Tujadili: Dunia ya machale!!!!!!!!

Kongosho ni kweli, maisha hayawezi kwenda bila imani? Simaanishi mambo ya Mungu.
Na Eiyer, unasemaje; ninahitaji kuearn trust yako kwanza ndipo unitrust au unaweza kunitrust kwakuwa sijakupa sababu bado za kutonitrust?
 
Last edited by a moderator:

cc vijana wa kingoni,,,,,,
 
Kongosho ni kweli, maisha hayawezi kwenda bila imani? Simaanishi mambo ya Mungu.
Haya ni maneno yangu pia
Na Eiyer, unasemaje; ninahitaji kuearn trust yako kwanza ndipo unitrust au unaweza kunitrust kwakuwa sijakupa sababu bado za kutonitrust?
Hapana
Unachotakiwa ni kujifunza kuwaamini wengine
Naweza kukuamini sio kwasababu umeniambia hivyo ila kwakuwa wewe umejenga mazingira ya kuaminika

Imani hujengwa!
 
Kaunga ninavojua trust ni vurtue...na kama virtue nyingine, imeshakuwa eroded with time kutokana na muingiliano wa kitamaduni unaoshabihishwa na utandawazi.

Matokeo yake ndo kila kitu kwa machale......
 
Last edited by a moderator:
rafiki, huu ni uchokozi wa wazi kabisaaaaaa!
 
Kaunga ninavojua trust ni vurtue...na kama virtue nyingine, imeshakuwa eroded with time kutokana na muingiliano wa kitamaduni unaoshabihishwa na utandawazi.

Matokeo yake ndo kila kitu kwa machale......

Sikutegemea maoni tofauti especially kutoka kwako maana nakumbuka mchango wako kwa kamusi. Kwa maneno mengine unataka kuniambia machale ni silaha muhimu kwa zama hizi za muingiliano mkubwa wa kitamaduni? Lakini ni tamaduni zipi mfano zilizotuingilia ambazo zimetufanya tushindwe kuaminiana?

Mimi nisingelaumu sana tamaduni, rather ningelaumu ugumu wa maisha na ubinafsi wa kupindukia kama wadau karibu wote walivyochangia.
 
Last edited by a moderator:
Unaposema maisha hayawezi kwenda bila imani labda sijakuelewa, lakini kuna watu hawaamini wenzao na wanaishi kama kawaida.

Kuna mtu hata kuwa wapenzi tu, anakusainisha mkataba, ila ni dalili ya kutokuwa na imani na wewe. Lakini anaishi kama kawaida.


Labda useme kuwa maisha bila kuamini watu kadhaa yanachosha, kila saa inabidi uwe umejilinda.

Kongosho ni kweli, maisha hayawezi kwenda bila imani? Simaanishi mambo ya Mungu.
Na Eiyer, unasemaje; ninahitaji kuearn trust yako kwanza ndipo unitrust au unaweza kunitrust kwakuwa sijakupa sababu bado za kutonitrust?
 
Kaunga apo underline hebu nifafanulie bana sijaelewa....sredi ya kamusi naikumbuka...inahusiana na hii au umemuunda 'kaizer' wako wa namna flani


Hapo bold, ndicho ninachosema, kutokuwa mbinafsi pia ni virtue, na ugumu wa maisha unaletwa partly na aina ya mfumo wa maisha tuliouchukua kwa maana ya mfumo wa kibepari, unaowajali wachache kunufaika huku wengi wakielea kwenye lindi la umaskini (ugumu wa maisha)

So kwa mtazamo wangu kama tunalenga ile kuaminiana, huko kumepotea siku hizi sio kama zamani, enzi za mababu zetu
 
Last edited by a moderator:
Ukishaumwa nyoka ukiona mjusi lazima ushtuke.

Unaweza kumwamini mtu kumbe yeye ana lake jambo; likishakutokea jambo baya kwa sababu ya kumwamini mtu - inakuwa vigumu kuendelea kuwaamini wengine. Binafsi nilowahi kuyaona kwa umri huu ni mengi, hivyo kwa lolote inabidi kutanguliza uwazi mbele - ukishakuwa muwazi kwa mtu unayetaka kushirikiana naye kwa lolote lile - we unakuwa salama zaidi kwani kila kitu unakijengea mazingira ya kutoleta madhara mbeleni. Hapa maandishi ya makubaliano / mikataba iliyo wazi ni muhimu sana.
 
Unaposema maisha hayawezi kwenda bila imani labda sijakuelewa, lakini kuna watu hawaamini wenzao na wanaishi kama kawaida.

"Kuishi kama kawaida" maana yake nini?
 

Nafikiri Eiyer alimaanisha maisha yanakuwa magumu usipoamini watu, usipoamini huyu dreva atakufikisha salama kazini, usipoamini hayo maembe uliyonunua hayajadungwa sindano za sumu, usipoamini kuwa housegirl hajakojolea mkojo kwenye chai yako, usipoamini nyama choma uliyokula huenda ni nyama ya mbwa etc. Labda hii nimeexagerate lakini ofcourse as you said huwezi muamini kila mtu kwa baadhi ya mambo lakini you got to trust someone, awe mume, mke, dada, rafiki haijalishi. It is okay kuwa na siri walau moja au mbili lakini zile zisizo na madhara makubwa.
 
Last edited by a moderator:

Safi kabisa
Haya ndio nilikuwa namaanisha

Halafu sio maisha yatakuwa magumu bali hayataenda kabisa!
 

Kwenye uzi ule ulizungumzia umuhimu wa uaminifu kwa wana ndoa, ndio maana nikasema nilitegemea mchango unahamasiha uaminifu; au sivyo ulivyomaanisha kwenye post yako ya awali?

Na nimekuuliza pia kuwa machale ni remedy au silaha ya kujihami na kuvunjika kwa uaminifu? Sasa kila mtu akijihami hiyo familia itakuwaje au hayo maisha yatakuwaje au hiyo partnership katika biashara itakuwa vipi?
 

Umesema vyama, ila kuna uwazi pasipo uaminifu? Utaaminifu nimeweka wazi kila kitu? Kuna mikataba ambayo inakuwa na clauses ambazo ziko vague ili kuacha room ya mwingine kumzidi kete mwingine. Mimi nafikiri uaminifu ni kitu muhimu sana na it begins with you.
 
mi nafikiri watu wanaaminiana sana, wapo wengi tu wanaingia kwenye biashara bila hata makubaliano ya kimaandishi, hapo wanaongozwa na kuaminiana.
tuna wapenzi wetu na tunashiriki nao sex, ni imani hiyo mpaka kuoneshana viungo vyenu vya uzazi.
trust ipo sana sema tu kinachosumbua wengi ni hofu ya kutendwa lakini huwezi ukafanya yote hayo bado useme huwaamini watu wako.
 

Mh!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…