Kuna watumishi wa Serikali wasio na viwango kabisa

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,765
Kuna changamoto kwenye sekta hii ya utumishi wa umma. Kubwa sana ni kukosa viwango (standards) na muendelezo (continuity). Hii continuity watu wa filamu wanaijua sana, la sivyo kazi zao zingekuwa vioja. Sasa vioja hivyo wanafanya hawa watumishi wa serikali.

Tukianza na standards nikiangazia idara mbili za umma (NHIF & RITA) Tunategemea pale ambapo mtafuta huduma anafika ofisi husika na kukutana na mtumishi ambaye anakuhudumia leo. Bahati mbaya ofisi za umma jambo lako haliwezi isha kwa siku moja. Sasa utakaporudi kesho na viambatanisho ulivyoagizwa unakutana na mtumishi mwingine ambaye naye anakosoa viambatanisho ulivyoagizwa awali. Unapoomba kuonana na yule wa awali pengine asiwepo muda huo au vyovyote tu.

Matokeo yake utaondoka na kwenda kufanya kadiri ya mtumishi wa pili alivyoelekeza. Pale unapoona sasa umekalimisha, hasa ujazaji wa nyaraka, makosa mengine yanaibuliwa katika nyaraka zako. Kwao kukuambia rudi kafanye hiki sio ishu. Hawaangalii muda na gharama utakazotumia katika ufuatiliaji.

Sambamba na hilo hawatoi taarifa sahihi kwa wateja kwamba utaratibu ni huu mwanzo hadi mwisho.

Najua kuwa wapo watumishi ambao wanajua kwa usahihi hatua kwa hatua nini cha kufanya ili mteja jambo lake likamilike kwa wakati. Tatizo linakuja pale ambapo utaelekezwa kwa mtumishi ambaye hayuko kwenye hiyo cheni ya huduma. Ndio hao hukosoa jambo ambalo awali lilishawekwa sawa

Kwenye suala la mwendelezo hapa napo pa kutazamwa. Leo unafika ofisi fulani. Unafanya yako kisha yanatokea mapungufu unaambiwa uje kesho. Kesho ukija unakutana na mtumishi nwingine au unaelekezwa kwa mwingine ambaye anataka uanze kumwelezea jambo lako upya. Inakera sana. Mwisho unamaliza jambo lako kwa kuchelewa, na pe gine ukiwa nje ya muda.

Utumishi wa umma ni sehemu muhimu sana. Hata kama nitaelekezwa kwa mtumishi mwingine kupata huduma ileile au mwendelezo wake, basi ajue afanyacho na sio kupiga ramli.

Lingine toka NHIF ni hiki kioja cha kulipia kumtoa au kurekebisha jina la mtegemezi. Kweli? Kwa vigezo vipi nataka kumtoa mtu kwenye list ya wategemezi wangu nipewe control numba nikalipie? Kufuta tu jina la mtu hata baada ya kuambatanisha vielelezo vyote nilipie? Hapa NHIF watupatie ufafanuzi kwa kweli.
 
Njia pekee itakayowezesha hizo changamoto kuisha, ni mpaka tu pale huduma zote zitakuwa zikipatikana mtandaoni,maana viambatanisho husika vitakuwa vinaeleweka. Na hilo litafanikiwa,endapo mfumo wa NIDA utakuwa umekamilika,na kuweza kifikiwa na taasisi nyingine.

Kabla ya hapo,nahisi unatakiwa kujiongeza ili uhudumiwe.

Na kuhusu ilo na NHIF, kwanza sababu ya kufuta jina ni ipi? Kumbuka zipo zisizoeleweka na kukubalika. Kama ilivyo kwenye kuongeza mtu,hata kumfuta usipende mtelezo. Kuna makosa watu wanafanya, lazima yawagalimu au wafikilie mara mbili kabla hawajaamua.
 
Kuhusu mfumo mtandao nao bado tatizo maana nimeenda RITA nikakutana na changamoto hizo. Wanaweka e-service halafu wanakuja kuuingilia manually.

Kuhusu kufuta mtu yawezekana ni marehemu, au alikuwa ni mke/mume na sasa mmeachana. Sambamba na hilo haihalalishi gharama. Kwa hiyo nikishalipia kumtoa mtu na hizo sababu zinakuwa halali?
 
Kwenye kufa au kuachana, ni vielelezo vya kutosha,maana kuna swali moja. Ulimuandikisha mwenyewe. Kama kafa,death certificate ipo wapi. Kama mmeachana, hati ya taraka kisheria ipo wapi. Kama vyote huna, muache aendelee. Hapo kwenye kuomba pesa, nadhani ulitakiwa kujiongeza wakurahisishie. Japokuwa,akimfuta,ikafunguliwa kesi, atajibu nini?! Maana mifumo hii siku hizi na yenyewe mimbea,aliyefuta au kujaza anajulikana tu.
 
Tatizo sio kutoa chochote maana mazingira hayo hayapo. Kama yapo basi ni ya kiufundi sana. Tatizo ni kuwa, hata kama vielelezo vyote umekamilisha, kwa nini pawepo na gharama ya kufuta au kurekebisha jina, ndio hoja yangu
 
Mkuu,labda sitoliingilia sana,maana limekaa kisiasa(mpaka uamzi huo utolewe,kuna majadiliano).
Navyoelewa mimi lakini,simaanishi kwamba inatakiwa iwe hivyo. Hakuna huduma ya bule kwenye taasisi zote za kiserikali,labda zile zenye wafadhili. Labda tuziite tu service charges: unakuta sekta fulani kuna mapato fulani inatakiwa ikusanye. Usishangae documents zote zimekamilika,lakini kulipia lazima.

Nakupa mfano labda wa kubadili jina au kulisahihisha. Ni kazi ya kuedit tu. Lakini mpaka wajue kwa nini,wajiridhishe kujatenda kosa la jinai, huko kote wanakozunguuka,nahisi kuna gharama wanakuwekea. Na kuepuka hilo zoezi mara kwa mara,maana ikiwa bure, leo mtu atamtoa,kesho aandikishe mwingine,keshokutwa amtoe,...... Vitu kama hivyo.
 
Una hoja. Lakini kiuhalisia mtu hakurupuki tu kwenda kumtoa mtegezi, maana anaingia mwingine. Kitendo cha kuwepo wategemezi ni kwamba michango.ya mwanachama inaingia. Zipo huduma zilipaswa kuwa bure na zisizo na konakona kwa lengo la kuongeza tija ila kwa kuwa serikali inatolea macho kodi, tozo, nk wanabaki kufumba macho
 
Back
Top Bottom