Tujadili kuhusu "VAT"

Hii ni nadharia nzuri sana kuisoma lakini ukweli ni kwamba kila utakapokwenda, Duniani kote, VAT hulipwa na mlaji na siyo mwuzaji.

Hivi pale bandarini, uleagiza gari lako, unalipishwa VAT, anayelipa ni yule aliyekuuzia gari au wewe uliyenunua?

Habari ni ndefu lakini ya kupotosha wasiojua. Kwenye nchi nyingi za wenzetu bei zote unazoambiwa, hazina VAT, wakati wa malipo ndiyo utaongezewa VAT. Kwenye risiti ya malipo, hata kwenye zile mashine, inaonesha bei ya kitu, halafu VAT, ambacho ni kiasi ambacho umeongezewa wewe mnunuzi baada ya kulipia ile bidhaa.

Huyu mwenzetu ameamua kuwafurahisha watu.
 
Nadhani shida ni kuwa katika chochote kuna gharama za uzalishaji..ambazo plus VAT ndio bei ya kitu???? Sasa kama VAT ilikuwa haijawa imposed at the bwginning...na bei ilikuwa ni ile.tu ya uzalishaji what do we do??? Naomba somo hapa
 
Noqchojua mimi kwa akili yangu fupi makampuni makubwa au waagizaji hukusanya VAT kutoka.kwa walaji kwa niaba ya serekali na si walipaji wa VAT?? .... ndio maana ukienda.kwenye DUTY FREE SHOPS hakuna VAT na wenye maduka.haya hawadaiwi VAT na serekali zao??naomba kurudishwa darasani
 
Heh! Tena?
Jenniec achana na huyu msukule wa BRN .......meza meza wa mfumo wa elimu......hata hajaelewa nilichozungumzia amedandia treni kwa mbele............nilichokuelewesha ndicho hicho hicho..........ila ni kwamba hakifanyiki kama nilivyokielezea.........
 
Tuache kuzunguka, hii ni consumption tax mlaji ndy analipa hii kodi na sio mzalishaji ikiwa kama tunahitaji mzalishaji wa huduma alipe basi tutafute jina lingine la kodi hii. Tatizo tulilonalo hivi sasa watu hawataki kusema ukweli nani anastahili kulipa. Kwa mfano kamishna mkuu wa TRA anasema VAT analipa mtoa huduma hii ni kitu cha ajabu sijawahi kukiona na huyu ameamua kujitoa ufahamu kwa hofu ya ajira yake. Watu wanaosikiliza mabishano hay mwisho wa siku watatuona wajinga au mzumbukuku yaan VAT alipe mlaji kama ni kweli kamishna mkuu TRA mwambie mwanao atoe jibu hili kwenye mtihani wa swali moja uone kama hatapata sifuri
 
daaas. wajameni mmetuvuruga. which is which. sisi tunafata maagizo ya serikali ndio final. ambayo TRA wenyewe ndio waliyaeleza. wao ndio wataalam wa kukusanya kodi. fullstop. sijajua huu uzi maana yake nini
 
....
Example

Consider the manufacture and sale of any item, which in this case we will call a widget. In what follows, the term "gross margin" is used rather than "profit". Profit is the remainder of what is left after paying other costs, such as rent and personnel costs.

Without any taxEditA widget manufacturer, for example, spends $1.00 on raw materials and uses them to make a widget.The widget is sold wholesale to a widget retailer for $1.20, leaving a gross margin of $0.20.The widget retailer then sells the widget to a widget consumer for $1.50, leaving a gross margin of $0.30.

With a sales taxEdit

With a 10% sales tax:

The manufacturer spends $1.00 for the raw materials, certifying it is not a final consumer.The manufacturer charges the retailer $1.20, checking that the retailer is not a consumer, leaving the same gross margin of $0.20.The retailer charges the consumer ( $1.50 x 1.10 ) = $1.65 and pays the government $0.15, leaving the gross margin of $0.30.

So the consumer has paid 10% ($0.15) extra, compared to the no taxation scheme, and the government has collected this amount in taxation. The retailers have not paid any tax directly (it is the consumer who has paid the tax), but the retailer has to do the paperwork in order to correctly pass on to the government the sales tax it has collected. Suppliers and manufacturers only have the administrative burden of supplying correct certifications, and checking that their customers (retailers) are not consumers.
 
Jenniec achana na huyu msukule wa BRN .......meza meza wa mfumo wa elimu......hata hajaelewa nilichozungumzia amedandia treni kwa mbele............nilichokuelewesha ndicho hicho hicho..........ila ni kwamba hakifanyiki kama nilivyokielezea.........
Ok
 
Maelezo mengi lakini unakosea kulinganisha Habari za juice na issue inayoendelea na mabenk ebu jaribu kufananisha na hiyo issue ya benk na utoedescription kama unayoisema
 
Sasa wewe uliyeelewa utuambie kama huu mfumo ni rafiki kwa maendeleo ya taifa letu na kwa raia.......maana wasomi wa tanzania huwa mnasahau kitu kimoja hii elimu ni ya mkoloni.......na alikuwa anaitumia kumnyonya raia mzawa leo tumerithi bado mnaona ni ujanja........kwa kifupi ukisha maliza degree yako unajiona mzungu ili hali ni mtu mweusi hadi unyayo.....

Soma vizur uelewe hoja niliyoleta sio unaruka tiki taka kwenye sakafu yenye utelezi utatulia kisogo uumie.....

Na hii mifumo ya kurithi haiishii kwenye kodi tu hata kwenye ulinzi na usalama mtaona mambo ni yale yale......askari anapewa mafunzo ya ukatili dhidi ya raia sio mafunzo ya kumtetea ...kumlinda....na kumuelekeza raia ...ila ni kumkung'uta kama ngoma iwe kwa kosa dogo au kubwa........na bado ukikosoa bado watakuja wanaojua zaidi watakwambia hapana askari wanavyofanya ni sahihi hapa nchini......

Inaboa sana watu mnavyeti halafu vimewavimbisha akili tu na manotes ya kumeza na hamjajifunza ili kuibadili direction nchi yetu iende kuzuri........tumia jicho la tatu
naona mkuu unataka kujaza thread..
 
Umepotosha umma brother tena saaana....sometimes kama hamjui how tax system work achieni wataalam wawasaidie wapo tax consultant wapo accountants na economist...sema unachojua
 
I am Certified Public Accountant so consult watu wanaojua before saying anything which is techinical
 
Neno VAT ni neno la kiuchumi au la kibiashara la lugha ya kiingereza(english) ikiwa ni ufupisho wa maneno "VALUE ADDED TAX yaani kwa kiswahili ni kodi ya ongezeko la thamani.

VAT ni aina ya kodi ambayo hutozwa kwenye mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa ya aina yeyote kubwa kwa ndogo lakini pia kwa malipo ya huduma zozote! Kwa kifupi ni kiasi ambacho hutozwa kwa muamala wowote na hutozwa kwa yule anayepokea tu na si mtoaji.

Kwa muda mrefu serikali yetu imekuwa ikitoza aina hii ya kodi kwenye malipo yanayofanyika katika manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchini(si mauzo yote hufanikiwa kuchajiwa kwasababu ya ukwepaji kodi na mifumo isiyokidhi mahitaji pamoja na biashara nyingi kutokuwa rasmi). Aina hii ya kodi hukadiriwa kulingana naongezeko la thamani au kushuka kwa thamani ya bidhaa au huduma usika.......tafsiri yake ni kuwa kama bidhaa au huduma itapanda au kushuka bei then kiwango cha kodi inayochajiwa nacho kitapanda au kushuka kulingana na asilimia ambayo hutozwa.....( kwasasa ni asilimia 18).

Kuna kasumba ambayo imejengeka katika akili za watanzania (wasomi na hata wasio wasomi) kuwa tozo la kodi ya V.A.T huwa inatakiwa kulipwa na mnunuaji wa bidhaa pale anapokwenda dukani kwa maana ya kwamba hii kodi tokea bidhaa ina nunuliwa basi kila anayeuza hii bidhaa humtupia mzigo wa kulipa anayenunua bidhaa kitu ambacho si sahihi. Ntakupa mfano ili unielewe vema.......Tutachukulia kiwango cha VAT ni asilimia kumi (10%) ili kurahisisha mahesabu........ila kiwango halisi cha VAT kwa sasa ni asilimia kumi na nane (18%).
mfano,


bakhresa anazalisha juice ya azam mango Juice hii hutengenezwa na maembe. Bakhresa anakwenda shambani kwa mkulima ambaye tutachukulia anamiembe ambayo ni ya asili hivyo hakuna gharama yeyote ya uzalishaji hapo ila tu ameisimamia miembe yake imekuwa na imezaa kwahiyo pesa ya kwanza katika hii scenario ni wakati bakhresa analipia maembe kwaajiri ya kupeleka kiwandani kwake kwaajiri ya kukamua juice.

Tuchukulie bakhresa amechukua tani 10 ambazo ni kwa ujumla wake amemlipa mkulima shilingi laki mbili (200,000/=). Sasa hapa ndio habari ya VAT huanza........kwa maana huu ni muamala wa kwanza wa malipo ya kifedha unafanyika kutoka kwa bakhressa kwenda kwa mkulima.

Hivyo basi.....mkulima hypothetically anatakiwa kuwa na ile mashine na TRA ili amuandikie risiti bakhresa na kuwapatia serikali kupitia wakala wake (TRA) mapato yao ya asilimia kumi (10%) kodi ya tozo la ongezeko la thamani kutoka sifuri (0) hadi laki mbili (200,000) ambayo itakuwa ni shilingi elfu ishirini (20,000). Hivyo basi bakhresa hatotakiwa kulipa zaidi ya 200,000/= kwa mkulima na hatolipa chochote kwa serikali maana yeye hajapokea chochote ila ametoa. Mkulima atatakiwa kubaki na 180,000/= baada ya kutoa 20,000/= ya VAT

Bakhressa atasafirisha huu mzigo kwenda kiwandani kwake kwakutumia fuso ya mtu binafsi anaetoa huduma hiyo.......tuchukulie atalipia 30,000 kama gharama ya usafiri. Pia huyu msafirishaji anatakiwa kuwa na Kifaa cha risiti cha tra ili aweze kulipa vat kila wakati mtu anapofanya malipo kwake. Hivyo basi katika hatua hii pia msafirishaji atatakiwa kulipa 10% ya 30,000 kama VAT bakhressa hatalipia zaidi ya 30,000 na VAT haimuhusu maana hajapokea ametoa.
Baada ya mzigo kufika kiwandani bakressa ataanza kutengeneza juice yake.......tuchukulie kwamba maembe yanatoa juice nyingi kiasi kwamba anaweza kupanga bei ya sh.2500/= kwenda kwa muuzaji wa jumla shilingi 2000 /= ni kufidia gharama alizoingiza na 500 ni faida kwaajiri yake. Tuchukulie Mangi mwenye duka la jumla amekuja kununua boksi 100 za juice ya bakhressa ambazo zitamgharimu sh. 250,000/= .....bakhressa atatakiwa kulipa VAT kwasababu katika muamala huu yeye ndiye anapokea Mangi hatotakiwa kulipa zaidi ya 250,000/= kwa bakhressa ili kupata hizo boksi 100.Hivyo basi bakhressa atapokea sh. 250,000/= na atakata VAT ambayo ni 10% ya 250,000/= ambayo ni sh.25,000/= iende serikalini na yeye atabaki na 225,000/=.
Mangi atakwenda na mzigo dukani kwake ili akauze reja reja kwa wauzaji wa reja reja. Mangi atalipia usafiri wa bajaji kubeba hizi boksi 100. Tufanye bajaji ni sh.5000/=. Huyu jamaa wa bajaji anatakiwa kuwa na kile kifaa cha TRA pia ili alipe kodi. Hivyo tuchukulie anacho hivyo basi atalipa vat pia 10% ya sh.5000/= ambayo ni shiling 500/= Mangi hatolipia chochote zaidi ya 5000 hapa........Mzigo utafika dukani kwa Mangi tayari kwaajiri ya mauzo.
Mangi atauza kila boksi kumi kwa bei ya sh. 3000 kila boksi hivyo bei yake ya jumla ni sh. 30,000/=. Muuzaji wa rejareja anayeitwa Faki atakwenda dukani kwa Mangi kununua mzigo wake ili apeleke dukani kwake kuuza reja reja. Faki atamlipa Mangi shilingi 30,000 kwa boski kumi. Faki hatolipia VAT hapa na hatomlipa Mangi zaidi ya sh. 30,000/= .......Mangi atakiwa anatakiwa ampe Faki risiti ya TRA kutoka katika kifaa cha tra ambayo itaonyesha kuwa amelipia VAT (10% ya sh. 30,000/=) ambayo ni sh. 3000/= kwenda serikilini kupitia TRA. Faki atakwenda na hii bidhaa dukani kwake ili akauze reja reja kwa boksi moja moja kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mimi au wewe. Faki atapanda Boda boda pia atalipia gharama ya sh. 3000/=. Boda boda atatakiwa ampatie risiti ya TRA Faki kwa malipo yaliyofanyika ambapo bodaboda atalipia VAT kwa serikali kupitia kifaa cha TRA(Tanzania bado havijaletwa ila tunatakiwa kuwa navyo) boda boda atalipa sh.300/= kwenda serikalini kupitia TRA.Faki hatolipia VAT hapa na hatolipia zaidi ya sh.3000/= kwaajiri ya gharama za usafiri. Faki atafika dukani pake na kuweka maboksi ya juice tayari kwa kuuza. Mimi nitakwenda dukani kwa faki kununua juice boksi moja. Faki anauza boksi moja ya juice kwa bei ya sh.3500/=. Mimi nitanunua hii box kwa shilingi 3500/= hiyo hiyo. Faki atalipia VAT 10% ya 3500/=ambayo ni 350/= iende serikalini kupitia tra. Mimi hapa sitotakiwa kulipia zaidi ya sh.3500/= na sitolipia VAT kamwe kwasababu nimelipia na sitauza ninakwenda kuitumia hii juice. Hapa ndipo kodi aina ya Vat hukomea kwa muuzaji wa mwisho. Kama umefuatilia vizuri huo mtiririko basi utakuwa umejifunza mambo mengi kuhusu VAT. Mojawapo ni kuwa....
(1)VAT hailipwi na anayenunua bidhaa au huduma ila anayeuza ndiye hulipa..
(2)Vat huchajiwa kama tozo ya ongezeko la thamani na hivyo basi huchatozwa pale tu ambapo kuna muamala mpya unafanyika yaani mauziano mapya.
(3)VAT kwa tanzania kiuhalisia tofauti na kwenye mfano hapo juu huwa inarushwa au hukwepwa na wanaouza bidhaa au huduma kwa kuificha ndani ya bei wanayokupa na ukiwahoji wanakwambia vat imepanda ndio maana na bei imepanda .....hili ni kosa kubwa kisheria na wengi huwa wanalifanya wakijua ni haki yao kumbe si halali hata kidogo kwa wao kulipa vat halafu ile vat wanairudisha kijanja kwenye bei ya vitu wanavyouza au huduma mfano hapo faki angeniuzia mimi juice kwa bei ya sh. 3,850/= badala ya 3500 ili ndani ya hiyo bei akwepe Kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT nimlipie mimi.
Nakaribisha maswali.........uchangiaji........na pia nyongeza kama kuna kitu kimepungua au hakipo sawa.

HIYO SCENARIO YAKO HIJAKAA VIZURI NENDA KASOME VAT ACT NA GOOGLE HOW VAT WORKS UTAOUNA FROM POINT OF MANUFACTURE TO END SELLER NA NI ONLY VAT REGISTERED ANA ADD VAT, KWENYE MFANO WAKO HAPA KAMA BAKHRESA AKINUNUA MAEMBE KWA MKULIMA ALIYESAJILIWA NA VAT ATAMWEKEWA BAKHRESA18% (MF 500+18%(500)= 590) HIYO VAT TUNAITA INPUT TAX, NA VIVYO VIVYO KWENYE USAFIRISHAJI NA GHARAMA ZOTE WATAMWEKEA, ILA COST ZAKE NI ZILE TU KABLA YA VAT, AKISHATENGENEZA JUICE AKISET SP =COST+ PROFIT, ATA ADD 18% YA VAT INAITWA OUTPUT TAX, ATAKACHOFANYA ATACHUKUA OUTPUT TAX -INPUT TAX IKIWA KUBWA ANAWALIPA TRA, IKIWA NDOGO ANALIPWA NA TRA, HIVYO NDO NCHANGANUO WA VAT ULIVYO NA NDO MAANA INAITWA TAX ON CONSUPTION KITAALAMU WANASEMA NI INDIRECT TAX, VAT REGISTERED YY NI WAKALA WA KUKUSANYA VAT HALIPI YY,
 
HIYO SCENARIO YAKO HIJAKAA VIZURI NENDA KASOME VAT ACT NA GOOGLE HOW VAT WORKS UTAOUNA FROM POINT OF MANUFACTURE TO END SELLER NA NI ONLY VAT REGISTERED ANA ADD VAT, KWENYE MFANO WAKO HAPA KAMA BAKHRESA AKINUNUA MAEMBE KWA MKULIMA ALIYESAJILIWA NA VAT ATAMWEKEWA BAKHRESA18% (MF 500+18%(500)= 590) HIYO VAT TUNAITA INPUT TAX, NA VIVYO VIVYO KWENYE USAFIRISHAJI NA GHARAMA ZOTE WATAMWEKEA, ILA COST ZAKE NI ZILE TU KABLA YA VAT, AKISHATENGENEZA JUICE AKISET SP =COST+ PROFIT, ATA ADD 18% YA VAT INAITWA OUTPUT TAX, ATAKACHOFANYA ATACHUKUA OUTPUT TAX -INPUT TAX IKIWA KUBWA ANAWALIPA TRA, IKIWA NDOGO ANALIPWA NA TRA, HIVYO NDO NCHANGANUO WA VAT ULIVYO NA NDO MAANA INAITWA TAX ON CONSUPTION KITAALAMU WANASEMA NI INDIRECT TAX, VAT REGISTERED YY NI WAKALA WA KUKUSANYA VAT HALIPI YY,
Hapa naanza kupata picha mbili zenye jina moja ila muonekano tofauti zote ni VAT ila mlipaji ndipo utofauti unajitokeza na katika uchunguzi wangu hii yako inatumika kwa 99% katika mzingira yetu.
Ombi langu kama ungeweza kutoa ufafanuzi kama wa mleta maada ungetusaidia wengi na tukapata elimu ya kutosha kabisa.
 
VAT inalipwa na Mfanyabiashara (Impact),
Mzigo anabeba Consumer (Incidence).

Hii ni tabia ya INDIRECT TAX zote, always Impact na Incidence hua ni kwa watu wawili tofauti
 
Napenda nifufue hii mada kwa kuuliza swali jinsi gan Tanzania mainland na Zanzibar wanavyokusanya VAT.


Ukiingiza mzigo kupitia bandari ya Dsm tunalipa VAT, mteja akija kutoka Zanzibar nikimuuzia mzigo nae akifika bandari ya Zanzibar anachajiwa tena VAT hii imekaaje,

Tunafanyaje hapo ili mteja asiumie kwa sababu nchi ni moja???

Msaada plz,
 
Neno VAT ni neno la kiuchumi au la kibiashara la lugha ya kiingereza(english) ikiwa ni ufupisho wa maneno "VALUE ADDED TAX yaani kwa kiswahili ni kodi ya ongezeko la thamani.

VAT ni aina ya kodi ambayo hutozwa kwenye mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa ya aina yeyote kubwa kwa ndogo lakini pia kwa malipo ya huduma zozote! Kwa kifupi ni kiasi ambacho hutozwa kwa muamala wowote na hutozwa kwa yule anayepokea tu na si mtoaji.

Kwa muda mrefu serikali yetu imekuwa ikichaji aina hii ya kodi kwenye malipo yanayofanyika katika manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchini(si mauzo yote hufanikiwa kuchajiwa kwasababu ya ukwepaji kodi na mifumo isiyokidhi mahitaji pamoja na biashara nyingi kutokuwa rasmi).
Aina hii ya kodi hukadiriwa kulingana naongezeko la thamani au kushuka kwa thamani ya bidhaa au huduma usika.......tafsiri yake ni kuwa kama bidhaa au huduma itapanda au kushuka bei then kiwango cha kodi inayochajiwa nacho kitapanda au kushuka kulingana na asilimia ambayo hutozwa.....( kwasasa ni asilimia 18).

Kuna kasumba ambayo imejengeka katika akili za watanzania (wasomi na hata wasio wasomi) kuwa tozo la kodi ya V.A.T huwa inatakiwa kulipwa na mnunuaji wa bidhaa pale anapokwenda dukani kwamaana ya kwamba hii kodi tokea bidhaa ina nunuliwa basi kila anayeuza hii bidhaa humtupia mzigo wa kulipa anayeishia wa mwisho kitu ambacho si sahihi. Ntakupa mfano ili unielewe vema.......

Mfano:

Tutachukulia kiwango cha VAT ni asilimia kumi (10%) ili kurahisisha mahesabu........ila kiwango halisi cha VAT kwa sasa ni asilimia kumi na nane (18%).


mfano, bakhresa anazalisha juice ya azam mango
Juice hii hutengenezwa na maembe. Bakhresa anakwenda shambani kwa mkulima ambaye tutachukulia anamiembe ambayo ni ya asili hivyo hakuna gharama yeyote ya uzalishaji hapo ila tu ameisimamia miembe yake imekuwa na imezaa kwahiyo pesa ya kwanza katika hii scenario ni wakati bakhresa analipia maembe kwaajiri ya kupeleka kiwandani kwake kwaajiri ya kukamua juice.

Tuchukulie bakhresa amechukua tani 10 ambazo ni kwa ujumla wake amemlipa mkulima shilingi laki mbili (200,000/=). Sasa hapa ndio habari ya VAT huanza........kwa maana huu ni muamala wa kwanza wa malipo ya kifedha unafanyika kutoka kwa bakhressa kwenda kwa mkulima. Hivyo basi.....mkulima hypothetically anatakiwa kuwa na ile mashine na TRA ili amuandikie risiti bakhresa na kuwapatia serikali kupitia wakala wake (TRA) mapato yao ya asilimia kumi (10%) kodi ya tozo la ongezeko la thamani kutoka sifuri (0) hadi laki mbili (200,000) ambayo itakuwa ni shilingi elfu ishirini (20,000). Hivyo basi bakhresa hatotakiwa kulipa zaidi ya 200,000/= kwa mkulima na hatolipa chochote kwa serikali maana yeye hajapokea chochote ila ametoa. Mkulima atatakiwa kubaki na 180,000/= baada ya kutoa 20,000/= ya VAT.

Bakhressa atasafirisha huu mzigo kwenda kiwandani kwake kwakutumia fuso ya mtu binafsi anaetoa huduma hiyo.......tuchukulie atalipia 30,000 kama gharama ya usafiri. Pia huyu msafirishaji anatakiwa kuwa na Kifaa cha risiti cha tra ili aweze kulipa vat kila wakati mtu anapofanya malipo kwake. Hivyo basi katika hatua hii pia msafirishaji atatakiwa kulipa 10% ya 30,000 kama VAT bakhressa hatalipia zaidi ya 30,000 na VAT haimuhusu maana hajapokea ametoa.
Baada ya mzigo kufika kiwandani bakressa ataanza kutengeneza juice yake.......tuchukulie kwamba maembe yanatoa juice nyingi kiasi kwamba anaweza kupanga bei ya sh.2500/= kwenda kwa muuzaji wa jumla shilingi 2000 /= ni kufidia gharama alizoingiza na 500 ni faida kwaajiri yake.

Tuchukulie Mangi mwenye duka la jumla amekuja kununua boksi 100 za juice ya bakhressa ambazo zitamgharimu sh. 250,000/= .....bakhressa atatakiwa kulipa VAT kwasababu katika muamala huu yeye ndiye anapokea Mangi hatotakiwa kulipa zaidi ya 250,000/= kwa bakhressa ili kupata hizo boksi 100.
Hivyo basi bakhressa atapokea sh. 250,000/= na atakata VAT ambayo ni 10% ya 250,000/= ambayo ni sh.25,000/= iende serikalini na yeye atabaki na 225,000/=.

Mangi atakwenda na mzigo dukani kwake ili akauze reja reja kwa wauzaji wa reja reja. Mangi atalipia usafiri wa bajaji kubeba hizi boksi 100. Tufanye bajaji ni sh.5000/=. Huyu jamaa wa bajaji anatakiwa kuwa na kile kifaa cha TRA pia ili alipe kodi. Hivyo tuchukulie anacho hivyo basi atalipa vat pia 10% ya sh.5000/= ambayo ni shiling 500/= Mangi hatolipia chochote zaidi ya 5000 hapa........
Mzigo utafika dukani kwa Mangi tayari kwaajiri ya mauzo. Mangi atauza kila boksi kumi kwa bei ya sh. 3000 kila boksi hivyo bei yake ya jumla ni sh. 30,000/=.
Muuzaji wa rejareja anayeutwa Faki atakwenda dukani kwa Mangi kununua mzigo wake ili apeleke dukani kwake kuuza reja reja.
Faki atamlipa Mangi shilingi 30,000 kwa boski kumi. Faki hatolipia VAT hapa na hatomlipa Mangi zaidi ya sh. 30,000/= .......Mangi atakiwa anatakiwa ampe Faki risiti ya TRA kutoka katika kifaa cha tra ambayo itaonyesha kuwa amelipia VAT (10% ya sh. 30,000/=) ambayo ni sh. 3000/= kwenda serikilini kupitia TRA.
Faki atakwenda na hii bidhaa dukani kwake ili akauze reja reja kwa boksi moja moja kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mimi au wewe.
Faki atapanda Boda boda pia atalipia gharama ya sh. 3000/=. Boda boda atatakiwa ampatie risiti ya TRA Faki kwa malipo yaliyofanyika ambapo bodaboda atalipia VAT kwa serikali kupitia kifaa cha TRA(Tanzania bado havijaletwa ila tunatakiwa kuwa navyo) boda boda atalipa sh.300/= kwenda serikalini kupitia TRA.Faki hatolipia VAT hapa na hatolipia zaidi ya sh.3000/= kwaajiri ya gharama za usafiri.

Faki atafika dukani pake na kuweka maboksi ya juice tayari kwa kuuza.
Mimi nitakwenda dukani kwa faki kununua juice boksi moja.
Faki anauza boksi moja ya juice kwa bei ya sh.3500/=. Mimi nitanunua hii box kwa shilingi 3500/= hiyo hiyo. Faki atalipia VAT 10% ya 3500/=ambayo ni 350/= iende serikalini kupitia tra.
Mimi hapa sitotakiwa kulipia zaidi ya sh.3500/= na sitolipia VAT kamwe kwasababu nimelipia na sitauza ninakwenda kuitumia hii juice. Hapa ndipo kodi aina ya Vat hukomea kwa muuzaji wa mwisho.

Kama umefuatilia vizuri huo mtiririko basi utakuwa umejifunza mambo mengi kuhusu VAT. Mojawapo ni kuwa....
(1)VAT hailipwi na anayenunua bidhaa au huduma ila anayeuza ndiye hulipa..

(2)Vat huchajiwa kama tozo ya ongezeko la thamani na hivyo basi huchatozwa pale tu ambapo kuna muamala mpya unafanyika yaani mauziano mapya.

(3)VAT kwa tanzania kiuhalisia tofauti na kwenye mfano hapo juu huwa inarushwa au hukwepwa na wanaouza bidhaa au huduma kwa kuificha ndani ya bei wanayokupa na ukiwahoji wanakwambia vat imepanda ndio maana na bei imepanda .....hili ni kosa kubwa kisheria na wengi huwa wanalifanya wakijua ni haki yao kumbe si halali hata kidogo kwa wao kulipa vat halafu ile vat wanairudisha kijanja kwenye bei ya vitu wanavyouza au huduma
mfano
hapo faki angeniuzia mimi juice kwa bei ya sh. 3,850/= badala ya 3500 ili ndani ya hiyo bei akwepe Kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT nimlipie mimi.



Nakaribisha maswali.........uchangiaji........na pia nyongeza kama kuna kitu kimepungua au hakipo sawa.
Mimi sio mwanauchumi, ila nahisi kuna kitu hakipo sawa kwani kwa hayo maelezo yako; haijani ingia akilini bidhaa moja ya maembe ikalipiwe VAT zote hizo kwa kila hatua? si itapanda bei sana ishindwe kuuzika?
Lakini pia umesema VAT ni value added TAX, kwa kiswahili ni kodi ya ongezeko la dhamani; sasa
Mkulima aliyeuza maembe kwanini achajiwe VAT kwani ameongeza dhamani gani kwenye hayo maembe?
Mwisho kabisa, Bidhaa moja hailipiwi VAT mara nyingi hivyo, kwa hiyo kuna mahala unatakiwa upunguze (offset) ile VAT iliyokwisha lipiwa mwanzo; sasa sina hakika kama wewe ni mwanauchumi au umesoma tu kwenye mitandao; hii INAMAANISHA huna elimu ya kutosha kufundisha watu habari za VAT
 
Back
Top Bottom