Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,705
Neno VAT ni neno la kiuchumi au la kibiashara la lugha ya kiingereza(english) ikiwa ni ufupisho wa maneno "VALUE ADDED TAX yaani kwa kiswahili ni kodi ya ongezeko la thamani.
VAT ni aina ya kodi ambayo hutozwa kwenye mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa ya aina yeyote kubwa kwa ndogo lakini pia kwa malipo ya huduma zozote! Kwa kifupi ni kiasi ambacho hutozwa kwa muamala wowote na hutozwa kwa yule anayepokea tu na si mtoaji.
Kwa muda mrefu serikali yetu imekuwa ikichaji aina hii ya kodi kwenye malipo yanayofanyika katika manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchini(si mauzo yote hufanikiwa kuchajiwa kwasababu ya ukwepaji kodi na mifumo isiyokidhi mahitaji pamoja na biashara nyingi kutokuwa rasmi).
Aina hii ya kodi hukadiriwa kulingana naongezeko la thamani au kushuka kwa thamani ya bidhaa au huduma usika.......tafsiri yake ni kuwa kama bidhaa au huduma itapanda au kushuka bei then kiwango cha kodi inayochajiwa nacho kitapanda au kushuka kulingana na asilimia ambayo hutozwa.....( kwasasa ni asilimia 18).
Kuna kasumba ambayo imejengeka katika akili za watanzania (wasomi na hata wasio wasomi) kuwa tozo la kodi ya V.A.T huwa inatakiwa kulipwa na mnunuaji wa bidhaa pale anapokwenda dukani kwamaana ya kwamba hii kodi tokea bidhaa ina nunuliwa basi kila anayeuza hii bidhaa humtupia mzigo wa kulipa anayeishia wa mwisho kitu ambacho si sahihi. Ntakupa mfano ili unielewe vema.......
Mfano:
Tutachukulia kiwango cha VAT ni asilimia kumi (10%) ili kurahisisha mahesabu........ila kiwango halisi cha VAT kwa sasa ni asilimia kumi na nane (18%).
mfano, bakhresa anazalisha juice ya azam mango
Juice hii hutengenezwa na maembe. Bakhresa anakwenda shambani kwa mkulima ambaye tutachukulia anamiembe ambayo ni ya asili hivyo hakuna gharama yeyote ya uzalishaji hapo ila tu ameisimamia miembe yake imekuwa na imezaa kwahiyo pesa ya kwanza katika hii scenario ni wakati bakhresa analipia maembe kwaajiri ya kupeleka kiwandani kwake kwaajiri ya kukamua juice.
Tuchukulie bakhresa amechukua tani 10 ambazo ni kwa ujumla wake amemlipa mkulima shilingi laki mbili (200,000/=). Sasa hapa ndio habari ya VAT huanza........kwa maana huu ni muamala wa kwanza wa malipo ya kifedha unafanyika kutoka kwa bakhressa kwenda kwa mkulima. Hivyo basi.....mkulima hypothetically anatakiwa kuwa na ile mashine na TRA ili amuandikie risiti bakhresa na kuwapatia serikali kupitia wakala wake (TRA) mapato yao ya asilimia kumi (10%) kodi ya tozo la ongezeko la thamani kutoka sifuri (0) hadi laki mbili (200,000) ambayo itakuwa ni shilingi elfu ishirini (20,000). Hivyo basi bakhresa hatotakiwa kulipa zaidi ya 200,000/= kwa mkulima na hatolipa chochote kwa serikali maana yeye hajapokea chochote ila ametoa. Mkulima atatakiwa kubaki na 180,000/= baada ya kutoa 20,000/= ya VAT.
Bakhressa atasafirisha huu mzigo kwenda kiwandani kwake kwakutumia fuso ya mtu binafsi anaetoa huduma hiyo.......tuchukulie atalipia 30,000 kama gharama ya usafiri. Pia huyu msafirishaji anatakiwa kuwa na Kifaa cha risiti cha tra ili aweze kulipa vat kila wakati mtu anapofanya malipo kwake. Hivyo basi katika hatua hii pia msafirishaji atatakiwa kulipa 10% ya 30,000 kama VAT bakhressa hatalipia zaidi ya 30,000 na VAT haimuhusu maana hajapokea ametoa.
Baada ya mzigo kufika kiwandani bakressa ataanza kutengeneza juice yake.......tuchukulie kwamba maembe yanatoa juice nyingi kiasi kwamba anaweza kupanga bei ya sh.2500/= kwenda kwa muuzaji wa jumla shilingi 2000 /= ni kufidia gharama alizoingiza na 500 ni faida kwaajiri yake.
Tuchukulie Mangi mwenye duka la jumla amekuja kununua boksi 100 za juice ya bakhressa ambazo zitamgharimu sh. 250,000/= .....bakhressa atatakiwa kulipa VAT kwasababu katika muamala huu yeye ndiye anapokea Mangi hatotakiwa kulipa zaidi ya 250,000/= kwa bakhressa ili kupata hizo boksi 100.
Hivyo basi bakhressa atapokea sh. 250,000/= na atakata VAT ambayo ni 10% ya 250,000/= ambayo ni sh.25,000/= iende serikalini na yeye atabaki na 225,000/=.
Mangi atakwenda na mzigo dukani kwake ili akauze reja reja kwa wauzaji wa reja reja. Mangi atalipia usafiri wa bajaji kubeba hizi boksi 100. Tufanye bajaji ni sh.5000/=. Huyu jamaa wa bajaji anatakiwa kuwa na kile kifaa cha TRA pia ili alipe kodi. Hivyo tuchukulie anacho hivyo basi atalipa vat pia 10% ya sh.5000/= ambayo ni shiling 500/= Mangi hatolipia chochote zaidi ya 5000 hapa........
Mzigo utafika dukani kwa Mangi tayari kwaajiri ya mauzo. Mangi atauza kila boksi kumi kwa bei ya sh. 3000 kila boksi hivyo bei yake ya jumla ni sh. 30,000/=.
Muuzaji wa rejareja anayeutwa Faki atakwenda dukani kwa Mangi kununua mzigo wake ili apeleke dukani kwake kuuza reja reja.
Faki atamlipa Mangi shilingi 30,000 kwa boski kumi. Faki hatolipia VAT hapa na hatomlipa Mangi zaidi ya sh. 30,000/= .......Mangi atakiwa anatakiwa ampe Faki risiti ya TRA kutoka katika kifaa cha tra ambayo itaonyesha kuwa amelipia VAT (10% ya sh. 30,000/=) ambayo ni sh. 3000/= kwenda serikilini kupitia TRA.
Faki atakwenda na hii bidhaa dukani kwake ili akauze reja reja kwa boksi moja moja kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mimi au wewe.
Faki atapanda Boda boda pia atalipia gharama ya sh. 3000/=. Boda boda atatakiwa ampatie risiti ya TRA Faki kwa malipo yaliyofanyika ambapo bodaboda atalipia VAT kwa serikali kupitia kifaa cha TRA(Tanzania bado havijaletwa ila tunatakiwa kuwa navyo) boda boda atalipa sh.300/= kwenda serikalini kupitia TRA.Faki hatolipia VAT hapa na hatolipia zaidi ya sh.3000/= kwaajiri ya gharama za usafiri.
Faki atafika dukani pake na kuweka maboksi ya juice tayari kwa kuuza.
Mimi nitakwenda dukani kwa faki kununua juice boksi moja.
Faki anauza boksi moja ya juice kwa bei ya sh.3500/=. Mimi nitanunua hii box kwa shilingi 3500/= hiyo hiyo. Faki atalipia VAT 10% ya 3500/=ambayo ni 350/= iende serikalini kupitia tra.
Mimi hapa sitotakiwa kulipia zaidi ya sh.3500/= na sitolipia VAT kamwe kwasababu nimelipia na sitauza ninakwenda kuitumia hii juice. Hapa ndipo kodi aina ya Vat hukomea kwa muuzaji wa mwisho.
Kama umefuatilia vizuri huo mtiririko basi utakuwa umejifunza mambo mengi kuhusu VAT. Mojawapo ni kuwa....
(1)VAT hailipwi na anayenunua bidhaa au huduma ila anayeuza ndiye hulipa..
(2)Vat huchajiwa kama tozo ya ongezeko la thamani na hivyo basi huchatozwa pale tu ambapo kuna muamala mpya unafanyika yaani mauziano mapya.
(3)VAT kwa tanzania kiuhalisia tofauti na kwenye mfano hapo juu huwa inarushwa au hukwepwa na wanaouza bidhaa au huduma kwa kuificha ndani ya bei wanayokupa na ukiwahoji wanakwambia vat imepanda ndio maana na bei imepanda .....hili ni kosa kubwa kisheria na wengi huwa wanalifanya wakijua ni haki yao kumbe si halali hata kidogo kwa wao kulipa vat halafu ile vat wanairudisha kijanja kwenye bei ya vitu wanavyouza au huduma
mfano
hapo faki angeniuzia mimi juice kwa bei ya sh. 3,850/= badala ya 3500 ili ndani ya hiyo bei akwepe Kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT nimlipie mimi.
Nakaribisha maswali.........uchangiaji........na pia nyongeza kama kuna kitu kimepungua au hakipo sawa.