Mapendekezo ya serikali ya kupunguza matumizi ya fedha taslimu

Mapendekezo ya serikali ya kupunguza matumizi ya fedha taslimu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Serikali imependekeza mikakati mipya ya kupunguza matumizi ya fedha taslimu na kukuza uchumi wa kidijitali kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Hatua hiyo inajumuisha kuweka sharti la lazima kwa baadhi ya huduma kulipwa kidijitali, pamoja na kusitisha kabisa usambazaji na matumizi ya vocha za kukwangua za simu (scratch cards) katika maeneo yote ya mijini yenye miundombinu wezeshi.

"Eneo la nne ni kupunguza matumizi ya fedha taslimu. Mheshimiwa Spika, ili kupunguza matumizi ya fedha taslimu katika mwaka wa 2026/27 inapendekezwa kufanya maboresho yafuatayo:

Mosi, kuweka sharti la baadhi ya malipo ya huduma na biashara kufanyika kwa njia za kidijitali kama ilivyoainishwa katika aya ya 61 ya hotuba yangu.

Pili, kusitisha usambazaji wa matumizi ya vocha za kukwangua za muda wa maongezi katika maeneo yote ya mijini ili kuendelea kuwezesha malipo ya kidijitali.

Tatu, kuweka sharti la matumizi ya vifaa vya malipo ya kidijitali yaani Lipanamba na Lipa kwa QR kama moja ya kigezo wakati wa utoaji na uhuishaji wa leseni za biashara.

Nne, kuweka sharti la kufungua akaunti ya benki kama moja ya kigezo kwa utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara na ushirika katika shughuli za madini, mifugo, mazao, mbao, na uvuvi, na kuhakikisha miamala inafanyika kupitia akaunti husika.


Na tano, kuweka sharti la uthibitisho wa malipo ya kidijitali kuwa rejea ya lazima itakayotumika kuidhinisha maombi ya uhamishaji wa mali kama vile ardhi, majengo, na magari kama inavyoelezwa katika aya ya 64 ya hotuba yangu"


 
Nchi hii kwa kweli, sasa hapo wasaidia watu au wanawaumiza watu. Mfano kulipa kwa simu hayo makato ya mitandao nani anawajibika nayo
 
Back
Top Bottom