Tujadili matumizi ya V8 katika Taifa letu

Tujadili matumizi ya V8 katika Taifa letu

Kuna bifu kati ya mbunge Msukuma na mkurugenzi wa Geita ndipo Msukuma a katengeneza fitna lakini hizo Gari hata CCM wanazo nyingi kuliko hata chama Tawala cha Japan zinakotengenezwa
Miderators,
Please Reserve this supper comment.
 
Bado siamin Kama Ni kweli ununuz unafanywa kwa maamuz ya mtu mmoja..
Hata kama maamuzi yanafanywa na KUNDI LA WATU, hao pia wanaweza kuwa corrupted tu na kufanya maamuzi ya hovyo. Mfano ni maamuzi ya Madiwani wa hiyo Halmashauri inayopigiwa kelele.
 
Polepole aliwahi kutunanga Watanzania akisema wao Kama viongoz wa chama wanatembelea mashangingi na makatibu wa mikoa wanatembelea cruiser hardtop (Kama sikosei), akatuambia wanampango wakuwanunulia viongoz wote magari ya kifahari......hii ilikua kauli ya chama, nadhan wakurugenzi wanaitekeleza kwa vitendo. Msukuma baada yakuona mkurugenzi ana gari nzuri na wakati akisubiri chama kimnunulie V8 kaamua kumwondoa mkurugenzi. Tukumbuke hawa ndio waliofanya yao 28/10/2020 wakaambiwa awatatumbuliwa.....mwanasiasa Hana fadhila
Hard top ni makatibu wa wilaya, na baada ya ushindi wa kushtukiza hard top hazitabaki wilayani zitashuka ngazi ya Kata.
 
V8 ni hasara kwa mlipa Kodi halina umuhimu zaidi ya prestige ufahari kuwatambia masikini
 
Miongozo na go ahead wanazitoa wenyewe, alafu sasa wanajifanya kushangaana...

Siasa ndivyo zilivyo...




Cc: mahondaw
 
Ukweli ni kwamba kwenye halmashauri nyingi budget ya uendeshaji wa haya magari ni kubwa sana kuliko hata budget ya elimu au afya. Ndio jivyo unakuta wanafunzi wanakaa chini au wafonjwa wanakosa hudima mujimu hospitali lkn Viongozi wanajinunilia magari ya kifahari. Nadhani tufike mahali tuaajiri watu wenye usafiri wao kabisa, unawapa posho ya usafiri tuu, hasipotokea kazini unafuta unaajiri mwingine

Ule msamaha wa kodi kwa watumishi kuingiza magari ndo ulikuwa sahihi,Ili wajinunulie magari yao
 
Kama ni wazalendo wa kweli watembelee land lover.
 
Kutumbuliwa kwa Mkurugenzi wa Geita kumeibua mjadala kuhusu kiongozi gani anapaswa kumiliki au kutembelea gani.

Hoja kuu inatokana na kile kinachoelezwa kuwa V8 si anasa kwa wakurugenzi na wamekuwa wakitumia gari hizi kwa miaka kadhaa sasa.

Hi hoja ilipowasilishwa Bungeni wakati wa Spika Makinda ilizua mjadala mkali sana na Serikali ikaazimia kutafuta magari ya bei ya chini lakini baadhi ya mabeberu weusi wakakataa wakidai Mkurugenzi lazima awe na gari la hadhi yake.

Maisha yameenda kasi na karibia viongozi wote waandamizi wa nchi hii wanatumia v8 na mashangingi mengine ya kifahari. Hivyo Mkurugenzi wa Geita amefuata nyayo tu.

Jambo linalozua mtafaruku ni kuhusu utaratibu wa ununuzi wa magari ya Serikali yakiwemo ya wakurugenzi. Je, kwa mfumo wa Sasa ambao fedha zote zipo hazina na huduma nyingi zinalipwa kwa control number, Mkurugenzi alinunua gari bila Hazina kushirikishwa? Je, kama walishirikishwa walipitisha vipi Kibali ambacho kipo kinyume na circula ya serikali? Kwanini wote waliokula mchongo wakuingizia Serikali hasara wasitumbuliwe?

Nadhani Mhe. Jafo tume yako ipe adidu za rejea, moja ya adidu za rejea iwe "kupitia mchakato mzima wa ununuzi wa gari ilo" then wakikuletea ripoti isome public tujifunze mchakato wa manunuzi tujue kama tatizo lipo kwa Mkurugenzi au lipo kwenye mfumo wa manunuzi ili marekebisho yafanyike.
Tatizo nafikiri kila kiongozi anatakiwa kuwa na gari kulingana na hadhi/cheo chake. Mfano kwa hao maDED wanatakiwa kutembelea GX standard, zikifuatiwa na GX-R hizi naziona kwa wakuu wa mikoa, VX na VX-R kwa mawaziri. Sasa DED wa Geita yeye alichofanya ni kuvuta hiyo VX-R ambayo hata mkuu wa mkoa hana hadhi ya kuipata.
 
Piga mnada V8 zote wakurugenzi wa mijini watumie Kruger na wale wa vijijini watumie Pajero iO
 
Back
Top Bottom