Tujadili Mbeya ya viwanda.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
Sera ya sasa ya serikali ni viwanda. https://www.jamiiforums.com/forums/habari-na-hoja-mchanganyiko.42/create-threadkila mkoa unatakiwa kuweka mazingira na kutathmini aina ya viwanda vitajengwa humo. mkoa wa Mbeya unaweza kuwa na viwanda ambavyo vikauza soko la Zambia, DRC, Malawi na Southern Highlands. hilo ni eneo la karibia watu milioni 100. pia usafiri wa anga, barabara na Treni ni rahisi kwenda kwenye masoko hayo. Ni moja ya mikoa michache iliyo sehemu nzuri kwa viwanda. mi naona ingefaa tuanze na viwanda vifuatavyo.

1. viwanda vya nguo. nchi nyingi zinapoanzisha viwanda huanza na hivi vya nguo. pia hivi viwanda havihitaji teknolojia kubwa sana. Tuweke kiwanda cha vitenge pale Mbeya maana nchi hizi watu wake wanapenda mno vitenge. pia viwepo vya jeans, socks, mashuka suruali na mashati.

2. Tujenge kiwanda cha Mbolea. Eneo la songwe pana phosphate nyingi sana. Morocco tuliyoiomba pesa inapata pesa nyingi kutoka kwenye mbolea na ndiyo maana haiiachii western sahara sababu kuna phosphate nyingi.

unafikiri nini kifanyike ili Mbeya itoke kwenye uchumi wa kilimo hadi wa viwanda? viwanda gani vijengwe?

gwankaja, DUBULIHASA, masopakyindi, Bujibuji, Gwankaja Gwakilingo .
 
Nimependa, napenda kuishi mby kuliko dar, tufanye mchakato viwanda huko maana fursa zipo
 
Rohohuwa inaniuma sana nikoina jinsi maembe, maparachichi, ndizi na matunda kadha wa kadha vikioza aukuuzwa bei ya kutupa mkoani Mbeya. Kulipaswa kuwepo na kiwanda cha kusindika haya matunda au cha juisi.mbeya kuna potentials nyingi mnoooo. Am so very proud of being mtoto wa Mbeya.
Note* Ila nakereka na mpangilio mbovu unaochefua roho wa jiji la Mbeya
 
viwanda ambavyo vilitakiwa kuwepo mbeya
kiwanda cha kusindika matunda na kuteletea juice kama za parachichi na ndizi
kiwanda cha kuchakata kakao na kahawa kwenda katika level kama ya majani ya chai
vipodozi ambavyo hutokana na mazao yapatikanayo mbeya
mchele ambao ungeuzwa nchi jirani
mengine muongezee wakazi wa sae, mama john ,uyole,jakalanda ,mafffiat,mwanjelwa bila kuwasahau vijana wa mbalizi kalibuni sana
 
Rohohuwa inaniuma sana nikoina jinsi maembe, maparachichi, ndizi na matunda kadha wa kadha vikioza aukuuzwa bei ya kutupa mkoani Mbeya. Kulipaswa kuwepo na kiwanda cha kusindika haya matunda au cha juisi.mbeya kuna potentials nyingi mnoooo. Am so very proud of being mtoto wa Mbeya.
Note* Ila nakereka na mpangilio mbovu unaochefua roho wa jiji la Mbeya
Mkuu mbeya ni miongoni mwa mikoa inayo zalisha matunda kwa wingi ila naona wanao tuongoza hawautangazi kwa wawekezaji
 
Msimu huu maembe yanaoza tu na pale kiwira kwa mia zote matunda ni mengi mno na ya kila aina hakika kiwanda cha kusindika matunda kinafaa kabisa mby
 
Km walivyosema wadau viwanda vingi vya usindikaji matunda na utengenezaji wa juisi ungesaidia ajira kwa vijana na mkoa ungesonga mbele sana.

Pia nadhan usindikaj wa minofu ya samaki ungesaidia pia kuinua kipato cha wanambeya na mkoa kiujumla kwa sababu mbeya tuna mito, mabwawa na ziwa nyasa. Hata hivyo pia pangefanyika uanzishwaji wa mabwawa ya kufuga samaki ili wananchi wapate kipato baada ya kuwauza hao samaki kwenye viwanda vya usindikaji minofu ya samaki, hii kitu ya kuanzisha mabwawa ingekuwa rahis sana coz mby tuna mvua almost through out the year.

Viwanda vya unga wa aina mbalimbali kwa sababu mby tuna kila aina ya nafaka za kutosha. Nina uhakika soko lote la bahresa tungeliteka ndan na nje ya mby.

Kule kyejo tuna gesi asilia ambayo ingetusaidia kwenye uzalishaji viwandani kwetu.
 
kwakweli tunahitaji kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa kinasindika unga wa mahindi. siyo mahindi yatoke nyanda za juu, yaende Dar au kibaha kusagwa na kisha yaturudie kwenye mifuko. ila ile gas nasikia ni carbon dioxide. kingine ni uwekezaji wa geothermal. wataalamu wanassema maeneo ya Rungwe na Majimoto Songwe kuna ptential kubwa ya geothermal. wakenya wako mbali kwenye geothermal.
 
Tanzania tuna tatizo moja,mazao mengi ni ya msimu,sasa kiwanda hakiwezi kutegemea maligafi za msimu,kwa upande wa mazao ya kilimo tuanze kuelimisha watu kwanza walime kisasa.
 
Back
Top Bottom