Tuitishe Uchaguzi Mkuu mapema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuitishe Uchaguzi Mkuu mapema?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 8, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kutakuwa na faida gani au hasara gani endapo tutaamua kuitisha uchaguzi mkuu mapema na hivyo kuondokana na mlolongo wa kashfa na watuhumiwa wa kashfa mbalimbali na hatimaye kuunda serikali mpya?

  Wakati serikali mbalimbali duniani zinapokabiliwa na tuhuma za ufisadi wa viongozi wake huwa zinalazimika kuitisha uchaguzi mpya kwanini na sisi tusiamue kuitisha uchaguzi mpya ili kuunda bunge jipya na hatimaye kupata timu mpya ya viongozi?

  Kwa mfano, Bunge likiamua kuikataa hii bajeti inayokuja kwa sababu x,y na hivyo kuonesha kukataa sera za serikali, je tutakuwa tayari kuitisha uchaguzi mkuu mapema?

  Je yawezekana tiba ya matatizo yetu kwa wakati huu ni kuamua tu kuanza moja na serikali mpya huku wale wote ambao wanatajwa kuhusishwa na ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kutokupewa nafasi na kuwekwa pembeni na vyama vyao?

  Kwa mfano, baada ya kashfa za matumizi ya fedha ambazo zinaikabili serikali ya Uingereza msukumo mkubwa upo kwa Waziri Mkuu Gordon Brown kujiuzulu na mawaziri wake kadhaa tayari wameamua kuachia ngazi. Na kuna uwezekano ni masaa tu kabla Brown mwenyewe hajaamua kujiuzulu ingawa inaonekana anapata kuungwa mkono kwa wakati huu na watu ndani ya chama chake.

  Je, serikali ilivyo sasa yaweza kujikuta inalazimishwa kujiuzulu siyo kwa sababu ya Kikwete ambaye bado anaungwa mkono na wananchi wengi bali kwa sababu ya mawaziri wake ambao ameendelea kuwang'ang'ania licha ya udhaifu mkubwa wa kiuongozi?

  Yawezekana kuitisha uchaguzi mkuu mapema unatunusuru na siasa za uchafu na kisasi ambazo zinaelekea kutawala tunapoelekea 2010. Kulisalimisha taifa letu na kuleta uongozi mpya ambao utakuwa na ajenda mpya (ila ya maisha bora imeshindwa) ndiyo njia pekee ya kurudisha heshima na mwelekeo wa ujenzi mpya wa taifa.

  Tuendelee kusubiri hadi 2010 kuanza upya, au tuamua kuanza upya mapema kwani inaruhusiwa kikatiba?
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes. Uitishwe sasa. Is too late. Ni kwa ajili kuondoa mafisadi wote
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Je tuki itisha uchaguzi sasa na watu wale wale wakarudi madarakani? Wenzetu wakiitisha uchaguzi katika hali hiyo hawa wachagui tena viongozi hao ila sisi utaitisha uchaguzi tena halafu watu wale wale wapigiwe kura tena. I don't think this will work for us.
   
 4. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapana, wakape kipaza sauti yaani MIC
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  MMKJJ,
  Kwanza hao wabunge watakaokaa, kwamfano, kuikataa hii bajeti inayokuja kwasababu zozote zile, wapo wapi, wakati wapo bize kubonyeza waongezewe mishahara!
  Tuondelee kuota tu lakini nchi hii....!!!
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tutakushtaki kwa uchochezi wewe.........lol
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Na kwa kuongezea tu ratiba ya bunge inaonyesha kuwa Waziri Mkullo atasoma bajeti yake siku moja baada ya Rais Kikwete kulihutubia bunge. Hotuba yake inaelezwa kuwa itakuwa na kila aina ya kuwapoza wabunge ambao wanaonekana kuwa moto na bajeti hiyo - ama uko au hauko nasi, period.

  Hapana Mwanakijiji, Bunge letu kuna wakati linakaa kama baraza la kuhalalisha uzembe, ufisadi na kutowajibika. Mambo yanapokuwa mazito, uCCM hupenyezwa kama vile rupia inavyopenyezwa kwenye udhia. Ni hapo makelele yao (their bluff) hunyamazishwa na thubutu kohozi lisikike.
  wamepikwa, wameiva - wana CCM haoo !

   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mnahela zakulipia uchaguzi... wazungu hawajapanga kuwapa hadi mwakani
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Thinking aloud is always healthy hata kama unayafikiria ni mambo ya kusadikika.
  Hata bajeti iwe mbaya kiasi gani, kwa CCM dorminated bunge, usitegemee muujiza wa kuunga mkono uondoshwaji wa shilingi bila kurudishwa. Kumbuka hoja ya kuondoa shilingi, haipigiwi kura ya simple majority, ile ya wanaokubali waseme ndiyo, ... ndiyooo..Wasiokubali waseme siyo..kimya!. Waliokubali wameshinda!.
  Hoja ya kuondoa shilingi inapigiwa kura kwa mbunge mmoja mmoja kuitwa kwa jina lake, kusimama na kuunga mkono ama kupinga.
  Bunge linatawaliwa na wabunge wa CCM wa aina 3. Wanye njaa, maoportunist na watumishi wachache wa wananchi.
  Hivi kweli unategemea wabunge wenye njaa na maoportunist watathubutu kuunga mkono hoja kama hii?!. wakale wapi?.
  Ndio maana wapenda demokrasia wakweli kote nchini wakiwemo wanaCCM wenyewe, wangependa kuona healthy opposition as the balance of power ili kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, wanaipiga chini serikali na kuanza moja.
  Tanzania hiyo ni ile ya hayati Shaaban Robert kwenye 'Kusadikika' na ndio naiona Tanzania iliyo kwenye macho ya Mzee Mwanakijijini kwenye mada hii.
  by the way, bakuli la uchaguzi mkuu 2010 limeishajaa, muda wowote kuanzia sasa serikali itatangaza ujazo wa bakuli hilo na kuwashukuru nchi wafadhili!.
   
 11. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Swali lipo hapa, ikilazimu kuwa hivyo, ni nani ataitisha uchaguzi huo? Halafu hivi uchaguzi 2010 umepangwa kuwepo October (as usual) au December (as per 5-year duration from previous election) ??
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani ni wakati muafaka tuitishe uchaguzi mpya oktoba mwaka huu kwa sababu sioni mwelekeo wa serikali ya JK. Ameshindwa kuonyesha kile wananchi tulicho kitarajia ambacho ni pamoja na kuwalinda wezi wa mali ya umma.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
 14. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKJJ,

  Nimewaza sana kuhusu Ka-inzi na safari yake. Nakatakia maisha mema na yenye fanaka. Kapitie kwangu "the rock city" walau kafungue kinywa.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa KATIBA hii na TUME hii ya UCHAGUZI na MAZINGIRA haya tuliomo, uchaguzi mpya hautatusaidia sana. Sio tu huo wa haraka bali hata wa 2010.
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pasco,YOU ARE TALKING!
   
 17. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  WildCard!

  Nakushukuru sana kwa kuliweka hilo wazi!! M.Mwanakijiji kwa katiba iliyopo hata tukifanya uchaguzi 2025 CCM watashinda cut my neck!!! Bila ya katiba mpya nasema mpya mimi siendi kupiga kura mpaka nife!! WaTZ walivyo wapuuzi hawawezi kuchambua kitu shit. Nadhani na nilishasema ng'ombe kwa asili yao they see everything green period!!

  Na Watanzania have been brainwashed kwa kuangalia moshi wa MWENGE unaokimbizwa mitaani kila mwaka nafikiri ni aina fulani ya dini ya kishetani na mimi sijawahi kufukuza mwenge normally I close my eyes and nose ! Niliuona labda 1968 au kabla sikumbuki!! Tanzanians can only see green colour just like ng'ombe!!!!

  UCHAGUZI AS PROPOSED BY MWANAKIJIJI IS A WASTE OF PUBLIC FUNDS BORA Muwalipe walimu mishahara Nasikia bunge ni fupi si zaidi ya mwezi hawana pesa!!!
   
 18. J

  Jafar JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nchi zifanyazo hilo huwa wamesema hivyo kupitia KATIBA yao. Halafu, sisi hatuna political maturity ya kutufikisha hapo, tunaongea sana vitendo vichache na siku zinaenda. Kwa wazo lako si baya ila nina hakika mafisi (kifupi cha mafisadi) watafanya kila liwalo ili serikali hii iendelee maana hawana uhakika wa timu itakayokuja, waliopo sasa wapo mikononi mwao. Kuthibitisha zaidi udhaifu wa serikali ya JK, Pinda aliwahi kusema bungeni kuwa mafisi haya yana nguvu nyingi za kipesa kiasi hata yeye aliogopa kuchukua hatua stahiki.

  Narudia, watanganyika hatuna ujasiri wa vitendo na hii national weakness mafisi wanaielewa sana.
   
 19. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni mawazo mazuri sana na ya kizalendo. Ni ukweli ulio wazi kwamba sasa nchi yetu inayumba sana hivi sasa. Wale wote wenye moyo wa kizalendo wachangie tuone ni jinsi gani tunaweza kuinusuru nchi yetu. Wanasheria tupeni maoni yenu kuhusu uwezekano wa kuitisha uchaguzi mapema. Tumechoka na ubabaishaji!
   
 20. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  MKJJ
  Ni hoja chokonozi ila bado watanzania wengi hatujaelewa umuhimu wa sanduku la kura..
  tuendelee kujifunza na kutafakari kwa mapana na makini umuhimu wa chaguzi zetu..

  there is a wind of change coming....
   
Loading...