Tuishi kwanza..harusi itafuata baadae!

Tuishi kwanza..harusi itafuata baadae!

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,190
^^
Naomba tujadiliane kwa mabinti ambao wamekutana na wanaume ambao hawako tayari kwa harusi au kuhalalisha ndoa.
Anakupenda sana lakini kwa sababu ambazo pengine ni za msingi au la! Hayuko tayari kwa harusi,,ndoto ambayo umeiota tangu utoto.
Lakini anakuambia "...tuishi kwanza,,harusi itafuata baadae"
Je,unamwelewa vipi mwanaume wa aina hiyo?

Harusi ni tafrija inayofanyika baada ya watu wawili kufunga ndoa. Bila shaka unamaanisha ndoa?
 
Yes,,kumekuwa na dhana ya wanawake kuona kuwa kuingia kwenye ndoa bila harusi,,hiyo si ndoa.
Unalichukuliaje
^^
 
Kwa upande fulani inasaidia kupimana; kiasi kwamba mambo yasipokuwa mazuri mnaweza kuachana bila kuwa na kiwingu kile cha "until death do you apart".

Tukirudi upande mwingine, ndoa/harusi ni nini zaidi ya mkataba? So Mkataba unakupa uhalali, unakupa insurance na mengine ingawa sio lazima upendo wa kweli. So kwa mdada, kupata uhalali basi ndoa ni muhimu; lakini je mkaka yeye hahitaji huo uhalali?
 
Asante Kaunga
Uhalali unahitajika kwa mwanaume pia lakini pengine mambo hayajawa sawa na anahitaji muda.
Je,inamvunja nia ya ndoa mwanamke ikiwa mwanaume atasimamia msimamo huo?
After all,,ndoa ni zaidi ya sherehe
^^
 
Last edited by a moderator:
Wazazi wetu walizaa kwanza halafu ndoa ilifuata
'
Wengine tumezishuhudia ndoa hizo tukiwa wakubwa!
 
Eiyer
Mtazamo wa dada zetu wanaona bila harusi hakuna ndoa?
Je inaweza kuwa sababu ya ndoa zilizofungwa kwa harusi za gharama kuvunjika mapema?
^^
 
Last edited by a moderator:
Kwa upande fulani inasaidia kupimana; kiasi kwamba mambo yasipokuwa mazuri mnaweza kuachana bila kuwa na kiwingu kile cha "until death do you apart".

Tukirudi upande mwingine, ndoa/harusi ni nini zaidi ya mkataba? So Mkataba unakupa uhalali, unakupa insurance na mengine ingawa sio lazima upendo wa kweli. So kwa mdada, kupata uhalali basi ndoa ni muhimu; lakini je mkaka yeye hahitaji huo uhalali?

Mm naona ni kukosa msimamo na kuto kujiamini juu ya mahusiano yao. Hainiingii akilini kushi bila ndoa mkiwa na mitazamo ama ya kuachana ama kuoana hapo baadae. Lakini kwa wale wenye nia moja ya kwamba tunaishi bila ndoa kwasababu zilizo nje ya uwezo wao at that particular time hao hakuna shida lkn niko kinyume na wale ambao wanaishi hivyo eti bado wanasomana tabia, kwakweli hawa hawako sahihi na hawajautambua utu wao
 
Binafsi nilikuwa na mawazo kama hayo kabla ya ndoa ila mchumba wangu alikataa na tukafunga ndoa vizuri tu. Tatizo ninaloliona hapa ni je huyo kijana kweli atatimiza hiyo ahadi au badae ataghairi??Pia sio desturi yetu sis waafrika kukubali kuishi na mtu kabla ya ndoa na jamii haiwezi kukuelewa. Cha muhimu hapa ni sisi kubadilika na kuwa na harusi fupi ambazo hazina gharama kubwa kama sasa.
 
Kaunga embu tofautisha bhana.....!

Harusi ni ile sherehe au tafrija
Ndoa ni lile tendo la kukutana mwanaume na mwanamke hapo ndo mmefunga ndoa:love: ....!

SASA JIULIZE UNA NDOA NGAPI .........................!
 
Aisee kwa mambo yalivyo sasa hivi na jinsi ambavyo wengine viapo vya ndoa tunavyovitake serious ni nzuri IMO kuishi japo hata kwa miezi kadhaa ili kuona kama tunaweza ku-co-exist. Sioni uhusiano wa UTU na kuchunguzana tabia kwa two mature adults ambao wamekulia katika mazingira tofauti na kuamua kutengeneza familia.
Zamani enzi za wazazi wetu (wangu walifunga ndoa 60s) ambapo wachumba walikuwa wanachunguzwa na familia nzima na wakati mwingine recommendation inatoka kwa family members.
Sasa hivi kwenye maisha ya kukimbizana na boarding schools kuanzia chekechea hata wazazi tu hawazijui vizuri tabia za watoto wao; swala la kuishi pamoja (at least hiyo ni njia rahisi ya kufahamu kama mwenzio ni kikojozi, au akikasirika anakuwaje etc) kabla ya BIG commitment ni muhimu.
 
Aisee kama ni hivyo hazipungui...God l cant even count....
 
Nyie watu wote mnaohangaika na mambo ya ndoa, mnahitaji kununua kitabu hiki. kinaeleza haki zilizopo katika ndoa either ndoa ya kudhaniwa ambayo watu wameishi kinyumba kwa kipindi walau miaka miwili bila kufunga ndoa, na ndoa zilizosajiliwa na kusherehekewa kwa dini zote hapa Tanzania. kitabu hiki tunakipandisha bei mwezi ujao toka alfu kumi hadi alfu kumi na tano. bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI au angalia hapa chini.

View attachment 103023
View attachment 103023
View attachment 103024View attachment 103024View attachment 103024View attachment 103024
 
Binafsi nilikuwa na mawazo kama hayo kabla ya ndoa ila mchumba wangu alikataa na tukafunga ndoa vizuri tu. Tatizo ninaloliona hapa ni je huyo kijana kweli atatimiza hiyo ahadi au badae ataghairi??Pia sio desturi yetu sis waafrika kukubali kuishi na mtu kabla ya ndoa na jamii haiwezi kukuelewa. Cha muhimu hapa ni sisi kubadilika na kuwa na harusi fupi ambazo hazina gharama kubwa kama sasa.

^^
Asante Nsuri
Lakini sherehe ya siku moja imeleta tofauti gani ktk maisha yako ya ndoa?
^^
 
Last edited by a moderator:
Aaaaaaaaaah Wapi! Umfuje fuje nani bila pete kidoleni!????????? Thubutu yakooo! Mtu unatumika mpaka unakuwa nyapu nyapu bila mkataba wala agano! Khaaaaaaa!

Hapo ukishaingizwa kingi la kuishi wote lazima UMUABUDU coz huna ujanja, akighairi kwisha kazi kwako!!!!!!!!!!

Mimi hata mwanaume alieishi na mtu kiaka 4 japo ndoa haikuwepo simtakiiiiiiiiii!

Mimi sipendi mambo ya kuona oana coz ni kuzibiana opportunity, na kuwekeana viwingu kwenye bright future ahead na kufanya future iwe soo predictable! Window for hope of landing major Romance down the life road is closed.

Ila pia mambo ya kuishi ishi na mtu anakufuja fuja, unachakaaa hatma yako huijui siyataki pia. Mambo unaishi kwenu au kwako mnakutana SPECIAL FO SPENDING SOME QUALITY TIME TOGETHER! Then baada ya hapo kila mtu stress anaipelekea familia yake. Mjini Hapa!
 
Aisee kwa mambo yalivyo sasa hivi na jinsi ambavyo wengine viapo vya ndoa tunavyovitake serious ni nzuri IMO kuishi japo hata kwa miezi kadhaa ili kuona kama tunaweza ku-co-exist. Sioni uhusiano wa UTU na kuchunguzana tabia kwa two mature adults ambao wamekulia katika mazingira tofauti na kuamua kutengeneza familia.
Zamani enzi za wazazi wetu (wangu walifunga ndoa 60s) ambapo wachumba walikuwa wanachunguzwa na familia nzima na wakati mwingine recommendation inatoka kwa family members.
Sasa hivi kwenye maisha ya kukimbizana na boarding schools kuanzia chekechea hata wazazi tu hawazijui vizuri tabia za watoto wao; swala la kuishi pamoja (at least hiyo ni njia rahisi ya kufahamu kama mwenzio ni kikojozi, au akikasirika anakuwaje etc) kabla ya BIG commitment ni muhimu.

Imagine kama ni ww umeishi na kijana kama 6month hivi halafu mnashindwana tabia, jamii itakuchukuliaje? baada ya hapo unatafuta mwingine ambae mtaoana hapo baadae nae unaishi nae miezi mitano mnasomana tabia kisha unagundua hafai. Unatafuta mwingine tena inakuwa mwendelezo..........endless.
 
Aaaaaaaaaah Wapi! Umfuje fuje nani bila pete kidoleni!????????? Thubutu yakooo! Mtu unatumika mpaka unakuwa nyapu nyapu bila mkataba wala agano! Khaaaaaaa!

Hapo ukishaingizwa kingi la kuishi wote lazima UMUABUDU coz huna ujanja, akighairi kwisha kazi kwako!!!!!!!!!!

Mimi hata mwanaume alieishi na mtu kiaka 4 japo ndoa haikuwepo simtakiiiiiiiiii!

Mimi sipendi mambo ya kuona oana coz ni kuzibiana opportunity, na kuwekeana viwingu kwenye bright future ahead na kufanya future iwe soo predictable! Window for hope of landing major Romance down the life road is closed.

Ila pia mambo ya kuishi ishi na mtu anakufuja fuja, unachakaaa hatma yako huijui siyataki pia. Mambo unaishi kwenu au kwako mnakutana SPECIAL FO SPENDING SOME QUALITY TIME TOGETHER! Then baada ya hapo kila mtu stress anaipelekea familia yake. Mjini Hapa!

^^
But lara 1 cheti cha ndoa hakikupi guarantee ya ndoa yenye furaha..i.e umemkataa mnae-match nae kwa kigezo cha kukunyima harusi tu.
Huoni kuwa wapo waliofanyiwa harusi za gharama lakini bado wanasota?
Cc. Heaven on earth Ablessed @FP @Cynithia Chriss
^^
 
Last edited by a moderator:
Imagine kama ni ww umeishi na kijana kama 6month hivi halafu mnashindwana tabia, jamii itakuchukuliaje? baada ya hapo unatafuta mwingine ambae mtaoana hapo baadae nae unaishi nae miezi mitano mnasomana tabia kisha unagundua hafai. Unatafuta mwingine tena inakuwa mwendelezo..........endless.

Hadi muamue kuishi pamoja maana yake mmekwenda mbali. Sio kila boyfriend ni wa kuishi naye pamoja. Halafu, kuna limit ya nini jamii inadictate katika maisha yako; kwa swala la mahusiano ya two mature people f.ck jamii, sijali kabisa. Nimeishi na mtu mmoja tu na kwa more than 3 years na the guy turns up to be no one abuser; na ninashukuru Mungu kwa kuahirisha mara kibao yeye kunitolea mahari na ninamshukuru Mama yangu kwa kuwa alikuja kunielewa mwishoni.

Anyway ni mitazamo tu, na hakuna mtazamo ambao utakugurantee usalama au happiness kwenye maswala ya mahusiano. So ni bora kufanya kile ambacho you are more comfortable na ulichoamua mwenyewe ili usiwe na mtu wa kumlaumu baadaye.
 
^^
Eiyer
Mtazamo wa dada zetu wanaona bila harusi hakuna ndoa?
Je inaweza kuwa sababu ya ndoa zilizofungwa kwa harusi za gharama kuvunjika mapema?
^^

Harusi za siku hizi ni za hovyo sana,wanapriotize harusi badala ya ndoa,wanataka sifa,ujinga ulioje!
 
Last edited by a moderator:
mwanaume yoyote atakae mwambia mwanamke hivyo ujue tayari kashamuona huyo mwanamke ni mdebwwedo na mpaka mwanaume anamwambia mwanamke hivyo basi huyo mwanamke kakaa kihasara hasara tuu
 
Back
Top Bottom