Tuikubalie DR Congo kujiunga na EAC?

Rwanda na Burundi wako ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini migogoro yao imetushinda Tanzania, Kenya na Uganda mpaka leo. Imetuletea gharama kubwa na upotezaji mwingi wa muda na rasilimali, unadhani Kongo ambayo ni nchi kubwa ndiyo tutaiweza ?
Rwanda na Burundi migogoro yao ilikuwa ya ndani ilihali Drc Mashariki migogoro yao ilichangiwa sana na nchi jirani (Rwanda na Uganda) hivyo itakuwa rahisi wao kupunguza mivutano huko Kivu.
 
Una uhakika kabisa na hichi ulichosema ?
 
Mkuu Red Giant nilitoa ahadi ya kurudi na sasa nimerudi na nitachangia kidogo juu ya hii mada ambayo ni muhimu kabisa. Nitatoa maoni kama Mwanasiasa, pia nitatoa maoni kama Mwansheria. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada:

Congo DRC isitengwe bali isiruhusiwe kuingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwasababu itaongeza changamoto ambazo tayari EAC inazo na imeshindwa kuzimaliza kwa muda mrefu. Changamoto kubwa ni hii ifuatayo hapa chini:

Mosi, nchi wanachama wa EAC wanakumbwa na matatizo ya kisiasa ndani ya nchi zao ambayo kwa namna moja au nyingine yameugharimu huu ukanda muda na rasilimali nyingi ambazo zingewekezwa katika kufanya mambo ya msingi.

Uganda mpaka leo wanapigana na waasi wa Lord's Resistance Army wa Bwana Joseph Konyi. Upande wa pili kuna sintofahamu kubwa sana kwenye siasa zake za ndani na hatufahamu nini kitatokea nchini humo baada ya Raisi Museveni kutoka. Tunaweza kuhisi kwamba Uganda iko salama lakini kumbuka tangu nchi hiyo inapata uhuru hakujawahi kuwa na Raisi ambaye hajatoka kwa vimbwanga na kusababisha kuchafuka kwa hali ya kisiasa nchini humo kuanzia Mutesa hadi Obote.

Rwanda nayo mpaka sasa iko kwenye vita isiyoisha na makundi ya waasi wa Kihutu ambao wako Congo DRC na duniani kote. Hivi karibuni siasa ya Rwanda imegubikwa na kiza kikali baada ya kusemekana kwamba kuna Watutsi ambao waliwahi kuwa ndani ya Serikali ya Raisi Paul Kagame wameunda mtandao mkubwa wa kutaka kumpindua. Rwanda kama nchi inaenda vizuri kwasasa lakini bado kuna sintofahamu kubwa kama Uganda ambako mpaka leo hawana uhakika na Smooth Transition of Power after the fall of their strongmen.

Burundi mpaka sasa unafahamu nini kimekuwa kinaendelea tokea mwaka 2015, na bado nako kuna sintofahamu kubwa sana na Serikali ya Raisi Nkurunzinza iko nje-ndani.

Tanzania na Kenya hazijatofautiani sana. Zimefanikiwa sana kwenye suala la Smooth Transition of Power hivyo kufanikiwa kukwepa sintofahamu nyingi za kisiasa ambazo zimewakuta mataifa ya jirani. Japo upande wa pili bado Kenya ina changamoto kubwa za kiusalama ambazo zimemfanya apoteze rasilimali nyingi sana kule Somalia akipambana na kikundi cha Al Shabaab huku Tanzania ikiwa inapita kwenye kipindi kigumu kisiasa ambacho pia kinaweza kuzaa sintofahamu kubwa sana huko mbeleni kama siasa yake itaendelea kwenye njia hii.

Ninachotaka kusema kwenye hoja hii ni hiki hapa: EAC iliundwa kama Jumuiya ya kiuchumi na siyo ya kisiasa. Haya ya siasa kama kuunda shirikisho ni malengo ya baadae sana (Future Objectives) ambayo hayatakiwi kuwa kwenye ajenda yoyote kwenye kipindi hiki.

Lengo kuu na ajenda ya sasa (Main and Primary Objective) inabidi iwe ni Uchumi kupitia soko la pamoja na sarafu moja. Kama tukifanikiwa kujenga uchumi wa pamoja basi ndiyo mambo ya siasa yaanze kuingia kwenye ajenda za vikao vyetu. Sasa machafuko ya kisiasa huwa yanatutoa kwenye mstari maana hutulazimisha kuacha kufanya mambo ya kiuchumi na kujiingiza kwenye siasa, kitu ambacho siyo lengo letu kama EAC kwasasa.

Tokea EAC iundwe tumekuwa tukitatua matatizo ya kisiasa yanayogharimu rasilimali nyingi kuliko kufanya mambo muhimu: Tunalazimika kufanya hivyo kwasababu ni majirani zetu lakini haswa kwasababu ni wanajumuiya wenzetu. Tulianza na Kenya mwaka 2007-2008: Kenya na Alshabaab 2012:Tukaja Rwanda na Tanzania mwaka 2013: Burundi mwaka 2015: Uganda na Rwanda 2019. Sasa tukiileta DRC na ilivyo na matatizo lukuki basi fahamu kwamba tutabeba na changamoto zao kuanzia uchaguzi hadi waasi wa Kagame na Museveni.

Pili, Congo DRC kama nchi imeshaigharimu SADC ambayo ilijiunga mwaka 1997 punde tu baada ya kumtoa Mobutu Sese Seko madarakani. SADC ilijikuta inatumia muda mwingi sana kushughulika na CONGO DRC badala ya kujikita kufanya mambo ya msingi. Ikumbukwe Mzee Kabila alivutana sana na viongozi wenzake wa SADC pale alipotaka wamsaidie kupambana kwenye The Congo War lakini wakawa wanasuasua. Wakina Quett Masire wanataka kumsuluhisha, yeye Kabila akawa anasusia vikao. Unadhani nchi kama hii ikijiunga na EAC na ikapatwa na tatizo tutakwepa kweli kuhusika ???

Tatu, wengi tunatamani Congo DRC ijiunge EAC kwasababu ya rasilimali zake. Basi kama itajiunga na EAC itageuzwa rasmi kuwa kichaka cha mashindano ya wizi wa rasilimali (Mineral Race) zake baina ya nchi wanachama wa EAC. Mfano hai tu, Umoja wa Mataifa (UN) waliwahi kutoa taarifa ya uchunguzi kwamba kipindi cha Vita ya Congo Zimbabwe ilipewa na serikali ya Laurent Kabila malipo ya dola za Kimarekani Bilioni 5 ambazo zimetoka kwenye hazina ya mali mbalimbali za watu wa Congo DRC. Haya malipo yalienda sambamba na mikataba ya madini na mafuta ambayo Zimbabwe na Angola waliipata kwa kumsaidia Kabila.

Upande mwingine inasemekana mataifa ya nje yalifanya ujangiri na kuua zaidi ya tembo 12,000 kwenye mbuga ya Garamba. Umoja wa Mataifa uliilaani Rwanda na Uganda kwa kuiba maelfu ya rasilimali za watu wa Congo DRC kwa kisingizio cha kupigana na waasi.

Sasa hii ilikuwa miaka ya 1999-2003, unadhani DRC ikijiunga rasmi na EAC Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda watakaa tu kuziangalia zile rasilimali ??? Utatokea mvutano mkubwa sana baina yetu kuanzia kwenye uchaguzi wa DRC maana kila nchi mwanachama atataka aweke kwenye serikali mtu ambaye atakuwa na ushawishi mkubwa sana kwake: Rwanda na Uganda pamoja na uswahiba wao mkubwa walishawahi kupigana kisa kugombania rasilimali za Congo DRC. Sasa Congo DRC ijiunge na EAC hapo wakaongezeka Tanzania na Kenya unadhani kutakuwa na utulivu ???

Mfano mwingine ,angalia kilichotokea Burundi mwaka 2015 pale ambapo Tanzania na Rwanda walipogombania ushawishi kwa serikali ya Bujumbura. Sasa piga picha Burundi alikuwa hana utajiri wowote ule, unadhani Congo mwenye utajiri atatuacha salama ???

Sisi Tanzania tuna utajiri mkubwa ambao Mungu ametupa na itakuwa ni ujinga kama tutataka Congo DRC iinge EAC kwasababu ya utajiri wake. Japo kimkakati (Strategically)ni jambo sahihi, lakini tatizo linakuja kwamba pale ambapo hatuna mpango maalumu wa nini tutafanya na Congo DRC baada ya kuwa karibu na sisi. Hivyo tuiache tu na tusitafute matatizo yasiyo na ulazima wowote ule: Pia tusichume dhambi with this Imperialistic Mindset....

NINI KIFANYIKE KUHUSU CONGO DRC?

Hapa nitatoa maoni kama mwanasiasa:
Mosi, EAC ijikite kwenye kuimarisha taasisi zake yenyewe (Consolidation and Amalgmation of it's Institutions) na siyo kujitanua (Enlargement of the bloc) kwa kutafuta au kuruhusu wanachama wapya.

EAC imeiga vitu vingi kutoka European Union (EU) ambayo zamani ilikuwa ni European Economic Community (EEC) lakini haifanyi vizuri kama ambavyo EEC ilifanya. Umoja wa Ulaya ulianza kama Umoja wa Uchumi (Economic Union) na siyo Umoja wa Kisiasa (Political Union), lakini baadae ndiyo ukafika hapa ulipo. Ulipitia hatua mbalimbali.

Ulianza kutengeneza kitu kinachoitwa The European Coal and Steel Community mwaka 1951 ambayo ilikuwa ni taasisi iliyoundwa kwa lengo la kuhakikisha makaa ya mawe na chuma vinasimamiwa na Chombo/Taasisi moja ya kimataifa inayojitegemea ili kuzuia mvutano baina ya nchi kubwa kama Ujerumani na Ufaransa ambao ulipelekea kutokea vita vya kwanza na vya pili vya dunia.

Aliyesuka huu mpango anaitwa Jean Monet ambaye alisema ili tuweze kujenga umoja imara ni lazima tuhakikishe mataifa yenye nguvu na rasilimali nyingi ya Ujerumani na Ufaransa yanaungwanishwa kiuchumi kiasi kwamba nchi yeyote haiwezi kufikiria kwenda vitani na mwenzake. Kweli walifanikiwa sana maana mkataba huu ulisainiwa na mataifa sita (Ujerumani Magharibi, Ufaransa, Italia, Ubelgiji na Luxembourg) hata yale ambayo yalikuwa hayana rasilimali kama Ubelgiji na Luxembourg walinufaika.

Mwaka 1957 wakasaini mkata wa kuunda taasisi nyingine iitwayo The European Atomic Energy Community ambayo kazi yake ilikuwa kuzimamia uzalisha wa nishati ya nyuklia Ulaya ili kuwasaidia wanachama kupunguza utegemezi kwenye mafuta, pia kuuza nishati ya akiba kwa mataifa yasiyo wanachama. Hili nalo walifanikiwa sana.

Mwaka 1957 wakatengeneza sasa Umoja wa Uchumi wa Ulaya ambao leo ndiyo Umoja wa Ulaya. Lakini hawakuwa na haraka na hili liliwezekana kwasababu wao walikuwa na hali nzuri ya kisiasa nchini mwao. Mwaka 1967 taasisi za European Economic Community, European Steel and Coal Community na European Atomic Energy Community ziliungwanishwa kuwa chombo kimoja. Biashara baina ya nchi wanachama ilikuwa kwa asilima 28.4% hadi kuwashangaza Muingereza na Marekani.

Hawakukimbilia kujitanua bali walijijenga kwanza wao kiuchumi na kisiasa kabla ya kuhakikisha wanayakaribisha mataifa mengine kama Uingereza mwaka 1973. Japo wanafanya vizuri lakini bado wana matatizo sana, Raisi wa Ufaransa Charles De Gaulle miaka ya 1969 hakupenda Uingereza ijiunge na EEC kwasababu alisema italeta matatizo kwenye jumuiya hivyo alipinga sana hadi anafariki.

Uingereza aliruhusiwa kujiunga baada ya De Gaulle kufariki. Lakini mbali na yote yale siasa za Uingereza zimeutikisa Umoja wa Ulaya kama ambavyo De Gaulle alionya akisema Muingereza anawakilisha maslahi ya Marekani. Sasa Uingereza taifa lililoendelea sana kuliko Congo DRC matatizo yake ya ndani yamevuruga Umoja wa Ulaya unadhani ni busara kuleta tena mgeni ???

Hapa hoja yangu ni hii: Kichwa na Moyo wa EAC ni Kenya na Tanzania wala siyo rasilimali za Congo DRC. Kama tunataka EAC imara basi ni lazima tuhakikishe Kenya na Tanzania zinaelewana na kuzungumza lugha moja. Maana binafsi naamini ushawishi wa Kenya na Tanzania wakiwa wanaongea lugha moja ni hatari kuliko mlipuko wa bomu la kiatomiki na hakuna taifa la Afrika linaweza kuwashinda. Raisi Kwame Nkhuruma alilifahamu vizuri hili suala ndiyo maana alipinga sana EAC isiwe nchi moja.

Kenya na Tanzania wakiungana basi lazima Uganda, Rwanda na Burundi watafuata tu. Kenya na Tanzania zina Uchumi mkubwa, ushawishi mkubwa sana kikanda na kimataifa, zimekaa pazuri sana kijiografia, zina rasilimali nyingi na zina watu wengi wanaozungumza lugha moja ya Kiswahili. Wakenya na Watanzania hawapatani kwasababu wamefanana mno tabia, fanya uchunguzi utaligundua hili.

Mtifuano wa kiuchumi na kihistoria baina ya Kenya na Tanzania ndiyo unavuruga EAC. Tunafanyiana hujuma badala ya kuunganisha nguvu za kitaasisi ili tujikwamue hapa tulipo. Hujuma kwenye kilimo, hujuma kwenye bandari na hujuma kwenye viwanda bila kufahamu kwamba Afrika Mashariki yote tunaweza kuwa Mamlaka moja ya Bandari ambayo ingetusaidia sana.

AU tungeweza kuanzisha Joint Venture Agreement kupitia Special Purpose Vehicle kwenye kuratibu biashara ya Usafiri wa anga. AU tukaunganisha nguvu kwenye tafiti za Uchimbaji wa mafuta na gesi (SPV) mbona tungefika mbali sana tu. Wazungu walitwangana ndiyo wakapata akili kwamba kumbe tunaweza kushirikiana bila mabomu na vifaru.

Lakini sisi tunataka kushindana kisa kulipizana visasi vya ugomvi wa Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere. Leo hii kwa mitandao ya kibiashara ambayo Kenya na Tanzania tunayo kupitia nguvu za diplomasia za nchi zetu kama tukishirikiana sauti yetu itafika hadi mwisho wa dunia. Nashangaa kwanini hatulioni hili. Binafsi Kenya and Tanzania are the Key, ndiyo maana hata Rwanda, Burundi na Uganda walipovutana hakikutokea kitu kikubwa sana: Lakini Kenyatta na Jakaya walipovutana EAC iliyumba. Hujiulizi kwanini ???

Pili, na mwisho kabisa natoa ushauri kama mwanasheria sasa: Congo DRC asiwe mwanachama ila aidha apewe nafasi ya mtazamaji (Observer Status) kwanza ndani ya EAC huku akijifunza mwenendo mzima wa EAC. Sambamba na hilo EAC tunaweza kusaini mkataba maalumu na Congo DRC (Sui-Generis Treaty) ambao utampa nafasi ya kipekee kunufaika kiuchumi bila kuwa mwanachama. Anaweza akaandaliwa vipengele (Extracts Clauses with Limitations ) kutoka mikataba mbalimbali (Protocols) ambayo EAC ameshasaini. Anaweza kufanya kama ambavyo Uingereza na Umoja wa Ulaya walifanya miaka ya 1960's- 1970's au ambavyo wanataka kufanya baada ya Brexit.

Tujijenge kwanza sisi ndiyo turuhusu waliovurugwa kama Congo DRC wajiunge.
Tutaunda jumuiya zikipandana tu na kuacha lengo la kuifanya Afrika ijitegemee, mfano ; KENYA imo COMESA, EAC na IGAD, utitiri wa jumuiya, ilikuwa Afrika iwe na blok Kama 4/5 hivi, zenye malengo ya kuweka mambo sawa ili kishajiisha maendeleo baina ya nchi za kiafrika ila huu utitiri ni uoza mtupu !!! Maoni yangu
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kwenye nchi changa zenye Uchumi mdogo kama zetu kupandanisha uanachama wa Jumuiya mbalimbali (Overlapping Membership) ni janga ambalo linazuia nchi wanachama kutimiza vizuri malengo ya baadhi ya Jumuiya.
 
Wadau wamechangia hoja nzito kwenye mada hii. Nami nimeona pia nichangie.

Kwanza, DRC kujiunga na EAC siojambo ambalo nilitarijia hivi karibuni hivyo basi ni mshangao mzuri kusikia kuwa DRC wanataka kijiunga na Jumuiya. Ukitazama vizuri siasa za Afrika Mashariki na kati na historia ya ukanda huu utakubaliana kuwa ni milima miwili peke yake ambayo haiwezi kukutana au kuungana haswa tangu mabadiliko ya uogozi katika nchi za Jumuiya na DRC.

Pili, sitaki kurudia hoja zilizowasilishwa awali kwenye uzi huu ila nigependa kuongezea mkondo mwingine kulingana na mtazamo wangu utakao egemea zaidi idadai ya watu na uchunguzi wa ramani ya Afrika ya Mashariki na kati.

Ni kweli kuwa DR Congo yapo madini mengi na ya dhamani ya juu sana ulimwenguni inayofanya dunia mzima kuitamania kwa ulafi mwingi hadi kunao waliotaka kuwangamiza WaCongo kwa miaka mingi tangu enzi ukoloni mpaka leo. Lakini hii haifai kuwa kigezo kikuu kwa kuwakubalia DR Congo kuingia katika Jumuiya.

Wala kutokuwa na amani na usalama dhabiti kwenye DR Congo kuwa kigezo kiku cha kuwakatalia au kuwaweka pembeni wakati huu wanapotaka kujiunga na Jumuiya.

Ukichunguza ramani ya eneo la Africa Mashariki na Kati sana sana kwa mtazamo wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, ni rahisi kwa wadau kuona vile DRC ni muhimu sana kimkakati (very important strategically) kwa sababu hio ndio njia fupi na rahisi kwa zote kuunganisha Bahari ya Hindi na Bahari ya Atlantik. Kumbuka wengi wame changia kuwa kigezo kikuu kinapaswa kuwa uchumi kwa hivyo kukiwa na miundo msingi ya barabara, reli na mawasiliano unao unganisha nchi hizi za Jumuiya, DRC na Bahari hizi mbili kutaweza kurahisisha kufanya biashara kwa eneo hili. Hii ndio sababu kuu nilisema hapo juu kuwa DRC kutaka kujiunga ilikuwa mshangao mzuri sana kwani ukingalia USA ilivyoundwa nikuwa ililetwa pamoja na vita vikuu moja wapo ya hiyo ni vita vya kunyakua maeneo kuenda magharibi mwa bara la Marekani kaskazini ili USA iweze kuenea kutoka Bahari ya Atlantic hadi Bahari ya Pacific kupitia California. Hapa Africa tunaona kuwa DRC inajileta yenyewe kutokana na hamu yake bila kushuritishwa.

DRC kujiunga na Jumuiya italeta faida ya kiuchumi katika sekta mingi sio kwa rasilimali ya madini tu. Hiyo idadi ya watu milioni themanini na tano ina uwezo mkubwa kukiwa na amani na usalama kwa mfano katika sekta ya elimu, ukulima na ufugaji na hata soko la bidha. Wakati huu kunao waliona hofu kuwa itaporomosha uchumi(GDP per Capita) na kuwa hali ya usalama DRC sio ya kuridhisha na mwisho kuwa rasilimali zake za madini zitavamiwa na nchi zingine za Jumuiya. Kwanza Kuporomoka kwa GDP per Capita hakufai kuwa hoja kabisa kwa sababu uwezo wa kiuchumi wa DRC bado haujaanzishwa wacha kutimizwa. Pili katika usalama, DRC itakuwa better off ndani ya Jumiya kuliko inje ya jumuiya. Nchi ambazo zimechangia katika mizozo ya usalama na vita nchini DRC ni majirani wa DRC na moja wapo ya nchi za Jumuiya. Kumekuwa na mizozo kati ya nchi za Jumuiya lakini hakuna vita vilivyotokana na mizozo hiyo. Kwa mfano kumekuwa na mizozo ya kiusalama kati ya Rwanda na Burundi, Rwanda na Uganda na migogoro ya kidiplomasia na uchumi kati ya Kenya na Tanzania lakini hakuna ule mzozo ulioleta tishio kwa Jumuiya au vita ndani ya Jumuiya kwa miaka ishirini sasa. Migogoro ndani ya Jumuiya itaendelea kuwa lakini haifai kufwanywa kimasksudi au kwa kiwango cha kutishia Jumuiya. Kwa maono yangu ningependekeza kuwepo na ofisi ya ubalozi ya Jumuiya ambayo itasimamiwa na Balozi wa amani, Usalama na mahusiano mazuri (peace, security and good relations) ambaye atakuwa anafanya shuttle diplomacy na kubisha hodi katika nchi yeyote ya Jumuiya ili kutimiza malengo yake na kutoa mapendekezo na riporti ambayo itatumiwa kufanya majadiliano au maamuzi ya ufahamu mwema (informed decision). Kumbuka mkataba wa Jumuiya inasema kuwa kunapaswa kuwa na ujirani mwema na utatatuzi wa migogoro kwa njia ya diplomasia. Kungekuwa au kukiwa na ofisi au kitengo huru cha ubalozi huu Uganda na Rwanda hawangeenda kuutatua mzozo wao kule Angola, mzozo kati ya Rwanda na Burundi ungeshughulikiwa na Jumuiya badala ya kupuuzwa. Lakini hilo ni pendekezo tu.

Hofu ya rasilmali za DRC kuvamiwa na nchi za Jumuiya ni halali lakini haipaswi kuwa. Ni ukweli kuna wale ambao wako na ulafi kwa haya madini lakini idadi yao ni chache kuliko wale ambao watakuwa na mtazamo wa kutoingila na kuvamia rasimali hizo kinyume na mapendeleo ya WanaDRC. Kumbuka maamuzi ya Jumuiya yanafanywa kwa njia ya makubaliano (consensus) kumanisha kuwa inahitaji mmoja anayetofautiana kuweka wengine kiukweli.

Kwa haya na mengi yaliyotajwa awali, Jumuhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo wakubaliwe kuingia Jumuiya jana sio leo wala kesho. DRC ni kama msichana mzuri aliyetayari kuenda date lakini ndio sisi hao tunataka kumfanya awe wa kungoja. Anaweza kubadilisha maamuzi yake na akatae kuenda date na Jumuiya kabisa kwa hizo ngoja ngoja. Kwa sababu ya DRC kuwa na strategic importance ya kuunganisha Jumuiya na Bahari ya Atlantic, DRC isikataliwe au kuwekwa pembeni bali wakubaliwe kujiunga na Jumuiya.
map.jpg
map.jpg
sgr.jpg
 
Hapo kwenye Tz na Kenya kupinganapingana sababu tunafanana sana ni kweli kabisa, kwenye saikolojia wanaita Narcissism of small differences. Tz na Kenya tungejua ushindani wetu ni psychological na tukaamua kuwa na sauti moja tusingeshikika. inabidi Chige na Wick na Denvers waione hii nondo.

Mkuu Red Giant unaona kinachoendelea saa siku za hivi karibuni: Kuna mambo mengi ambayo nadhani ni lazima Tanzania na Kenya wakae wayamalize kiuungwana na kindugu. Tanzania ni eneo la muhimu sana ambayo huzalisha chakula kinacholisha maeneo mengi ya Afrika Mashariki: Nadhani hatukutakiwa kuitumia hii nafasi yetu vibaya (Weaponizing Trade) kama silaha ya kisiasa.

Nakumbuka hapo mwanzoni niliwahi kusema kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki haitakiwi ijitanue tena kwasababu ina matatizo lukuki, na moja kati ya hayo matatizo ni Lack of Food Security kama ambavyo imedhihirika siku za hivi karibuni. Kama mwanachama wa jumuiya anaenda kuagiza maelfu ya kilomita kuagiza chakula ambacho kingepatikana kwa jirani yake basi jua kwamba kuna walakini mkubwa sana kimahusiano.
 
Habari wandugu. Inaonekana sasa hakuna tena cha kuzuia DRC kujiunga na ESC. Ujumbe wa EAC upo huko Goma kuangalia kama DRC imekizi vigezo. Na vigezo vikubwa ni.

1. Kupakana na EAC
2.Utayari na uelewa wa viongozi kuhusu haki na wajibu wa member wa EAC
3.Taasisi imara

Kuhusu usalama nimemsikia mjumbe mmoja akisema kuwa anategemea DRC kuwa imara zaidi ndani ya EAC.

Nafikiri sasa inatakiwa tujadili ni jinsi gani watanzania tunaweza kufaidika na ujio wa DRC ndani ya EAC.

Binafsi ntaongea jambo ninaloongea kila siku. Serikali irahisishe upatikanaji wa passport. Urasimu usiwepo. Bei iwe hata 50,000 na pia kigezo cha kupata kiwe kadi ya NIDA tu. Hatuwezi kuzitumia fursa hii vizuri kama hatutarahisisha watu kwenda kuzitumia.
Kwako MALCOM LUMUMBA
 
Hii jumuiya tulikuwa tukikosa nini ambacho sasa tunaweza kukipata kupitia hiyo jumuiya au toka irejeshwe sisi wananchi tumenufaika na nini kutokana na hiyo inayoitwa jumuiya.
 
Usiige kunya kwa tembo utachanika suezi kanali! Tulishindwa EAC ya mataifa matatu je mataifa nane tutaweza? kila raia atakimbilia Tanzania eti kuna usalama na utulivu kisingizio!Bara na visiwani tuu hakieleweki vizuri je nchini somalia utatanua kweli?kumbuka nchi ambazo hazina wakristu duniani ni Somali na saudi arabia.unakumbuka jinsi msomali alivyo waua wakristu pale wategate Kenya? eti kama wewe mkristu anakuua ila muislamu hakuuwi! Hii ni CV ya kuwakatalia kabisaa hawa maadui wa Dini ya emanueli!
 
Mkuu Red Giant nilitoa ahadi ya kurudi na sasa nimerudi na nitachangia kidogo juu ya hii mada ambayo ni muhimu kabisa. Nitatoa maoni kama Mwanasiasa, pia nitatoa maoni kama Mwanasheria. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada:

Congo DRC isitengwe bali isiruhusiwe kuingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwasababu itaongeza changamoto ambazo tayari EAC inazo na imeshindwa kuzimaliza kwa muda mrefu. Changamoto kubwa ni hii ifuatayo hapa chini:

Mosi, nchi wanachama wa EAC wanakumbwa na matatizo ya kisiasa ndani ya nchi zao ambayo kwa namna moja au nyingine yameugharimu huu ukanda muda na rasilimali nyingi ambazo zingewekezwa katika kufanya mambo ya msingi.

Uganda mpaka leo wanapigana na waasi wa Lord's Resistance Army wa Bwana Joseph Konyi. Upande wa pili kuna sintofahamu kubwa sana kwenye siasa zake za ndani na hatufahamu nini kitatokea nchini humo baada ya Raisi Museveni kutoka. Tunaweza kuhisi kwamba Uganda iko salama lakini kumbuka tangu nchi hiyo inapata uhuru hakujawahi kuwa na Raisi ambaye hajatoka kwa vimbwanga na kusababisha kuchafuka kwa hali ya kisiasa nchini humo kuanzia Mutesa hadi Obote.

Rwanda nayo mpaka sasa iko kwenye vita isiyoisha na makundi ya waasi wa Kihutu ambao wako Congo DRC na duniani kote. Hivi karibuni siasa ya Rwanda imegubikwa na kiza kikali baada ya kusemekana kwamba kuna Watutsi ambao waliwahi kuwa ndani ya Serikali ya Raisi Paul Kagame wameunda mtandao mkubwa wa kutaka kumpindua. Rwanda kama nchi inaenda vizuri kwasasa lakini bado kuna sintofahamu kubwa kama Uganda ambako mpaka leo hawana uhakika na Smooth Transition of Power after the fall of their strongmen.

Burundi mpaka sasa unafahamu nini kimekuwa kinaendelea tokea mwaka 2015, na bado nako kuna sintofahamu kubwa sana na Serikali ya Raisi Nkurunzinza iko nje-ndani.

Tanzania na Kenya hazijatofautiani sana. Zimefanikiwa sana kwenye suala la Smooth Transition of Power hivyo kufanikiwa kukwepa sintofahamu nyingi za kisiasa ambazo zimewakuta mataifa ya jirani. Japo upande wa pili bado Kenya ina changamoto kubwa za kiusalama ambazo zimemfanya apoteze rasilimali nyingi sana kule Somalia akipambana na kikundi cha Al Shabaab huku Tanzania ikiwa inapita kwenye kipindi kigumu kisiasa ambacho pia kinaweza kuzaa sintofahamu kubwa sana huko mbeleni kama siasa yake itaendelea kwenye njia hii.

Ninachotaka kusema kwenye hoja hii ni hiki hapa: EAC iliundwa kama Jumuiya ya kiuchumi na siyo ya kisiasa. Haya ya siasa kama kuunda shirikisho ni malengo ya baadae sana (Future Objectives) ambayo hayatakiwi kuwa kwenye ajenda yoyote kwenye kipindi hiki.

Lengo kuu na ajenda ya sasa (Main and Primary Objective) inabidi iwe ni Uchumi kupitia soko la pamoja na sarafu moja. Kama tukifanikiwa kujenga uchumi wa pamoja basi ndiyo mambo ya siasa yaanze kuingia kwenye ajenda za vikao vyetu. Sasa machafuko ya kisiasa huwa yanatutoa kwenye mstari maana hutulazimisha kuacha kufanya mambo ya kiuchumi na kujiingiza kwenye siasa, kitu ambacho siyo lengo letu kama EAC kwasasa.

Tokea EAC iundwe tumekuwa tukitatua matatizo ya kisiasa yanayogharimu rasilimali nyingi kuliko kufanya mambo muhimu: Tunalazimika kufanya hivyo kwasababu ni majirani zetu lakini haswa kwasababu ni wanajumuiya wenzetu. Tulianza na Kenya mwaka 2007-2008: Kenya na Alshabaab 2012:Tukaja Rwanda na Tanzania mwaka 2013: Burundi mwaka 2015: Uganda na Rwanda 2019. Sasa tukiileta DRC na ilivyo na matatizo lukuki basi fahamu kwamba tutabeba na changamoto zao kuanzia uchaguzi hadi waasi wa Kagame na Museveni.

Pili, Congo DRC kama nchi imeshaigharimu SADC ambayo ilijiunga mwaka 1997 punde tu baada ya kumtoa Mobutu Sese Seko madarakani. SADC ilijikuta inatumia muda mwingi sana kushughulika na CONGO DRC badala ya kujikita kufanya mambo ya msingi. Ikumbukwe Mzee Kabila alivutana sana na viongozi wenzake wa SADC pale alipotaka wamsaidie kupambana kwenye The Congo War lakini wakawa wanasuasua. Wakina Quett Masire wanataka kumsuluhisha, yeye Kabila akawa anasusia vikao. Unadhani nchi kama hii ikijiunga na EAC na ikapatwa na tatizo tutakwepa kweli kuhusika ???

Tatu, wengi tunatamani Congo DRC ijiunge EAC kwasababu ya rasilimali zake. Basi kama itajiunga na EAC itageuzwa rasmi kuwa kichaka cha mashindano ya wizi wa rasilimali (Mineral Race) zake baina ya nchi wanachama wa EAC. Mfano hai tu, Umoja wa Mataifa (UN) waliwahi kutoa taarifa ya uchunguzi kwamba kipindi cha Vita ya Congo Zimbabwe ilipewa na serikali ya Laurent Kabila malipo ya dola za Kimarekani Bilioni 5 ambazo zimetoka kwenye hazina ya mali mbalimbali za watu wa Congo DRC. Haya malipo yalienda sambamba na mikataba ya madini na mafuta ambayo Zimbabwe na Angola waliipata kwa kumsaidia Kabila.

Upande mwingine inasemekana mataifa ya nje yalifanya ujangiri na kuua zaidi ya tembo 12,000 kwenye mbuga ya Garamba. Umoja wa Mataifa uliilaani Rwanda na Uganda kwa kuiba maelfu ya rasilimali za watu wa Congo DRC kwa kisingizio cha kupigana na waasi.

Sasa hii ilikuwa miaka ya 1999-2003, unadhani DRC ikijiunga rasmi na EAC Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda watakaa tu kuziangalia zile rasilimali ??? Utatokea mvutano mkubwa sana baina yetu kuanzia kwenye uchaguzi wa DRC maana kila nchi mwanachama atataka aweke kwenye serikali mtu ambaye atakuwa na ushawishi mkubwa sana kwake: Rwanda na Uganda pamoja na uswahiba wao mkubwa walishawahi kupigana kisa kugombania rasilimali za Congo DRC. Sasa Congo DRC ijiunge na EAC hapo wakaongezeka Tanzania na Kenya unadhani kutakuwa na utulivu ???

Mfano mwingine ,angalia kilichotokea Burundi mwaka 2015 pale ambapo Tanzania na Rwanda walipogombania ushawishi kwa serikali ya Bujumbura. Sasa piga picha Burundi alikuwa hana utajiri wowote ule, unadhani Congo mwenye utajiri atatuacha salama ???

Sisi Tanzania tuna utajiri mkubwa ambao Mungu ametupa na itakuwa ni ujinga kama tutataka Congo DRC iinge EAC kwasababu ya utajiri wake. Japo kimkakati (Strategically)ni jambo sahihi, lakini tatizo linakuja kwamba pale ambapo hatuna mpango maalumu wa nini tutafanya na Congo DRC baada ya kuwa karibu na sisi. Hivyo tuiache tu na tusitafute matatizo yasiyo na ulazima wowote ule: Pia tusichume dhambi with this Imperialistic Mindset....

NINI KIFANYIKE KUHUSU CONGO DRC?

Hapa nitatoa maoni kama mwanasiasa:
Mosi, EAC ijikite kwenye kuimarisha taasisi zake yenyewe (Consolidation and Amalgmation of it's Institutions) na siyo kujitanua (Enlargement of the bloc) kwa kutafuta au kuruhusu wanachama wapya.

EAC imeiga vitu vingi kutoka European Union (EU) ambayo zamani ilikuwa ni European Economic Community (EEC) lakini haifanyi vizuri kama ambavyo EEC ilifanya. Umoja wa Ulaya ulianza kama Umoja wa Uchumi (Economic Union) na siyo Umoja wa Kisiasa (Political Union), lakini baadae ndiyo ukafika hapa ulipo. Ulipitia hatua mbalimbali.

Ulianza kutengeneza kitu kinachoitwa The European Coal and Steel Community mwaka 1951 ambayo ilikuwa ni taasisi iliyoundwa kwa lengo la kuhakikisha makaa ya mawe na chuma vinasimamiwa na Chombo/Taasisi moja ya kimataifa inayojitegemea ili kuzuia mvutano baina ya nchi kubwa kama Ujerumani na Ufaransa ambao ulipelekea kutokea vita vya kwanza na vya pili vya dunia.

Aliyesuka huu mpango anaitwa Jean Monet ambaye alisema ili tuweze kujenga umoja imara ni lazima tuhakikishe mataifa yenye nguvu na rasilimali nyingi ya Ujerumani na Ufaransa yanaungwanishwa kiuchumi kiasi kwamba nchi yeyote haiwezi kufikiria kwenda vitani na mwenzake. Kweli walifanikiwa sana maana mkataba huu ulisainiwa na mataifa sita (Ujerumani Magharibi, Ufaransa, Italia, Ubelgiji na Luxembourg) hata yale ambayo yalikuwa hayana rasilimali kama Ubelgiji na Luxembourg walinufaika.

Mwaka 1957 wakasaini mkata wa kuunda taasisi nyingine iitwayo The European Atomic Energy Community ambayo kazi yake ilikuwa kuzimamia uzalisha wa nishati ya nyuklia Ulaya ili kuwasaidia wanachama kupunguza utegemezi kwenye mafuta, pia kuuza nishati ya akiba kwa mataifa yasiyo wanachama. Hili nalo walifanikiwa sana.

Mwaka 1957 wakatengeneza sasa Umoja wa Uchumi wa Ulaya ambao leo ndiyo Umoja wa Ulaya. Lakini hawakuwa na haraka na hili liliwezekana kwasababu wao walikuwa na hali nzuri ya kisiasa nchini mwao. Mwaka 1967 taasisi za European Economic Community, European Steel and Coal Community na European Atomic Energy Community ziliungwanishwa kuwa chombo kimoja. Biashara baina ya nchi wanachama ilikuwa kwa asilima 28.4% hadi kuwashangaza Muingereza na Marekani.

Hawakukimbilia kujitanua bali walijijenga kwanza wao kiuchumi na kisiasa kabla ya kuhakikisha wanayakaribisha mataifa mengine kama Uingereza mwaka 1973. Japo wanafanya vizuri lakini bado wana matatizo sana, Raisi wa Ufaransa Charles De Gaulle miaka ya 1969 hakupenda Uingereza ijiunge na EEC kwasababu alisema italeta matatizo kwenye jumuiya hivyo alipinga sana hadi anafariki.

Uingereza aliruhusiwa kujiunga baada ya De Gaulle kufariki. Lakini mbali na yote yale siasa za Uingereza zimeutikisa Umoja wa Ulaya kama ambavyo De Gaulle alionya akisema Muingereza anawakilisha maslahi ya Marekani. Sasa Uingereza taifa lililoendelea sana kuliko Congo DRC matatizo yake ya ndani yamevuruga Umoja wa Ulaya unadhani ni busara kuleta tena mgeni ???

Hapa hoja yangu ni hii: Kichwa na Moyo wa EAC ni Kenya na Tanzania wala siyo rasilimali za Congo DRC. Kama tunataka EAC imara basi ni lazima tuhakikishe Kenya na Tanzania zinaelewana na kuzungumza lugha moja. Maana binafsi naamini ushawishi wa Kenya na Tanzania wakiwa wanaongea lugha moja ni hatari kuliko mlipuko wa bomu la kiatomiki na hakuna taifa la Afrika linaweza kuwashinda. Raisi Kwame Nkhuruma alilifahamu vizuri hili suala ndiyo maana alipinga sana EAC isiwe nchi moja.

Kenya na Tanzania wakiungana basi lazima Uganda, Rwanda na Burundi watafuata tu. Kenya na Tanzania zina Uchumi mkubwa, ushawishi mkubwa sana kikanda na kimataifa, zimekaa pazuri sana kijiografia, zina rasilimali nyingi na zina watu wengi wanaozungumza lugha moja ya Kiswahili. Wakenya na Watanzania hawapatani kwasababu wamefanana mno tabia, fanya uchunguzi utaligundua hili.

Mtifuano wa kiuchumi na kihistoria baina ya Kenya na Tanzania ndiyo unavuruga EAC. Tunafanyiana hujuma badala ya kuunganisha nguvu za kitaasisi ili tujikwamue hapa tulipo. Hujuma kwenye kilimo, hujuma kwenye bandari na hujuma kwenye viwanda bila kufahamu kwamba Afrika Mashariki yote tunaweza kuwa Mamlaka moja ya Bandari ambayo ingetusaidia sana.

AU tungeweza kuanzisha Joint Venture Agreement kupitia Special Purpose Vehicle kwenye kuratibu biashara ya Usafiri wa anga. AU tukaunganisha nguvu kwenye tafiti za Uchimbaji wa mafuta na gesi (SPV) mbona tungefika mbali sana tu. Wazungu walitwangana ndiyo wakapata akili kwamba kumbe tunaweza kushirikiana bila mabomu na vifaru.

Lakini sisi tunataka kushindana kisa kulipizana visasi vya ugomvi wa Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere. Leo hii kwa mitandao ya kibiashara ambayo Kenya na Tanzania tunayo kupitia nguvu za diplomasia za nchi zetu kama tukishirikiana sauti yetu itafika hadi mwisho wa dunia. Nashangaa kwanini hatulioni hili. Binafsi Kenya and Tanzania are the Key, ndiyo maana hata Rwanda, Burundi na Uganda walipovutana hakikutokea kitu kikubwa sana: Lakini Kenyatta na Jakaya walipovutana EAC iliyumba. Hujiulizi kwanini ???

Pili, na mwisho kabisa natoa ushauri kama mwanasheria sasa: Congo DRC asiwe mwanachama ila aidha apewe nafasi ya mtazamaji (Observer Status) kwanza ndani ya EAC huku akijifunza mwenendo mzima wa EAC. Sambamba na hilo EAC tunaweza kusaini mkataba maalumu na Congo DRC (Sui-Generis Treaty) ambao utampa nafasi ya kipekee kunufaika kiuchumi bila kuwa mwanachama. Anaweza akaandaliwa vipengele (Extracts Clauses with Limitations ) kutoka mikataba mbalimbali (Protocols) ambayo EAC ameshasaini. Anaweza kufanya kama ambavyo Uingereza na Umoja wa Ulaya walifanya miaka ya 1960's- 1970's au ambavyo wanataka kufanya baada ya Brexit.

Tujijenge kwanza sisi ndiyo turuhusu waliovurugwa kama Congo DRC wajiunge.
Moronight walker maoni yangu niliyatoa hapa. Nitakachoshauri leo hii ni kutojihusisha kabisa na hizi siasa za Rwanda, DRC, Kenya na Uganda. Tanzania haiwezi kubadilisha chochote kwenye huu mgogoro.
 
Back
Top Bottom