mengine ana-assume tu kumbe ndivyo sivyo. Hakuna kitu kilichokuwa naona muujiza kama 'alteration in rocks' lakini kiuhalisia ize tu, anyway. Changamoto ya kwanza.

Pili, kuwa na marafiki wengi, afu mchumba mmoja, makusudio yake yalikuwa mchumba mkishindwana unateua rafiki mwingine kuwa mchumba?? Kama ndio, nafasi ya upendo iko wapi? Je, wana-assume kuwa upendo ni equally distributed kati ya marafiki au wachumba tofauti??? Changamoto ya pili.

Lakini pia, ishu ya kuwa na plan B katika dunia ya leo ambayo asilimia kubwa ni kuvuana kyupiz kabla ya ndoa inakuwaje? Nafasi ya uaminifu? Kama wakati wa uchumba tu ambapo bado unamhemuko wa mwenza wako, hamu haikuishi una Plan B, je mkiingia kwenye ndoa? Pale ambapo umeshajua mapungufu yake anakoroma usiku, akila anarusha chakula, labda ni insecure. he is no longer exciting, utakuwa mwaminifu?? Je wakati anashambuliwa na magonjwa kama kisukari, utakuwa mwaminifu?? Je ambapo hana uzazi, utakuwa mwaminifu??
Je wapenzi mtakuwa mnaaminiana wakati mnajua kila mmoja alikuwa na plan B wakati wa uchumba?? Changamoto ya tatu.

Lakini pia, unapokuwa na Plan B, wakati Plan A iko active, una uhakika kiasi gani Plan B itakuoa pale A mambo yanapokwenda mrama? Je Plan B nayo ikiingia mitini? Kutakuwa na haja ya kuwa na Plan C and D labda??

Aisee, ndoa na mapenzi hayana mahakama wala insurance kwa mtizamo wangu. Noana hapa Plan B inataka kutumika kama insurance hivi.
 
kwani hapo ume cc kutokana na status? yangu umeijuaje?

Back to topic: Kwa kweli mpango wa kando mara nyingi unatokana na wengi walio kwenye mahusiano kutokuwa na uaminifu, si vyema kuwa na mtu mwingine pembeni wakati unaye ambaye umeji commit kwake
 
unajua concept ya ndoa nayo katika dunia ya utandawazi hii imekuwa ngumu sana kuijadili.

Kwanza waliowafundisha mafunzo hayo ya uchumba ni watawa au watu wenye ndoa zao?? Nataka kupima uzoefu wao wa hali halisi. Mtu anayekufundisha theory ya kuogelea wakati si mwogeleaji ni ngumu sana kujua changamoto za swimming pool, bahari, mto na ziwani. Mengine ana-assume tu kumbe ndivyo sivyo. Hakuna kitu kilichokuwa naona muujiza kama 'alteration in rocks' lakini kiuhalisia ize tu, anyway. Changamoto ya kwanza.

Pili, kuwa na marafiki wengi, afu mchumba mmoja, makusudio yake yalikuwa mchumba mkishindwana unateua rafiki mwingine kuwa mchumba?? Kama ndio, nafasi ya upendo iko wapi? Je, wana-assume kuwa upendo ni equally distributed kati ya marafiki au wachumba tofauti??? Changamoto ya pili.

Lakini pia, ishu ya kuwa na plan b katika dunia ya leo ambayo asilimia kubwa ni kuvuana kyupiz kabla ya ndoa inakuwaje? Nafasi ya uaminifu? Kama wakati wa uchumba tu ambapo bado unamhemuko wa mwenza wako, hamu haikuishi una plan b, je mkiingia kwenye ndoa? Pale ambapo umeshajua mapungufu yake anakoroma usiku, akila anarusha chakula, labda ni insecure. He is no longer exciting, utakuwa mwaminifu?? Je wakati anashambuliwa na magonjwa kama kisukari, utakuwa mwaminifu?? Je ambapo hana uzazi, utakuwa mwaminifu??
Je wapenzi mtakuwa mnaaminiana wakati mnajua kila mmoja alikuwa na plan b wakati wa uchumba?? Changamoto ya tatu.

Lakini pia, unapokuwa na plan b, wakati plan a iko active, una uhakika kiasi gani plan b itakuoa pale a mambo yanapokwenda mrama? Je plan b nayo ikiingia mitini? Kutakuwa na haja ya kuwa na plan c and d labda??

Aisee, ndoa na mapenzi hayana mahakama wala insurance kwa mtizamo wangu. Noana hapa plan b inataka kutumika kama insurance hivi.
mapenzi ya siku hizi asilimia kubwa ni kuvaliana vyupi ..sasa utavaa za wangapi? Yaani ugegedwe kote kote kisa ndoa? Bora niikose ndoa mi i can accomodate one person only yooo! Mapenzi ni kujidedicate na kujicommit jamani! Huwezi penda watu wawili maotkeo yake utashindwa kuperform vizuri na utakosa kote
najipenda kuliko ndoa yenyewe mae!
 
Kaunga may be hapa niseme ukweli kuhusu mimi.

mume wangu alikua rafiki yangu wa kawaida sana, yaani alikuwa ni good friend kwangu hope Mentor unajua vyem this histry. mchumba niliyekuwa naye ambaye alikuwa ni mhaya siku aliponiboa tu nilikwenda kwake kumlalamikia, na nilipochoka but sjui nini kilitokea yeye akaingia kuwa mchumba.

as for me hii kwangu nilisema the mhaya wasn't my choice, manake kama ingekuwa hivyo basi ingework out ila so long as haikufanikiwa basi haikupangwa.

Mhaya is still our good friend na ndio loya wa familia. thanks God kwa wakai tuko friends hakuwah kunigegeda nafkir ndio maana ameweza kuwa rafiki wa familia.
 
Last edited by a moderator:
Unajua concept ya ndoa nayo katika dunia ya utandawazi hii imekuwa ngumu sana kuijadili.

Kwanza waliowafundisha mafunzo hayo ya uchumba ni watawa au watu wenye ndoa zao?? Nataka kupima uzoefu wao wa hali halisi. Mtu anayekufundisha theory ya kuogelea wakati si mwogeleaji ni ngumu sana kujua changamoto za swimming pool, bahari, mto na ziwani. Mengine ana-assume tu kumbe ndivyo sivyo. Hakuna kitu kilichokuwa naona muujiza kama 'alteration in rocks' lakini kiuhalisia ize tu, anyway. Changamoto ya kwanza.

Pili, kuwa na marafiki wengi, afu mchumba mmoja, makusudio yake yalikuwa mchumba mkishindwana unateua rafiki mwingine kuwa mchumba?? Kama ndio, nafasi ya upendo iko wapi? Je, wana-assume kuwa upendo ni equally distributed kati ya marafiki au wachumba tofauti??? Changamoto ya pili.

Lakini pia, ishu ya kuwa na plan B katika dunia ya leo ambayo asilimia kubwa ni kuvuana kyupiz kabla ya ndoa inakuwaje? Nafasi ya uaminifu? Kama wakati wa uchumba tu ambapo bado unamhemuko wa mwenza wako, hamu haikuishi una Plan B, je mkiingia kwenye ndoa? Pale ambapo umeshajua mapungufu yake anakoroma usiku, akila anarusha chakula, labda ni insecure. he is no longer exciting, utakuwa mwaminifu?? Je wakati anashambuliwa na magonjwa kama kisukari, utakuwa mwaminifu?? Je ambapo hana uzazi, utakuwa mwaminifu??
Je wapenzi mtakuwa mnaaminiana wakati mnajua kila mmoja alikuwa na plan B wakati wa uchumba?? Changamoto ya tatu.

Lakini pia, unapokuwa na Plan B, wakati Plan A iko active, una uhakika kiasi gani Plan B itakuoa pale A mambo yanapokwenda mrama? Je Plan B nayo ikiingia mitini? Kutakuwa na haja ya kuwa na Plan C and D labda??

Aisee, ndoa na mapenzi hayana mahakama wala insurance kwa mtizamo wangu. Noana hapa Plan B inataka kutumika kama insurance hivi.

hakyamama Kaunga ngoja kwanza nimsifu zombie bana!
unajua ametubadilishia sana huyu kiumbe !
 
Last edited by a moderator:
PLAN B??????
lol!naomba nifanye declaration!mi niliolewa na plan A
iiiila sasa!
kwa maisha haya ya wadogo zetu yanavoendelea haya!
nahisi kama uhalali wa plan b umeshakuwa ndo mpango mzima!
binti kaleta home mchumba january mchumba kamwacha march dada zake twaitwakwenye kikao cha kwanza!
kijana kapeleka posa june august kaachwa oct anatangaza ndoa!
basi mradi ndo imeshakuwa!
napata hofu kuwa hizo ndoa fwata hizo kama kweli ni uchumba au urafiki mpya!SIDHANI!
 
mmmh! Kaunga unaongelea vibuzi?? ila kama ni kuwa na mtu ambaye atakuwa ni substitute ya uliye naye akikumwaga especially kwenye urafiki ama uchumba ni ok with me.

ila kwenye ndoa ndio siyo. na huwez ukamwambia mtu kwamba wewe ni mchumba mbadala hapana wala ni mchumba but mume wangu atakuwa fulan no. hapa unakuwa na mchumba ambaye baada ya kwenda home kujitambulisha basi hawa waliokuwa kwenye reserve list unawaondoa.

kama mchumba hajaenda home basi unaweza ukawa na substitute ambayo utakuwa unapima viwangoo vyao, ili kama mchezaji kiungo hakidhi viwango basi sabu huwa wanachukua namba mbona na yeye huweza kumwondoa mchezaji kiungo kabisa.

ikumbukwe kwamba hapa sisemi ni mafiga matatu ama ni mahawara la hasha nasemea kuwa na mtu ambaye unajua huyu asipoelekea basi huyu anaweza kucover nafasi yake na aka make good hubby.
 
Last edited by a moderator:
Kaunga may be hapa niseme ukweli kuhusu mimi.

mume wangu alikua rafiki yangu wa kawaida sana, yaani alikuwa ni good friend kwangu hope Mentor unajua vyem this histry. mchumba niliyekuwa naye ambaye alikuwa ni mhaya siku aliponiboa tu nilikwenda kwake kumlalamikia, na nilipochoka but sjui nini kilitokea yeye akaingia kuwa mchumba.

.
Mh! Unaweza uka'explain uhusiano wa hapo kwenye red na kuachana kwenu please?
 
Bahati mbaya kuna mambo mengine hayahitaji kuwa na 'plan B'
Mfano katika hili la mahusiano, ukiwa na plan B tuu jina litakalo kufaa bila kupepesa macho ni MALAYA.
Ni kama muumini wa dini flani eti awe na kadini kengine pembeni just incase! Mmh!! Hapana.
The only plan B katika hilo ni kujiondoa kama huyo unayemtegemea hakufai, au ameku'disapoint unakuwa singo kwa muda then ndio upate mwengine.

labda tujiulize kwanini watu wanakuwa na plan B, ni situation inawalazimu au ni tabia tu?
 
Back
Top Bottom