Tujadili jinsi ya kuwa nchi ya Viwanda

Tujadili jinsi ya kuwa nchi ya Viwanda

Kweli Tanzania ya viwanda inawezekana,
Ila miaka hii Mitano Isihesabiwe kama ni ya viwanda kabisa Bali maandalizi ya Viwanda halisi.
Maandalizi haya yafanywe katika mitazamo ya watu, kilimo, Utafiti wa kina wa masoko ya bidhaa, Miundombinu, Umeme,

Hata Kiongozi wa china Aliponza mabadiliko ya kweli ya kiuchumi Hakuwalaghai Wachina ila aliwambia vitu katika uhalisia.
Kwamba China Inakwenda kuwa Nchi tajiri Sana, Lakini Hatutakuwa wote Matajiri kwa miaka hii mitano ya kwanza. Bali wataanza wachache sana wengine mtakuja baadae. Hii ilikuwa miaka ya 1978, lakn miaka ya 2000 china inaongoza kwa kuwa na matajiri wengi vijana duniani kote. Soma kitabu DENG XIOPING AND TRANSFORMATION OF CHINA.

REALISTIC GOALS AND VISION ISIYOJICHANGANYA NA SIASA NDIO ITATUTOA HAPA. UKWELI NDIO UTALIPONYA TAIFA HILI NA KULIWEKA HURU, HURU KWELI KWELI NA SIO VINGINEVYO. HAKUNA DHAMBI KUBWA KAMA YA UFUASI NA KUJIPENDEKEZA.

NINI KIFANYIKE;
tuwaambie wananchi kuwa HUU NI MCHAKATO WA PHASE YA KWANZA YA TANZANIA YA VIWANDA NA USIMAMIZI WA HALI YA JUU WA FEDHA ZA UMMA, MFANO Baada ya miaka mitano hatutakuwa na haja ya kuimport MITUMBA BADALA YAKE NCHI ITAKUWA NA NGUO SPECIAL NZURI NA ZAKUTOSHA KWA BEI RAFIKI, SIO KUPANDISHA KODI ILI ZISIJE HUTU HATUJUI MASKNINI WASIOKUWA NA UWEZO WA KWENDA KWENYE MABOUTIQUE NA MADUKA YA KISASA HAWAJAWEKEWA MBADALA.

MAONI YANGU
MIAKA HII MITANO ILIPASWA HIWE YA VUGUVUGU LA KUIBADILISHA NCHI KUWA TAIFA LA KIJASILIAMALI TUKIANZA NA BADILIKO LA FIKRA KUHUBIRIWA NCHI NZIMA, MIAKA MITANO IJAYO VIWANDA VITAKUWA NI MATOKEO YASIYOPINGIKA NA YATAKUA AUTOMATIC.

MFANO
bud2015-entrepreneur-image.png
sure kabisa. hata kwenye miracle of river han (South Korea) miaka mitano ya kwanza ilikuwa maandalizi. walikuza kilimo, makaa ya mawe, umeme, chuma na viwanda vya mbolea.
 
Kama china kuzuri basi hamia huko. Hayo ni maneno ya wanasiasa hasa hasa kama ni wachina basi hao macoummunist ndiyo kabisa somo la uchumi linaingia sikio moja linatoka kwingine.

China yenyewe imeendelea kwasababu waliachana na ujamaa na waliacha kutegemea serikali ilete maendeleo. Kutegemea kuwaambia wananchi wavumilie haileti maendeleo yeyote. Tuache kujidanganya.

China bado hawatoi property rights inchi nzima na unakuta 33.1% ya wachina bado wanaishi kwenye umaskini. Miji yao mikubwa inaonekana mizuri na wana matajiri wengi kwasababu wana watu wengi pia lakini ikija kwenye uwekezaji wa mtu wa kawaida inakua shida.
USITUMIE HISIA KUCHAMBUA MAMBO MAKINI.
RUDI UKASOME CONNECTION KATI YA CULTURAL REVOUTION/THE GREAT LEAP FORWAD NA KAI FANG (OPENING UP)
NDIO UTAJUA NINI KILITOKEA NA KWA UTARATIBU GANI.
VITU HIVI VINAENDA KWA MIPANGO NA MIKAKATI MIKALI TENA YENYE CONTINUITY NA UVUMILIVU. NINAPOZUNGUMZIA MATAJIRI NAZUNGUMZIA RATIO. NDIO MAANA LEO MWANZA NI MASIKINI KULIKO MKOA MPYA MANYARA.
Prc1952-2005gdp.gif

Angalia hiyo modal hapo juu. Iliichukua china miaka mitano kwa uchumi kuanza kukua exponentially(1978-1984). Na sio kwa KUIGA UBEBALI bali ni kwa kitu kipya wao walichokiita SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS. Vision ikiwa powered na nguzo nne Mapinduzi ya KILIMO,VIWANDA,SAYANSI na TECHNOLOGY Pamoja na JESHI. Watu maelfu walitumwa Singapole Kujifunza na wengine sehemu mbalibali duniani kuja kuleta ujuzi nyumbani ili china ifanikiwe (SIsi tumeiga lakini walikuwa wanatangatanga wakitafuta posho tu bila kutuletea tija, bora wamezuiwa).

Watafanyaje, Wahamasishwa wanchi chini ya uongozi wa manispaa zao Kufungua Viwanda Vidogovidogo mtaji mdogo lakini vyenye kuleta faida kubwa focus ikiwa ni EXPORT (LIGHT INDUSTRY AND EXPORT LED GROWTH),
Mipango hii matunda yalionekana baada ya miaka mitano. Nguvu kubwa ikisukumwa VIJIJINI katika Surplus Productivity ambayo iliincourage INDUSTRIALIZATION Mijini wakati huohuo wakiwa na SPECIAL INDUSTRIAL ZONES zilizoandaliwa kwa kuvutia Wageni kuwekeza. HAikuwa Kazi ya Siku Moja au Mwaka mmoja.

Hata sisi Tunaweza.
 
Unaweza jenga hivyo viwanda, au hata kuimarusha hicho kilimo lkn tatizo likawa soko.
Purchasing power ya watanzania ni ndogo, mishahara ya wafanyakazi ni midogo.
Nani leo mwalimu wa shule ya msingi au sekondari au hata police ataenda kufanya shooping supermarket?

Kwa mshahara wa laki 6, ambapo inakubidi ulipe kodi, umeme, maji, usafuri,ada za watoto kwenda shule, chakula, watoto hawajavaa.

Tuache masihara, tukitaka viwanda tushushe riba za mikopo benk, tuongeze mishahara.
Leo unataka kiwanda cha viatu wakati unanunua kiatu kimoja unavaa mwaka mzima, hapo kiwanda kinafanya biashara kweli?
umeongea point kubwa sana. purchasing power ya watanzania ni ndogo sababu ya serikali kuwanyonya. imekuwa ikiwapangia bei wakulima na kuwakataza kuuza mazao yao nje ya nchi. kwa kisingizio njaa itaibuka. fikiria DRC kilo ya mchele ni Tsh 6,000. unadhani ni pesa ngapi tungepata watu wangeruhusiwa kuuza huko? watu wangapi wangeanza kulima kwa bei hiyo? hali iko hivyo kwenye viazi, maharage, mahindi nk.

nchi nyingi zinapoanzisha viwanda lengo la kwanza inakuwa import substitution. hili haliwezekani ikiwa wananchi ni masikini. serikali inabidi kwanza kuhakikisha kilimo chetu kinalipa.tutoe ujamaa.
 
Nnaona hata hauelewi ni nini maana ya utajiri wa cubic feet trillion 60 za gas aliotuwachia Kikwete.

Tumpongeze na tuongelee viwanda vya matrillioni kwa sasa, si hivyo vi billioni ushuzi.
Ya Kikwete ni mavi ya kale tunazungumzia ya Ngosha,viwanda vyake na ya bajeti yake.
Aghalabu uchumi wa gesi si wa leo ni mpango utakao chukua muda mrefu. Uwekezaji wa mafuta na gesi duniani kwa sasa umeshuka tokana na kuporomoka kwa bei na mahitaji
Saum njema
NB; Israel,Msumbiji na Indonesia pia wamegundua gesi nyingi hivyo kwa sasa kwenye soko la dunia gesi si dili kihivyo
 
Kwa kuongezea ili tuwe na tz ya viwanda serikali lazima iwarahasishie mazingira wjwekezaji na wafanyabiashara,na sio kuwawekea mazingira magumu kulazimisha makodi makubwa makubwa n.k kwa mfano lets say unamfanya biashara anaegza tissue,au toothpaste au vijiti vya meno matani kwa matani toka nje,gvt inaweza kumhamasisha mfanyabiashara huyu kutengeneza kiwanda hcho hapa tz,lakini as businesses man lazima ajihakikishie faida,so serikali yenyewe ijikite ktk kutengeneza mazingra hayo. Na pia serikali iongeze purchasing power ya wananchi ili market iwepo kwa kuwafanya wananchi wawe na kipato,cha mwisho ni miundombinu lazima iwe ya uhakika,ports,harbor,road and railway zote ziwe za kisasa na zisiwe obstacles za kipuuzi ili kurahisisha mvt ya product na material
Kabisa Mkuu!
 
Iyo #5 ilipasa iwe #1 kwani kabla ya hayo yote elimu ndio msingi wa yote watu kwanza wasomeshwe falsafa za kidunia kama ni Ujamaa, Ubepari au Uislamu kisha wapime ni nini washike kwa sababu watu ndio walengwa hao ndi wahujumu uchumi na itikadi. Viwanda sio lazima awamu ya jpm hata miaka 1000 ijayo sio mbaya. Ndio ukaona mataifa ya dunia yamefika pale. Tatizo watu wanataka viwanda na mtu anufaike papo kwa papo.
Nakubaliana na wewe Mkuu!
 
Ya Kikwete ni mavi ya kale tunazungumzia ya Ngosha,viwanda vyake na ya bajeti yake.
Aghalabu uchumi wa gesi si wa leo ni mpango utakao chukua muda mrefu. Uwekezaji wa mafuta na gesi duniani kwa sasa umeshuka tokana na kuporomoka kwa bei na mahitaji
Saum njema
NB; Israel,Msumbiji na Indonesia pia wamegundua gesi nyingi hivyo kwa sasa kwenye soko la dunia gesi si dili kihivyo

Si wa leo? Umelala kweli wewe, tena usingizi wa pono.

Huna habari kuwa Kinyerezi 1, 2, 3 na 4 zinatumia gas, na 1 ni leo hii? Au ulifikiri viwanda utaviendesha kwa kuni?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Tukifikiria kujenga viwanda kama enzi za Nyerere vitakufa kama vilivyokufa vya Nyerere na alivyotaifisha, vilikufa kabla yake, akiviona vinamfia.

Ni kuwawezesha tu wawekezaji, mfano mzuri na uliofanikiwa na kuleta tija ya haraka ni wa Mahathir Muhammad wa Malaysia.

Serikali iwe facilitator tu na isijiingize kwenye uendeshaji wa kila siku wa kiwanda chochote na wala tusisikie neno "kiwanda cha umma", ni ujinga ulioshindwa.

Tunahitaji nishati ya kutosha kwanza. Viwanda vya sasa vitaanzishwa na wenye nia ya kukamata masoko tokana na mahitaji. Serikali inaweka sera halafu private sector na waliomo ndio wachangamkie hizo fursa. Lazima watakaoanzisha viwanda walindwe...huwezi kuanzisha kiwanda hapa halafu bidhaa hiyo hiyo inaagizwa toka nje, chini ya kiwango na bila kulipiwa kodi ukasema utashindana nayo
 
imeshakuwa rasmi kwamba sera ya awamu hii ni viwanda. sera hii ikifeli tunaumia sote, pia ikifaulu tunafaidika sote. hivyo kama wadau tuchangiane mawazo kuhakikisha inafanikiwa. tuangalie ni changamoto gani tunakabili kuelekea uchumi wa viwanda? ninini suluhisho la changamoto hizo? majukumu serikali itimize? majukumu ya sekta binafsi? . viwanda gani tuvipe kipaumbele? unafikiri kiwanda kipi kinatakiwa kujengwa wapi?

Where no counsel is, the people fall, but in the multitude of counselors there is safety - Mossad
Its very simple.
Tumbua MAJIPU, funga midomo watanganyika, elekeza TV cameras zote kwako zikusifie kama kamuungu basi.
Viwanda vitakuja waaaaaa
 
Tunahitaji nishati ya kutosha kwanza. Viwanda vya sasa vitaanzishwa na wenye nia ya kukamata masoko tokana na mahitaji. Serikali inaweka sera halafu private sector na waliomo ndio wachangamkie hizo fursa. Lazima watakaoanzisha viwanda walindwe...huwezi kuanzisha kiwanda hapa halafu bidhaa hiyo hiyo inaagizwa toka nje, chini ya kiwango na bila kulipiwa kodi ukasema utashindana nayo
Umesahau Kinyerezi l, II, III na IV alizotuwachia Kikwete? Bila kusahau liganga na Mchuchuma.

Oops, na gas cubic feet trillion 60, nazo kwako si nishati?
 
Mimi naona waanze na uzalishaji wa nuclear tuanze na umeme wa nuclear ambao warusi walisema wako tayari kutupa tecnolgia baada ya hapo tutapata umeme wa kutosha then tutaanza hata kupamp maji kutoka ziwa victoria na ziwa tanyanyika ziwa rukwa na vyazo vingine kwa ajili ya umwagiliaji na matumizi ya mwananchi. Hapo viwanda vitapata umeme wa kutosha hata kisafisha madini na kuzalisha vitu vingine. Nje ya hapo sijui. .......
 
Umesahau Kinyerezi l, II, III na IV alizotuwachia Kikwete? Bila kusahau liganga na Mchuchuma.

Tuongee fact...Kinyerezi I imeanza lini kutoa hizo 150MW? Kinyerezi II JPM ameizindua baada ya kutoa hela ambayo haikutolewa wakati wa JK...Kinyerezi III sijasikia ilianza lini...Liganga na Mchuchuma zipo toka awamu ya kwanza. Tayari zimeshaanza kufanya kazi?

Nafikiri tupunguze maneno mengi..tufanye kwa mifano. Tanzania kama iliweza kusaidia ukombozi wa karibu nchi zote za kusini mwa Africa ikiamua kuukomalia uchumi wake itaubadili chini ya miaka 10...tukaongoza mbali tu
 
Mimi kwakweli ningependa Serikali iondokane kabisa na kujihusisha na mambo ya kujenga viwanda. Yenyewe ikaae katika kutunga sera na kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji huku ikiwapa nguvu wawekezaji wa ndani.

Nadhani Uwekezaji katika Sayansi na Technolojia umeshaulika kiaina. Lakini tukiwekeza kwenye Sayansi na kuwapa uhuru wagunduzi halafu wakawekewa mazingira mazuri itatufanya tusonge mbele kwa haraka.

Vilevile kuhamasisha wawekezaji wa ndani na kuwatafutia mikopo kwa ajiri ya kujenga viwanda.
Lakini kwa kuanza kabisa tungejenga viwanda vya kusindika mazao na baada ya kujenga hivyo viwanda vya kusindika mazao ndio sasa tunaweza kuhamasisha kilimo chenye tija.

Mimi napinga vikali kuanza kusisitia kilimo kabla ya kujenga viwanda, ni bora wakati tunajenga viwanda vya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi watu wakawa wanapatiwa elimu ya kilimo bora na chenye tija. Na baada ya viwanda kujengwa tayari watu wapo na ujuzi wa kulima, kuvua na kufuga kwa tija huku wakiwa na uhakika wa mazao yao kununuliwa.

Huwezi ukaniambia nilime ekari 100 za machungwa wakati sijui hayo machungwa yataenda wapi.
 
Mimi naona waanze na uzalishaji wa nuclear tuanze na umeme wa nuclear ambao warusi walisema wako tayari kutupa tecnolgia baada ya hapo tutapata umeme wa kutosha then tutaanza hata kupamp maji kutoka ziwa victoria na ziwa tanyanyika ziwa rukwa na vyazo vingine kwa ajili ya umwagiliaji na mayumizi ya mwananchi. Hapo viwanda vitapata umeme wa kutosha hata kisafisha madini na kuzalisha vitu vingine. Nje ya hapo sijui. .......
hata coal mkuu. China zaidi ya 50% ya umeme wao ni wa makaa.
 
Mkuu Annael
Nani utamwambia ajenge kiwanda cha kusindika machungwa wakati hajui machungwa atayapata wapi!!!

Malighafi ikiwa nyingi sokon viwanda huja automatically.

Tanzania kilimo chetu ni kwa ajili ya mahitaji yetu ya chakula na pia pamoja na hivyo bado pia tunacholima hakitoshelezi.

Kilimo kwanza vingine hufuataa automatic
 
Suala la msingi ni Rais kuboresha riba katika benk, kuna vijana kibao wanaotoka vyuon wana idea nzuri lkn tatizo ni mtaji, au mikopo na mikopo huwa na riba kubwaa.

Rais arekebishe mishahara ya wafanyakazi, aondoe kodi ambazo sio za lazima ambazo zinamnyonya mkulima.
 
Back
Top Bottom