Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu

Mungu wetu uliyejuu mbinguni tunakuomba umzibe mdomo huyo Cyprian Musiba kwa namna unavyojua wewe hakika kiumbe chako hichi kinaleta ufisadi ma uharibifu katika nchi yetu

Ewe Mungu tupokelee maombi yetu

Amiin.
 
Mkuu'
Mwananchi yeyote mzalendo, Mwananchi yeyote Mzalendo hawezi kuachia mawazo yake na maneno yake ya "kugawa' matabaka ya kijamii kwa kisingizio cha Uharakati na Uzalendo. Ni sawa tu na kugawa kidini, kikabila n.k

Binafsi naona hili sakata ni la Kimatabaka (social class warfare)matabaka huwa yanatokea-matokeo ya maendeleo ya kijamii na ndoa za tamaduni mpya-kwa maoni yangu sakata hili ni dalili hizo na matunda yake.

Mkuu pole sana, tabaka lako linachangia mwanga kule kusipoonekana. Limethibitishwa kimataifa! na vile vile ni kupongeze sana sana kwa CPJ award. MERITUS

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Aluta Continua
 
Musiba kila siku anaibua tuhuma nzito tena kwa maandishi kupitia magazeti yake. Kwanini haitwi kuhojiwa? Yeye ni nani katika ardhi hii ya Jamhuri Ya Muungano ea Tanzania?

Akituhumu yanayomhusu, watajwa wanaitwa ila akituhumu wengine anaonekana yuko SAWA.
 
Kwa maoni yangu ujenzi wa jf ni mchango mkubwa sana ambao umeutoa kwa Taifa letu.

Nakushauri achana na wanasiasa na makundi yao let them be and and do what they see right.

Wewe jikite kuendelea kuidumisha na kuiboresha JF. Nasema hivi kwa sababu kwa hatua uliyonayo sasa kila mwanasiasa atatamani kukutumia kwa maslahi yake na kundi lake bila kujali madhara atakayokuachia.

I stand to be corrected.
 
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?
Mkuu Musiba n msiba TU kwa Sasa katika nchi hii

Alimtegemea mtu ambaye naye alitegemea waganga akasahau kuna Mungu wa mbinguni bwana wa majeshi JEHOVA
 
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence

Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, ahojiwa kwa tuhuma za kula njama za kutaka kumuua Cyprian Musiba - JamiiForums
Mfungulie kesi uvute hata one B akome na kukomaa
 
Mkuu unasubiri nini kumfungulia mashita huyu shetani? Hafai
 
Hawajui tu kuishambulia JF nikuishambulia nchi nzima na wao wanajishambulia.

Hao polisi bila shaka walisema ni kwanini hawamuhoji Musiba ambaye ndiye mleta tuhuma na kwa.mujibu wa sheria mleta tuhuma ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisa tuhuma zake.

Sote tunaelewa lengo la awamu hii ya tano.

Tuko.pamoja endelea kupambana utashinda, Mungu yuko pamoja nasi. Huyo.Musiba ipo siki atabaki peke yake.
Awamu ya shetani
 
Back
Top Bottom