Tujadili ni wimbo gani uhimizao utaifa, uzalendo na utanzania

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
909
1,000
Nimemsikia msemaji wa Ikulu bwana msigwa akiwaomba wasanii aliowabatiza jina la Tanzania All Stars waimbe nyimbo ya kuhimiza uzalendo wakati wa shughuli ya kukabidhi taarifa ya tume ya pili inayochunguza usafirishaji makinikia.

Kwangu mimi hawa wasanii wameimba wimbo wa kawaida tu. Kwa wale tulioishi miaka mingi kidogo ebu tu ukumbuke wimbo unaoitwa "TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WANGU WOTE" Ukiusikiliza wimbo huu hata awe Mzee wa vijisenti angesikiliza nyimbo hii sidhani kama angesaini mkataba wa kifisadi na barrick au richmond au IPTL.

Kwa nionavyo mimi huu ndo wimbo wa kizalendo, kitaifa, na wakuleta umoja miongoni mwa watanzania. Na ingelibidi huu uwe wimbo wa Taifa kuliko huu tulionao sasa ambao tumeuiga kutoka afrika ya kusini ambao hauna viashiria vya kizalendo kulinganisha na Tanzania nakupenda kwa moyo wangu wote"

Mwisho kabisa naomba anaeweza ku upload wimbo huu wa Tanzania nakupenda kwa moyo wangu wote atuwekee ili Wadau mbalimbali wausikilize.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,074
2,000
Ngoja niusubirie hiyo audio kama ipo...hiyo waliyoimba sijaielewa sana hata mimi
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,216
2,000
KAMA TULISHINDWA KUJENGA MISINGI YA UZALENDO TOKA MWANZO,LEO HII TUTEGEMEE NYIMBO KUTUJENGEA UZALENDO!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom