Tujadili hili limekaaje

odamae

Senior Member
Nov 5, 2020
163
291
Yani Mimi mama angu amenikwaza sana anatupelekaje Mimi na mdogo angu course moja? Alafu uhasibu level ya diploma naona kama ni kukosa mawazo ya kuamua vitu bila kufikilia fani yenyewe haina ajira alafu wote tunasoma the same kozi!

Hii kwangu haijakaa poa japo imeshatokea lengo lake sijui lilikuwa nini tulimshauri dogo asome kozi nyingine aling'ang'ania mama dogo asome uhasibu mpaka anasoma! Hii italeta ushindani wa maisha bora kila mtu angesoma kozi yake alafu kingine inaleta dharau na kutoheshimiana.

Sasa dogo performance yake sio nzuri kabisa yani sijui itakuje....kichwa kizito tangu kitambo tulitaka asome kozi simple ambazo sio complicated lakini mama akakaza. Course work anazopata mi sijawahi kupata tangu nianze chuo yani course work zake za chini sana 28, 30 sasa sijui kama atachomoa.
 
Pole aisee.... jaribuni kuongea na mama upya japo yeye ndio analipa ada ila anahitaji ushauri tumieni hata rafiki yake/mtu mwenye ushawishi amueleze hali halisi ya mtaa

NB: Ila jukwaa umebugi
 
Kajadili wewe mama yako na ndugu yako..

Kama kila kitu mama yenu ndo anaamua basi ..bado hamjakua...
Bado kuwachagulia na wachumba tu
 
Unataka watu wajadili nn, mmoja wenu aa he masomo ana unatumbia kwamba wewe una akili zaidi ya mdogo wako???
 
Yani Mimi mama angu amenikwaza sana anatupelekaje Mimi na mdogo angu course moja? Alafu uhasibu level ya diploma naona kama ni kukosa mawazo ya kuamua vitu bila kufikilia fani yenyewe haina ajira alafu wote tunasoma the same kozi!

Hii kwangu haijakaa poa japo imeshatokea lengo lake sijui lilikuwa nini tulimshauri dogo asome kozi nyingine aling'ang'ania mama dogo asome uhasibu mpaka anasoma! Hii italeta ushindani wa maisha bora kila mtu angesoma kozi yake alafu kingine inaleta dharau na kutoheshimiana.

Sasa dogo performance yake sio nzuri kabisa yani sijui itakuje....kichwa kizito tangu kitambo tulitaka asome kozi simple ambazo sio complicated lakini mama akakaza. Course work anazopata mi sijawahi kupata tangu nianze chuo yani course work zake za chini sana 28, 30 sasa sijui kama atachomoa.
Bado hujakua.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom