Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Lakini pia mkuu ukitoka kazini 9:30 kwa mazingira ya DSM nyumbani ukiwahi basi ni saa 11 jioni hapo ubebe matunda ukapange road hiyo ni saa 1 usiku.
Dar kwa sasa masaa ya njian yamepungua kwa sana sehemu ya kupoteza sana maybe iwe within 1.30

Il ile ha mqsaa matatu hapana. Kwanza hata hiyo ndefu gongo la mboto tu wanawah saiv
 
Dar kwa sasa masaa ya njian yamepungua kwa sana sehemu ya kupoteza sana maybe iwe within 1.30

Il ile ha mqsaa matatu hapana. Kwanza hata hiyo ndefu gongo la mboto tu wanawah saiv
Ni rahisi sana kuandika mkuu lakini ukiingia kwenye utendaji sio kama unavyodhani
 
Yaani tujadili D kwa sababu gani kwani hicho ndicho kima cha chini? Hujui kuna watuwana C na wanaishi jijini?
Kima cha juu cha mshahara kwa elimu ya juu yaani degree maana serikalini masters haina mshahara wala huajiriwi kwa masters labda vyuo vikuu.
 
Njoo katav uone vijana wadogo kabisa wanavyofa ya maajabu

Unakuta mwl wa kawaida tu mshahara wa chini ya 540 yako Ila amejenga na anapangisha na

Watumishi wengi wamepanga nyumba za Walimu
Katavi huko ndio mtu anapanga nyumba nzima kwa 45,000/=
Nyumba haina thamani huko, huyo mwalimu aje ajenge kwa wanaume huku sinza nadhani hata pension yake haiwezi tosha kiwanja
 
Kima cha juu cha mshahara kwa elimu ya juu yaani degree maana serikalini masters haina mshahara wala huajiriwi kwa masters labda vyuo vikuu.
Nan kakudanganya kwenye vyuo vikuuu vya umma hawa payment structure ya watu wa masters?
 
TGS D ni kiwango cha mshahara kwa mtumishi mwenye shahada ya kwanza anaefanya kazi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa (halmashauri). Baada ya makato ya PAYE, NHIF na TUCTA kiasi kinachobaki ni around Tshs. 540,000/-. Hapo sijaweka makato ya HESLB.

Sasa hapa tuijadili hii 540,000 inayobaki. Je, inaweza kuendesha familia kwa watumishi walio mjini DSM, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya?

Kwa jinsi gani kiasi hiki kinaweza tosha:
1. Kulipa kodi ya nyumba
2. Chakula cha familia mwezi mzima
3. Nauli ya mtumishi kwenda na kurudi kazini hasa DSM
4. Mavazi ya familia
5. Chakula cha mtumishi akiwa kazini
6. Elimu ni bure ila kuna nauli na hela ya kula mtoto kila siku
7. Bili ya maji, umeme na king'amuzi

Leteni uzoefu hapa mnawezaje kumudu haya yote?

Karibu kwa mchango wako
Huyo jamaa anaye pokea around 500K kama miujiza vile kila mwezi anaonga 50k sasa sijui anawezaje survive..?
 
Katavi huko ndio mtu anapanga nyumba nzima kwa 45,000/=
Nyumba haina thamani huko, huyo mwalimu aje ajenge kwa wanaume huku sinza nadhani hata pension yake haiwezi tosha kiwanja
Katavi hata kujenga ni gharama nafuu sana ,hata vyumba vikiwa hata chini ya hapo ni sawa mm niliwahi hata kupewa nyumba nikae bure bila hata sent 0
 
Nilisoma sheria ajira zikawa ngumu ilinibidi nijichanganye na postgraduate ya ualimu, then niliajiriwa as mwalimu 2015 , cha kwanza nilipanga karibu na kituo cha kazi tena single room nikajiapiza sitaoa na kipato hicho, no TV, gas ndogo , nilikuwa napika , then nikawa nimeunda kikundi cha kuchangiana kila mwezi laki mbili, nilikuwa wa mwisho nilipata million moja, then nikakopa million moja na nusu bank, nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa chumba sebule hapo nilijenga mwaka , nilihamia humo kama ndege , then mwaka wa tatu nilianza kununua ngombe dume nawatumia watu home wanafuga, mwaka wa tano nilikuwa na madume kama watano nilipowauza nilifungua duka na kisha nikakopa milioni 1010000 then nilianza kununua mitamba na kuwapa watu kule home, Leo hii umri wangu 35 Naoa mwaka huu, Nina mashamba kwetu makubwa as mkulima mkubwa, nimejenga nyumba standard tu mjini, namiliki canter na Nina mifugo mjini ,Nina duka kubwa tu ,nasomesha watoto wangu 1 na wajomba 2 ila salary yangu ni 249000,_so pambana tu mzee utafika huo mtaji ni mkubwa
bora wewe una ndugu si wengine tuna vidonda ndugu
 
Katavi huko ndio mtu anapanga nyumba nzima kwa 45,000/=
Nyumba haina thamani huko, huyo mwalimu aje ajenge kwa wanaume huku sinza nadhani hata pension yake haiwezi tosha kiwanja
Acha dharau kijana nyumba Mzima 45,000/- hakuna

Nipo huku
Na pia tumajenga kwa gharama sana

Mfano tu cement sisi 22,000/-

Sio baada ya mfumuko wa bei Toka nchi ipate Uhuru

Wewe dar 12,000/-
Tu bei ambayo nikipata hapa najenga matusi kabisa nondo 28,000/-

Tuheshimu buana
 
Hapo hapo ofsini kwenu Kuna mlinzi wenu analipwa take home

270,000, amejenga, ana mke na anasomesha watoto watano.

My take: Hakuna mshahara mkubwa Wala mdogo, Ni suala la vipaumbele vya matumizi litakalowatofautisha mfanyakazi uyu na Yule kimaendeleo
yani
A. alipwe 4M na B. alipwe 600k alafu useme hakuna mishahara mikubwa wala midogo 😁😁😁
 
TGS D ni kiwango cha mshahara kwa mtumishi mwenye shahada ya kwanza anaefanya kazi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa (halmashauri). Baada ya makato ya PAYE, NHIF na TUCTA kiasi kinachobaki ni around Tshs. 540,000/-. Hapo sijaweka makato ya HESLB.

Sasa hapa tuijadili hii 540,000 inayobaki. Je, inaweza kuendesha familia kwa watumishi walio mjini DSM, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya?

Kwa jinsi gani kiasi hiki kinaweza tosha:
1. Kulipa kodi ya nyumba
2. Chakula cha familia mwezi mzima
3. Nauli ya mtumishi kwenda na kurudi kazini hasa DSM
4. Mavazi ya familia
5. Chakula cha mtumishi akiwa kazini
6. Elimu ni bure ila kuna nauli na hela ya kula mtoto kila siku
7. Bili ya maji, umeme na king'amuzi

Leteni uzoefu hapa mnawezaje kumudu haya yote?

Karibu kwa mchango wako
Akili hufanya kazi kulingana na changamoto uliyonayo ama vile ambavyo unataka ifanye! Mshahara ni sehemu tu ya namna ambavyo mtu anaweza kuendesha maisha yake, sio njia pekee! Kuna mmama alikuwa ananiuzia mboga mboga, ila amejenga na anasomesha mwanae Sekondari! Kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom